magnifico
JF-Expert Member
- Jan 14, 2013
- 13,982
- 34,307
Hapo kwenye sabufa akiweka wimbo wa Cabo Snoop Prakatatumba hata popo bawa hatoboi.Hilo la udi na ubani nimewahi kusikia pia na hata la taa lifanyie kazi. Kuna sehemu niliona watu wanajadili facebook ngoja nikaokote nondo nikuwekee hapa uzifanyie kazi. Pia kuna watu wanashauri usage pilipili na kumwaga unga wake wanapoishi. Nasikia ukiwaingia machoni hawaponi
Nimepitia sehemu walikuwa wanajadili na maoni ni kama ifuatavyo:
1. ziba njia zote wanazoingilia popo kisha changanya grisi na ugoro paka sehemu zote wanapenda kukaa
2. Chukua magunzi ya mahindi yachome ule moshi wake utawasambaratisha wote
3. Funga taa za LED mbili tu darini wataondoka wote
4. Washa pilipili kavu kwenye jiko weka darini. Wakitoka paka grisi walipotokea utawaona
5. Nunua kiatirifu yaani sumu iitwayo LAVA kichupa kidogo cc100 changanya yote kwa lita 5 za maji kisha spray darini
6. Chukua mafuta ya taa lita moja tafuta pakti tano za sabuni ya omo halafu changanya na maji lita ishini kisha mwaga walipo popo wataondoka milele hawatarudi
7.Nunua steel wire ziweke sehemu wanazoingilia na wanapolala watakimbia utawaona tena
8. Kuna miti inatoa matunda madogo madogo mekundu yanapendwa sana na popo kama ipo karibu na kwako hawatahama kamwe
9. Weka sub woofer darini fungulia mpaka mwisho watakimbia maana hawapendi kelele
10. Ugoro. Koroga ugoro mwaga darini utanishukuru baadae
Nimechukua maoni kumi bora nadhani ukiyatumia haya utatuletea mrejesho pia usisahau kunipa fungu la kumi (10%)