Jana kulikuwa na malumbano ya hoja ikihusu TATIZO LA UHABA WA SUKARI KUJIRUDIA KILA MARA NA KUYUMBISHA BEI SOKONI, NINI SULUHISHO LA KUDUMULA KUTATUA TATIZO HILI? Waalikwa walikuwa kutoka Bodi ya sukari, kutoka Wizara ya Kilimo na wote waliingia mitini.
Yaliyozungumzwa pale yanatisha. Kumbe wanaotawala uagizaji wa sukari ni wafanyabiashara wachache na wanaamua na kupanga bei ya sukari. Kuna maeneo katika nchi hii bei ya sukari imefika mpaka Tshs.6,000 kwa kilo na Watawala wapo na hakuna kinachofanyika.
Juzi juzi waliweka bei elekezi hakuna mfanyabiashara anayefuata bei elekezi na Wananchi wamebaki kama hawana mtetezi. Nchi hii wananchi wana shida. Ziara ya Makonda imeibua mengi. Wengi wapepotelewa na wapendwa wao.
Wengine mpaka sasa wana miaka 3 hawajapatikana, Kesi za ardhi ni lukuki, wafanyabiashara wanaonewa katika ukadiriaji wa kodi zao mfano wa Igunga. Watawala wapo hakuna wanachofanya.
Tuliahidiwa treni ya mwendo kasi kwenda Morogoro ingeanza safari Januari, 2024 lakini mpaka sasa ni kimya. Watawala wapo hakuna kinachofanyika.
Jana walishauri kuwa Mhe. Rais avunje Baraza lake la Mawaziri na kuwateua wanawake wote inaonekana wanaume hawamsaidii.
Matatizo yote yanaelekezwa kwa Mhe. Rais yeye ndo Baba na Mama yetu inampasa achukue hatua za haraka.