Lita Elfu 20 zaokolewa kwenye ajali ya lori la mafuta kuungua moto Ubungo

2025DG

JF-Expert Member
Jan 30, 2023
508
1,426
Kufuatia ajali ya lori la mafuta kuungua moto siku ya jana eneo la Ubungo Kibo Dar es Salaam, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kinondoni limesema kuwa zaidi ya lita elfu 20 za mafuta ziliokolewa kati ya lita elfu 39,500 zilizokuwa ndani ya lori hilo.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kinondoni Mrakibu Mwandamizi Elisa Mugisha, amesema pia takribani vibanda 19 vya wafanyabiashara vilivyokuwa vimeshika moto viliokolewa huku pikipiki mbili zikiteketea.

#EastAfricaTV
 
Nilikua Yale MANENO Jana huduma ya usafirishaji ilisimama Kwa MUDA wa masaa kadhaa....

Maeneo ya pale nikamuona RC Chalamila akiwa kwenye boda boda kuwai eneo la tukio......
 
Sasa kweli haujawahi Kuona moto kama ule morogoro msamvu
Uko serious na unachoandika au tatizo la kutosoma hoja Moto wa msamvu ulienda juu vile Moto wa jana umeenda juu kimo ch kupits mnazi unavyosema msamvu Moto unakuwa chini tu juu mimoshi ile jana Moto ungekuw ajari imetokea usiku juu kote kungekua mwanga mwekundu hadi Temeke tungeona.
 
huyo anabisha tuh
 
Back
Top Bottom