Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Viongozi wakuu wa Chadema wamefika uwanja wa Uhuru leo saa moja asubuhi ndipo wakazuiwa kuingia wakiambiwa wasubiri kwanza utaratibu.

Ilipofika saa tatu asubuhi viongozi kadhaa walianza kumiminika na kuruhusiwa kuingia uwanjani huku viongozi wa Chadema wakiwa bado getini.

Rais alipofika akaingia ndipo viongozi wa Chadema wakaambiwa hakuna tena kuingia uwanjani.

Ndipo nasema sasa kila mtu afanye shughuli yake ili mradi hatutavunja katiba.
Wala hawahitajiki waendelee na Saccos yao. Wanataka sifa si ulimsikia msaliti alivyosema jana alipokuwa pale Ufipa?
 
Çhadema mpo kama Watoto
Na mnajiona watu maalumu nchi hii
Kila mahali mnaingiza Siasa
Muache Upuuzi
 
Msafara wa Viongozi Wakuu wa CHADEMA, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Freeman Mbowe, wamezuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru walikokuwa wameenda kuhudhuria shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kumuaga Rais Mstaafu wa Awamu Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa.

Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Mbowe aliongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Bara), Mhe. Tundu Lissu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mhe. John Mnyika, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee, Mhe. Hashim Juma Issa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama, Mhe. Suzan Kiwanga na viongozi wengine waandamizi kutoka Makao Makuu ya CHADEMA, Viongozi wa Kanda 10 za chama, Viongozi CHADEMAwa Mikoa, Wilaya na Majimbo mbalimbali nchi nzima.
View attachment 1519379
Kutoka Uwanja wa Uhuru hapa, Dar es Salaam.
Wanaleta siasa hao hata kwenye msiba. Waende zao huko ufipa.
 
Kwanza Chadema walikuja na magari wakati serikali ilitangaza Watu wasije na magari

Halafu hawajui protocol. Kuwa Huwezi ingia na gari ndani ya uwanja Ni ya viongozi tu wa serikali wa kitaifa wanaoruhusiwa kuingia na magari hata viongozi wakuu wa dini hawaingii mule na magari Sasa wao wakaja na gari zao za mikopo walizokopa bungeni eti wanataka kuingia na magari Yaao waliyokopa bungeni!! Hata vibaka tu wa temeke wanajua kuwa Huwezi ingia na magari Kama si.kiongozi wa serikali wa kitaifa .Wao hata Hili tu hawajui
 
Pamoja na ukongwe wako humu JF haya majibu ni kama umejiunga June 2020...
Umekasirikia mambo kuliko yale yanayokasirisha! Wewe na ukongwe wako umeonyesha gubu! Toa ushauri, achana na maneno ya kwenye kanga. Mbona huyo kiazi misasa nimelike comment yake ambapo hakuongea ushuzi?
 
Msafara wa Viongozi Wakuu wa CHADEMA, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Freeman Mbowe, wamezuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru walikokuwa wameenda kuhudhuria shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kumuaga Rais Mstaafu wa Awamu Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa.

Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Mbowe aliongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Bara), Mhe. Tundu Lissu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mhe. John Mnyika, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee, Mhe. Hashim Juma Issa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama, Mhe. Suzan Kiwanga na viongozi wengine waandamizi kutoka Makao Makuu ya CHADEMA, Viongozi wa Kanda 10 za chama, Viongozi CHADEMAwa Mikoa, Wilaya na Majimbo mbalimbali nchi nzima.

Kutoka Uwanja wa Uhuru hapa, Dar es Salaam.
The fear reaction of the people. Lissu angeshangiliwa na kuwa aibu kwao
 
Civilisation ingeoneshwa jana.
√ Wakati nchi jirani wamepeperusha bendera zao za Taifa nusu mlingoti, CHADEMA walizipeperusha kwa bwembwe kumlaki Makamu wa M/Kiti wao;
√ Badala ya mtia nia ya Urais kwenda kutoa rambirambi kwa familia ya mfiwa, aliona ni bora ahutubie waliomlaki tena kwa lugha ya kejeli dhidi ya Serikali na marehemu (akilenga jumuia ya kimataifa kupitia vyombo vya habari vilivyokaribishwa kwa makusudi hayo);

Au mnaamini WaTz ni wajinga kama walivyoonesha wanachama na wafuasi wa CHADEMA jana, wakati kwa mila na desturi za kiafrika, msiba hupewa uzito mkubwa kijamii na kisiasa.

CHADEMA kitavuna kilichopanda jana.
Lissu ni mtu wa pekee sana na mwenye roho ya kipekee ..... may be Roho kama za akina Mandela.

Baada ya kumwagiwa risasi zote hizo na kutibiwa kwa miaka mitatu bado anaweza kuongea bila hasira na kwa tabasamu pana ....!!
 
Viongozi wakuu wa Chadema wamefika uwanja wa Uhuru leo saa moja asubuhi ndipo wakazuiwa kuingia wakiambiwa wasubiri kwanza utaratibu.

Ilipofika saa tatu asubuhi viongozi kadhaa walianza kumiminika na kuruhusiwa kuingia uwanjani huku viongozi wa Chadema wakiwa bado getini.

Rais alipofika akaingia ndipo viongozi wa Chadema wakaambiwa hakuna tena kuingia uwanjani.

Ndipo nasema sasa kila mtu afanye shughuli yake ili mradi hatutavunja katiba.

Mkuu Gsam viongozi wa Cdm hata wangeenda hapo uwanjani saa 11 asubuhi, bado wasingefurahiwa kuwepo hapo uwanjani, hasa hasa Lisu. Ni nani asiyefahamu uhasama uliopo baina ya Lisu na Magufuli? Hivi viongozi wa Cdm hawawezi kujifunza tabia za mtu na kujua wachukue maamuzi gani?

Kulikuwa na haja gani ya viongozi wa CDM kwenda kwenye huo msiba? Hivi ni kweli hamjui baadhi ya hatua na madhila wanayoyapata cdm hivi sasa yalikuwa na baraka za huyo Mkapa? Ni lini huyo Mkapa aliwahi kujihusisha na misiba ya cdm? Huyo Tundu Lissu alipigwa risasi nusura kufa, Mkapa aliwahi hata kutoa pole? Alithubutu hata kwenda kumtembelea? Jana kuna post nilishauri huru, kwamba Lissu asiende kwenye huo msiba, haya mnayosema humu ndani, mbona yalikuwa ni dhahiri yatatokea?

Cc: Mwengeso
 
Umekasirikia mambo kuliko yale yanayokasirisha! Wewe na ukongwe wako umeonyesha gubu! Toa ushauri, achana na maneno ya kwenye kanga. Mbona huyo kiazi misasa nimelike comment yake ambapo hakuongea ushuzi?
Duh!

Nimekuwa kiazi mkuu? Any way shukran
 
Civilisation imewapitia mbali sana MATAGA!

Usishangae wakaambiwa wameandamana bila Kibali.

Ubaguzi huu sasa unahamia mpaka kwenye misiba na ipo siku utakwenda zaidi ya hapo.

Ya jana yamewaumiza, na hizi ndio hasira zao.

Hatari ya uamuzi huu ni msiba kuchukua sura ya kisiasa na matokeo yake watu wanaweza kususa kushiriki ikiwamo kuondoka msibani kwa waliokwisha kufika.

Ila kama kuna sababu ya msingi ya kuwazuia,tuambiwe.
Kwani si toka Jana mshereheshaji alisema kutakuwa na mabasi maalum ya kuingia uwanjani kwa wageni maalum sasa wao kiranga gani cha kwenda na vitetenasi vyao kiwanjani? wangeenda kwa mguu mguu wangezuiwa ndio mngekuja kulialia humu.
 
Back
Top Bottom