Msaada tutani: Ndugu yangu Wa kiume ana tabia za kike, suluhisho la hili tatizo ni nini?

Balqior

JF-Expert Member
Jun 8, 2021
1,712
5,700
Nilikuwa simfahamu huyu ndugu yangu, ni mtoto wa mama mdogo, nimemfahamu juzi kwenye family gathering event😭ni damu yangu kabisa halafu kijana, mara ya kwanza nlivomuona tabia zake, na jinsi anavotembea, Nilipata mashaka nikahisi kuna kitu kimempungukia kama mwanaume.

Nlivyokuja kuongea naye sasa oh gosh 😭😭anavoweka mikono, vidole, halafu body language yake anajishebedua kwa pozi za kike kabisa, halafu Muda mwingi alikuwa anashinda jikoni na dada zake sijui wamemzoea.

Nikamvuta pembeni dada yake mmoja kuonyesha mshangao wangu, nikamwambia hili ni janga kwenye familia yetu, akaniambia In very simple way ni shida tu ya homoni..

Kuna waliowahi kuwa na Tatizo hili au ndugu wenye tatizo hilo halafu likarekebishika? Kingereza linaitwa "effeminacy" Maana Nimegoogle nikaona mwanaume kuwa hivyo na tabia za kike haimaanishi kuwa ni shoga, ila kuna uwezekano Mkubwa wa yeye Kuja kuwa shoga.

Janga hili kwenye familia yetu😭😭
 
Kama ana upungufu wa testosterone zipo tiba ila nae aanze kujitoa huko I mean akubali kwa hiari yake.. maana hiyo tiba inahitaji na kujitoa pia sio kudungwa misindano tu.

Mpeleke kwa mtabibu wa homoni wapo mahospitalini
 
Nimewahi kusoma na mtu kama huyo sekondari. alikuwa anatumia muda mwingi sana na wasichana. Atakuwa pamoja na sisi bwenini tu ambako hamna wakike.

Ongea yake na hata tembea Yake ni ya kike. Alikuwa tofauti kabisa na sisi wenzake wa kiume. Ila mawazo ya ushoga hayakuwa kabisa kichwani mwangu kumuhusu.

Ila kwa sasa haya mambo yamekuwa yanaongelewa sana mpaka namkumbuka jamaa.
 
Nilikuwa simfahamu huyu ndugu yangu, ni mtoto wa mama mdogo, nimemfahamu juzi kwenye family gathering event😭ni damu yangu kabisa halafu kijana, mara ya kwanza nlivomuona tabia zake...
Mkabili umuulize tatizo ni nini. Jaribu kumshauri atafute bibi utajua ukweli kwa atakavyochukulia suala hili. Jenga urafiki naye na umpeleke kwenye maeneo yenye mabinti ataingia box kirahisi au kutema na kujua kuna namna ambapo itabidi uanza uchunguzi upya.
 
Unakuta mzazi ana watoto wa kike 3 na wakiume 1 halafu wote anawaweka gate kali mpaka wanafikia balehe. Katika mazingira kama haya lazima huyu mmoja atakua na tabia za hao watatu.
mkuu hii naipa asilimia chache sana ni ngumu kunakili tabia za kike au kiume kama homoni zipo sawa! Nikajua utapata hofu za wao kulana!,about our sexual behaviours we do programmed inside.
 
Akiendelea shids huwaga wauni wanakuja wanamrarua kweli, na hapo ndio wanapomuingiza shimoni. Maana utabia wa kike, akionjeshwa ukike unavyokua ndio anaishiamo humo humo. Muwahi kuna wahuni mazombie, wanapenda kweli vijana wanaojifanya wa kike.
 
Kuna dogo nilisoma na primary alikuwa the same kuanzai kuongea kutembea kula kitu ni cha kike hata marafiki zake ni wa kike. Ila sijawahi kusikia akijihusisha na ushoga mpaka tunamaliza shule ya msingi hadi sekondari ila kama aliendelea na hali ile mpaka ukubwani sidhani kama wajuba walimwacha salama
 
Nilikuwa simfahamu huyu ndugu yangu, ni mtoto wa mama mdogo, nimemfahamu juzi kwenye family gathering event😭ni damu yangu kabisa halafu kijana...
Hii isikie kwa wenzako tu ila kama unandugu au mtu wako wa karibu alafu awe na tabia kama za kike wakati ni wakiume sijui au wa kike awe na tabia za kiumwe dah inaboa..

ila ndo ndugu yako sasa unabaki tu kujikaza alafu sasa unakuta dada zake wala wanafurah tuna kukenua mimeno pamoja nae ndio wanamuaharibu kabisa..
 
Inasikitisha sana Kuna dogo mmoja songea yaaani Kila kitu ni kama mwanamke, Cha ajabu amepewakibarua kwenye booking office Moja ya mabus kampuni kubwa tu...... Yaaani nikama demu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom