Msafara wa Viongozi CHADEMA wazuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru kumuaga Mzee Mkapa. Waitaka Serikali itoe maelezo...

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Msafara wa Viongozi Wakuu wa CHADEMA, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Freeman Mbowe, wamezuiliwa kuingia Uwanja wa Uhuru walikokuwa wameenda kuhudhuria shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kumuaga Rais Mstaafu wa Awamu Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa.

Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe. Mbowe aliongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Bara), Mhe. Tundu Lissu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mhe. John Mnyika, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee, Mhe. Hashim Juma Issa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama, Mhe. Suzan Kiwanga na viongozi wengine waandamizi kutoka Makao Makuu ya CHADEMA, Viongozi wa Kanda 10 za chama, Viongozi CHADEMAwa Mikoa, Wilaya na Majimbo mbalimbali nchi nzima.



Kutoka Uwanja wa Uhuru hapa, Dar es Salaam.

=====

UPDATES:

CHADEMA yaitaka Serikali itoe maelezo kwanini viongozi wake wakuu wamezuiwa kumuaga hayati Benjamin Mkapa!


1595936763201.png
1595936780906.png
 
Civilisation imewapitia mbali sana MATAGA!

Usishangae wakaambiwa wameandamana bila Kibali.

Ubaguzi huu sasa unahamia mpaka kwenye misiba na ipo siku utakwenda zaidi ya hapo.

Ya jana yamewaumiza, na hizi ndio hasira zao.

Hatari ya uamuzi huu ni msiba kuchukua sura ya kisiasa na matokeo yake watu wanaweza kususa kushiriki ikiwamo kuondoka msibani kwa waliokwisha kufika.

Ila kama kuna sababu ya msingi ya kuwazuia,tuambiwe.
 
Back
Top Bottom