Morogoro: Polisi wawatawanya wananchi waliotaka kuchota mafuta baada ya ajali ya lori

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,328
8,243
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, limefanikiwa kuwatawanya wananchi waliojitokeza kuchota mafuta, baada ya lori lenye namba za usajili T 810 AJL lililobeba mafuta aina ya dizeli kuacha njia na kuingia mtaroni kisha mafuta hayo kuanza kumwagika, katika eneo la Msimba lililopo wilayani Kilosa.

Mafuta.JPG

Onyo: Ni muhimu kuzingatia kwamba mafuta ya dizeli ni hatari sana na hayapaswi kuguswa au kuchotwa na mtu yeyote pindi gari lipatapo ajali. Hivyo ikiwa kuna ajali ya gari na mafuta ya dizeli yanamwagika kwenye barabara, ni muhimu kuwa makini na kutokaribia eneo hilo, kwani kuna hatari ya mlipuko.

Kama kuna chanzo cha moto chochote karibu, kama vile sigara au sparki, inaweza kusababisha mlipuko hatari. Hivyo, ni muhimu kuhakikisha kwamba unatoa taarifa kwa askari wa zimamoto na uokoaji haraka iwezekanavyo ili waweze kushughulikia tishio hilo kwa usalama zaidi.
 
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, limefanikiwa kuwatawanya wananchi waliojitokeza kuchota mafuta, baada ya lori lenye namba za usajili T 810 AJL lililobeba mafuta aina ya dizeli kuacha njia na kuingia mtaroni kisha mafuta hayo kuanza kumwagika, katika eneo la Msimba lililopo wilayani Kilosa.

View attachment 2610264

Onyo: Ni muhimu kuzingatia kwamba mafuta ya dizeli ni hatari sana na hayapaswi kuguswa au kuchotwa na mtu yeyote pindi gari lipatapo ajali. Hivyo ikiwa kuna ajali ya gari na mafuta ya dizeli yanamwagika kwenye barabara, ni muhimu kuwa makini na kutokaribia eneo hilo, kwani kuna hatari ya mlipuko.

Kama kuna chanzo cha moto chochote karibu, kama vile sigara au sparki, inaweza kusababisha mlipuko hatari. Hivyo, ni muhimu kuhakikisha kwamba unatoa taarifa kwa wataalamu wa usalama haraka iwezekanavyo ili waweze kushughulikia tishio hilo kwa usalama zaidi.
Kwanini polisi wachukue jukumu la askari wa zimamoto na uokoaji badala ya wahusika, endapo mlipuko ungetokea polisi wangetumia bunduki kuudhibiti?
 
Dizeli si kama mafuta ya taa tu,haina shida

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Mafuta ya taa ni highly combustible kuliko diesel! Diesel ina low combustibility.

Kuwaka kwa diesel ni tafauti na petrol, tafauti na mafuta ya taa.

Diesel unachota tu, kushika moto inashika, ila kwa tabu sana, achilia mbali kulipuka. Kimbembe ni petrol, kaa mbali nayo
 
Back
Top Bottom