Mke wa rafiki yangu anavaa mavazi ya kiume

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Rafiki yangu tuliyesoma wote yeye yupo kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Arusha ingawa bado hawaja tambulishana kwa ndugu na wazazi mpaka sasa.

Rafiki yangu amekuwa akiniomba ushauri sijui namsaidiaje, anadai kuwa anampenda sana huyo binti nae binti halikadhalika, tatizo kubwa ni kwamba huyo binti anapenda kuvaa nguo za kiume ikiwemo pensi, track, mashati ya kiume na kofia za kiume.

Kipindi chote huyu kaka amfahamu huyu binti hajawahi kuona nguo ya kike tangu waishi wote isipokuwa chupi tu za kike lakini nguo zote na viatu ni vya kiume.

Huyu kaka amekua akimshauri binti kuwa avae mavazi ya kike lakini binti amekaidi na kumjibu mwanaume kwani ni lazima! na wala hana mpango huo.

Sasa huyu kaka anawaza je atampelekaje kwao?
Je atamtambulishaje kwa rafiki zake?

Je, jamii kwa ujumla itamwelewaje huyo kaka itakapomuona huyu binti?
Je, watoto watakaozaliwa watamuonaje mama yao kwa tabia za yeye kuvaa mavazi ya kiume?
 
Muulize huyo jamaa yako papuchi hapewi kama anapewa na kufurahia show hayo mengine aachane nayo au aende dukani kumnunulia hayo magauni na blauzi nk.
Umesema kitu cha kike alichonacho ni chupi tu ina maana hata hata brazia au pedi au shanga au hereni ??
Au ni chai mbichi hiii??
 
Rafiki yangu tuliyesoma wote yeye yupo kwenye mahusiano na mwanamke kutoka Arusha ingawa bado hawaja tambulishana kwa ndugu na wazazi mpaka sasa.

Title "mke wa rafiki yangu..."

Uzi wenyewe, "bado hawajambulishana kwa ndugu na wazazi..."

Ufanyie remix uzi kwanza mkuu, halafu tuendelee na kushauri
 
Sion tatizo kama zinampendeza. Kuna jiran yangu girl friend wake alikua hivyo hivyo hakumuacha kajitajidi kumbadili akabadilika kdogo plus now kajifungua ndo ameanza kuvaa madera kdogo.
 
Kosa sio kuvaa hizo nguo..

Kosa ni huana kauli dhidi yake..

Na kama huna kauli dhidi ya mwanamke wako basi USIMUOE atakusumbua
 
Back
Top Bottom