Msaada tafadhali: Popo wamehamia kwenye nyumba yangu

Msaada tafadhali: Popo wamehamia kwenye nyumba yangu

USHUHUDA
Ni nakaa mbali na family kwenye nyumba kubwa iliyotulia. Na Mimi ni mtu wa Safari sana. Nilikuja kugundua kuna tatizo la popo wengi baada ya sehemu za gypsum kuanza kudondoka.

Baada ya kuomba ushahuri niliambiwa niweke taa darini watahama mara moja. Fundi umeme alifanya kazi nzuri ya kufunga taa zenye mwanga mkubwa. Zaidi alifagia mavi ya popo yalijaa gunia mbili(2)!

Kadiri siku zinavyoenda popo walipungua sana. Kwa kukisia walipungua kwa wastani wa 80% au 90% baada ya kuwasha taa mchana mfululizo kwa wiki mbili. Baada ya hapo nilisafiri kwa muda wa mwezi moja hivyo kutowasha taa darini.

Nilivyorudi niliishiwa nguvu baada ya kuona popo wameongezeka. Nikaendelea na zoezi la kuwasha taa takribani mwezi sasa. Popo wamepungua kwa Kama 50% lakini wamegoma kuhama kabisa.

Nilitembelea duka la TFA Arusha nikawaeleza tatizo wakanihakikishia kuna sumu ya vidonge inayoyeyuka ya kuua popo. Dawa hiyo kwanza inaua kila kiumbe hai kilichopo akiwemo binadamu! hivyo ni lazima kuhama nyumba kwa muda wa siku saba.

Kwa kweli hii dawa pamoja na kuona inaweza kuwa muwafaka ilinitisha sana. Nisije nikajiua mwenyewe! Lakini baada ya kuona popo wamegoma kabisa kuhama kwa taa, na wanaharibu nyumba kwa kasi nimeamua nitatumia hiyo dawa na nitahama nyumba kwa siku 10 ili kukwepa madhara yeyote.
Funga speakers (nimewaza tu, kama uliweka taa) uwe unafungulia mziki wenye kelele kama Singeli, na taa juu, hawawezi bakia hapo tena.
 
Funga speakers (nimewaza tu, kama uliweka taa) uwe unafungulia mziki wenye kelele kama Singeli, na taa juu, hawawezi bakia hapo tena.
Au paka oil chafu huko darini kuharibu mazingira yao kwa harufu na kukosa hewa
 
Funga speakers (nimewaza tu, kama uliweka taa) uwe unafungulia mziki wenye kelele kama Singeli, na taa juu, hawawezi bakia hapo tena.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]wewe jamaa umenichekesha sana,mwanzoni nilijua umeongea masihara kumbe uliongea serious kabisa

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Wangapi wanateseka na popo niko mwanza mm ni mtaalamu wa dawa nzuri ya kupaka Darin tuu ndani ya miaka miwili utaona popo Piga 0674477835 Bei zetu ni nafuu dawa 45000 inatosha vumba 10 na zaid
una maanisha utaona au hutaona?

Haya ni maneno mawili yanayo pingana kabisa.
 
Funga speakers (nimewaza tu, kama uliweka taa) uwe unafungulia mziki wenye kelele kama Singeli, na taa juu, hawawezi bakia hapo tena.
Mrejesho.
Nilitumia hiyo dawa, lakini baada ya hizo siku popo hawakufa japo walipungua. Siku moja nilipanda darini na fimbo kama kichaa!!! Nilipigapiga popo wote walioonekana (wengi wakiwa watoto). Wakahamaki na kukimbilia chemba ya kibaraza cha mbele, ambacho kimetenganishwa na ukuta hivyo vurugu zangu hazikuingia mbele ya huo ukuta
 
Dawa ya popo ni moja tu na hawatorudi tena (serious) ni kinyesi cha ng'ombe kwenye zile nafasi wanapopita. Kama ni wengi kisambaze darini wanahama. Kinyesi kibichi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom