Msaada tafadhali: Popo wamehamia kwenye nyumba yangu

Nimejenga kijijini kwangu, kuna vichaka vimenizunguka ambako ni makazi ya ndege na baadhi ya wanyama,wakiwemo popo.

Tatizo ni kwamba popo wengi wanaishi juu ya dari ya nyumba. Usiku ni makelele,wanachafua dari kwa vinyesi na mikojo.

Nilijaribu kumpandisha kijana darini mchana akiwa amefunga tochi kichwani,walimpiga balaa.

Naomba msaada wa namna ya kuwaondoa hawa wanyama.
Nilikuwa na tatizo hilo mpaka nilimpompata mtaalamu mmoja ambaye anatengeneza sumu na kuwawekea. Ni ndani ya saa 24 hutokuta hata mmoja akiwa hai na hawatorudi kwa muda wa miaka miwili.
.
.
Nitafute nikusaidie
 
Nashukuru kwa ushauri,nimeanza kufanyia kazi. Nitaleta mrejesho
Mkuu kwani hizo sehemu wanazopita haziwezi kuzibwa?

Kwa uzoefu wangu unaweza kuziba kabisa sehemu kati ya ukuta na bati. Kama zinahitajika vents zinawekewa wavu ili wadudu, ndege au Popo wasiweze kupita.
 
Hakuna dawa ya kuwaondoa popo moja kwa moja kiongozi watarudi tu.ILa lakufanya tafuta fundi aingie juu ya dari azibe kwa zege sehemu zote penye uwazi ukiwa juu ya dari utaona uwazi katika tofari na bati hiyo ndio dawa.Utakaa kwa raha mustarehe.
USHUHUDA
Ni nakaa mbali na family kwenye nyumba kubwa iliyotulia. Na Mimi ni mtu wa Safari sana. Nilikuja kugundua kuna tatizo la popo wengi baada ya sehemu za gypsum kuanza kudondoka.

Baada ya kuomba ushahuri niliambiwa niweke taa darini watahama mara moja. Fundi umeme alifanya kazi nzuri ya kufunga taa zenye mwanga mkubwa. Zaidi alifagia mavi ya popo yalijaa gunia mbili(2)!

Kadiri siku zinavyoenda popo walipungua sana. Kwa kukisia walipungua kwa wastani wa 80% au 90% baada ya kuwasha taa mchana mfululizo kwa wiki mbili. Baada ya hapo nilisafiri kwa muda wa mwezi moja hivyo kutowasha taa darini.

Nilivyorudi niliishiwa nguvu baada ya kuona popo wameongezeka. Nikaendelea na zoezi la kuwasha taa takribani mwezi sasa. Popo wamepungua kwa Kama 50% lakini wamegoma kuhama kabisa.

Nilitembelea duka la TFA Arusha nikawaeleza tatizo wakanihakikishia kuna sumu ya vidonge inayoyeyuka ya kuua popo. Dawa hiyo kwanza inaua kila kiumbe hai kilichopo akiwemo binadamu! hivyo ni lazima kuhama nyumba kwa muda wa siku saba.

Kwa kweli hii dawa pamoja na kuona inaweza kuwa muwafaka ilinitisha sana. Nisije nikajiua mwenyewe! Lakini baada ya kuona popo wamegoma kabisa kuhama kwa taa, na wanaharibu nyumba kwa kasi nimeamua nitatumia hiyo dawa na nitahama nyumba kwa siku 10 ili kukwepa madhara yeyote.
 
Wangapi wanateseka na popo niko mwanza mm ni mtaalamu wa dawa nzuri ya kupaka Darin tuu ndani ya miaka miwili utaona popo Piga 0674477835 Bei zetu ni nafuu dawa 45000 inatosha vumba 10 na zaid
 
Tafuta sumu ya panya ile ya pellets wanatengeneza farmers center
 
Sambaza vyumbani humo watakula maan ni chambo yenye sumu inafanya kazi vizuri tu
 
USHUHUDA
Ni nakaa mbali na family kwenye nyumba kubwa iliyotulia. Na Mimi ni mtu wa Safari sana. Nilikuja kugundua kuna tatizo la popo wengi baada ya sehemu za gypsum kuanza kudondoka.

Baada ya kuomba ushahuri niliambiwa niweke taa darini watahama mara moja. Fundi umeme alifanya kazi nzuri ya kufunga taa zenye mwanga mkubwa. Zaidi alifagia mavi ya popo yalijaa gunia mbili(2)!

Kadiri siku zinavyoenda popo walipungua sana. Kwa kukisia walipungua kwa wastani wa 80% au 90% baada ya kuwasha taa mchana mfululizo kwa wiki mbili. Baada ya hapo nilisafiri kwa muda wa mwezi moja hivyo kutowasha taa darini.

Nilivyorudi niliishiwa nguvu baada ya kuona popo wameongezeka. Nikaendelea na zoezi la kuwasha taa takribani mwezi sasa. Popo wamepungua kwa Kama 50% lakini wamegoma kuhama kabisa.

Nilitembelea duka la TFA Arusha nikawaeleza tatizo wakanihakikishia kuna sumu ya vidonge inayoyeyuka ya kuua popo. Dawa hiyo kwanza inaua kila kiumbe hai kilichopo akiwemo binadamu! hivyo ni lazima kuhama nyumba kwa muda wa siku saba.

Kwa kweli hii dawa pamoja na kuona inaweza kuwa muwafaka ilinitisha sana. Nisije nikajiua mwenyewe! Lakini baada ya kuona popo wamegoma kabisa kuhama kwa taa, na wanaharibu nyumba kwa kasi nimeamua nitatumia hiyo dawa na nitahama nyumba kwa siku 10 ili kukwepa madhara yeyote.

Tumia sumu ya panya ile ya pellets inayotengenezwa na farmers center ni nzuri
Tawanya vyumban inaua vizuri maan nimeitumia kuulia panya nikakuta na popo wengi wamekufa
 
Wangapi wanateseka na popo niko mwanza mm ni mtaalamu wa dawa nzuri ya kupaka Darin tuu ndani ya miaka miwili utaona popo Piga 0674477835 Bei zetu ni nafuu dawa 45000 inatosha vumba 10 na zaid
Sasa faida ipo wapi iwapo nitaona popo! Oh ni ujinga wenu ulimaanisha hutaona wewe kwa ujinga ukaondoa h
 
POPO HUWA HAWAONI. YALE MACHO SI YA KUONEA KITU YANA KAZI NYINGINE SIIJUII. Huo mwanga hautawafukuza. Nashauri wapulize ile dawa E40 huko kwenye dari.nimepiga ktk mwembe hao walikimbia maana walikuwa wanakula maembe machanga na kupunguza mazao.AVAE MASK ILE MAALUM AKIWA ANAPULIZIA. Harufu ya dawa hii inawafukuza. Hakikisha haiingii ndani ya vyumba. Wasiliana na wataalamu namna ya matumizi
Nilisikia wanatumia sauti kusafiri, yani wanatoa mlio then ndio wanajua njia iko wapi.
 
Tafta bint wakazi au masai ili uishi nao ukiondoka taratibu nyingine zisidumae
 
Nimejenga kijijini kwangu, kuna vichaka vimenizunguka ambako ni makazi ya ndege na baadhi ya wanyama,wakiwemo popo.

Tatizo ni kwamba popo wengi wanaishi juu ya dari ya nyumba. Usiku ni makelele,wanachafua dari kwa vinyesi na mikojo.

Nilijaribu kumpandisha kijana darini mchana akiwa amefunga tochi kichwani,walimpiga balaa.

Naomba msaada wa namna ya kuwaondoa hawa wanyama.
Hauna jirani Wanigeria hapo unapoishi au Wachina, utawasaidia kwa mboga.
 
Tafuta paa la transparent (pieces chache) utumie kuezeka maeneo kadhaa ili kuruhusu mwanga uingie darini, watahama wote.
Hawahami Nimeshashuhudia Hilo Mimi Nahusika na Hizo Kazi Za Kuwaangamiza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom