Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Jakaya tulimwambia kabla ya baraza la juzi kuwa wale wote wanaohisiwa kuwa wala rushwa watupwe nje ya baraza.

Magufuri ni kama Mrema ni mla rushwa na hilo JK analijua.

Magufuri amehusika kwenye ufisadi wa kuuza nyumba na aliomba rushwa ili boti za spidi ziende Mwanza.

kwangu mimi Magufuri kuendelea kuwa waziri ni katika kuyalinda mafisadi.

mliokuja hapa kumpigia debe tuambieni nyumba za serikali alivyafanya kuwa mradi wake binafsi. ktk mawaziri wanaotakiwa kuchunguzwa ni huyu Magufuri ili baraza libaki safi.

ndio maana Chenge akasema hivi ni vijisenti kwani anajua Mramba, Magufuri, Mkapa, Yona na Mungai wana mabilioni ya mapesa.

Kama magufuri ni mla rushwa na JK anajua hili mbona bado anarudi kwenye baraza? hii inanichanganya sana mkuu tafadhali fafanua kidogo hapa
 
Kama magufuri ni mla rushwa na JK anajua hili mbona bado anarudi kwenye baraza? hii inanichanganya sana mkuu tafadhali fafanua kidogo hapa
Magufuli si ndiyo huyo huyo pombe?sasa wa nini?tunataka timu mpya kabisa..na kama mh rais hawezi kufanya hivyo na yeye ajiuzulu tu!
 
Jakaya tulimwambia kabla ya baraza la juzi kuwa wale wote wanaohisiwa kuwa wala rushwa watupwe nje ya baraza.

Magufuri ni kama Mrema ni mla rushwa na hilo JK analijua.

Magufuri amehusika kwenye ufisadi wa kuuza nyumba na aliomba rushwa ili boti za spidi ziende Mwanza.

kwangu mimi Magufuri kuendelea kuwa waziri ni katika kuyalinda mafisadi.

mliokuja hapa kumpigia debe tuambieni nyumba za serikali alivyafanya kuwa mradi wake binafsi. ktk mawaziri wanaotakiwa kuchunguzwa ni huyu Magufuri ili baraza libaki safi.

ndio maana Chenge akasema hivi ni vijisenti kwani anajua Mramba, Magufuri, Mkapa, Yona na Mungai wana mabilioni ya mapesa.
Hizo ni falsafa zenu tu Nungwi..this time ni mpaka kieleweke..watajane wasitajane hiyo haijalishi!Tunataka tuone mambo!Fisadi apewe nafasi ya kumshughulikia fisadi?since when?Tanzania mpya inahitajika yenye maono mapya..tunataka kiongozi wa kutupitisha kwenye kasheshe hili bila mapigano ya kati ya masikini na mafisadi kuanza!
 
Kama magufuri ni mla rushwa na JK anajua hili mbona bado anarudi kwenye baraza? hii inanichanganya sana mkuu tafadhali fafanua kidogo hapa

Ni kama alivyorudi Chenge au Mramba kwenye baraza ndivyo alivyorudi Magufuri, Mwandosya aliipeleka kesi ya Magufuri kwa Mkapa lakini hakuna kilichofanyika kwani Mkapa alikuwa kwenye biashara maalum Ikulu. File la Magufuri ni baya sana fuatilia utajua dada yetu.
 
Kama magufuri ni mla rushwa na JK anajua hili mbona bado anarudi kwenye baraza? hii inanichanganya sana mkuu tafadhali fafanua kidogo hapa

Nilisahau na Mungai ambaye alisema kabisa kuwa anataka atumie muda huu kufanya biashara ana kampuni majuu ya kifisadi.
 
Nilisahau na Mungai ambaye alisema kabisa kuwa anataka atumie muda huu kufanya biashara ana kampuni majuu ya kifisadi.
Watu wote wa viwango vyao alivyovianisha fisadi Chenge ni lazima wawajibike!Kwa rais aelewe tu kuwa hakuna namna zaidi ya kudili na issue hii kamavile wananchi wanavyoona inafaa!Tujiadhari na machafuko..the president needs to take that route!
 
Magufuri ni kama Mrema ni mla rushwa na hilo JK analijua.

Mkuu Nungwi,

Heshima mbele, kwenye hili darasa tupo ukurasa mmoja, Magufuli, kuna wakati hata mimi nilitaka uupanda mkenge, mpaka nilizipata dataz kwamba ni sawa na Mrema na Keenja, wao wana tabia ya kujenga kitu kikaonekana lakini kumbe wametumia hela mara tatu ya zilizokadiriwa,

Magufuli, amejiuzia maeneo mengi sana ya ardhi, either yeye binafsi au kwa kuwatumia ndugu zake, halafu alifikia mahali nyumba ya serikali ilikuwa haiwezi kuuzwa bila kibali chake yeye kama waziri, that was out of the line kwa sababu nyingi ya hizo nyumba za NHC aliwauzia wasiopaswa kuuziwa, kwa kweli ana bahati sana kuendelea kuwepo kwenye cabinet, na ninajua kuwa kwenye huu mchezo tunaoendelea nao wa kuwakurupua mafisadi, yeye hana muda mrefu sana atachomolewa tu!

Hiyo wizara kama alivyosema Mtanzania, apewe damu mpya wako wengi sana wanaoweza!
 
Kwa walioko TZ

Hivi yule dada wa UDSM sheria, mwenye RAV4 aliekuwa anakaa MABIBO hostel ameshaolewa na MAGUFULI ? , kwa maana alikwa anajishau kuwa anazimaliza pesa za BARABARA zetu kipindi kile Mh. yuko Miundombinu.

Hakuwa sheria..kwanza ni mtalamu wa miamba..(Geologist)yuko dar.
Then si dhani kama anahusika moja kwa moja na barabara..

JPM alifanya kazi kwa kweli...sio utani...hayo ya personal affair yabaki kwake..kila mtu ana udhaifu wake.Mdada wa watu katulia anajifanyia kazi yake na kulea watoto wake na mzee JPM.

Call a spade a spade and not Big Spoon jamani.

Always
Buswelu
 
Heshima Mbele Wakuu,

Baada ya Mhe. Chenge kushindwa kujenga hata barabara moja toka achaguliwe kuwa waziri wa Miundombinu na kwa kuwa imedhihirika kwamba tuhuma alizonazo ni nzito na amekubali kuwajibika kwa manufaa ya umma.

Huu ni wakati muafaka wa kupendekeza ni nani anafaa kuchaguliwa kuwa Waziri wa Miundombinu. Kipindi cha Awamu ya tau Mhe. Magufuli alijitahidi sana kujenga barabara kwa kiwango cha rami mpaka nchi ikaanza kupendeza, mojawapo ya kazi ambazo ninamsifu ni ujenzi wa barabara za Mwanza mjini ambapo hapo kabla kulikuwa hakuna barabara za kiwango cha rami aliweza kujua barabara zote kwa jina na kujua ni wapi panatakiwa papewe kipaumbele.

Mie nadhani kuna haja ya yeye kurudishwa ili akamalize ahadi yake ya kuweka rami barabara ya Mtwara mpaka Mwanza.

Najua chaguo la Muungwana linaweza kuwa Ezekiel Maige kwa silimia 70, ila Namuomba mkuu wa kaya amrudishe Magufuli katika wizara hiyo!

Kabla hauja Post Thread angalia Nini umeandika...Hii Tread ni nzuri Lakini Maelezo Yako Ni Mavi Matupu!!

Muache Magufuli huko kwenye samaki!!JK
wasi kuchanganye...!!! JK Kwenye samaki Ulipatia..!!Pangua wengine Lakini Magufuli muache pale pale...kama Una nibishia Mtoe uone...
 
Ninyi nyote hamjui TEUZI za viongozi wa CCM na Serikali yake zinazingatia kigezo gani kikubwa.Ngoja niwajuze;Ni lazima anayeteuliwa awe tayari kutafuta/kukusanya fedha toka kwenye Taasisi/shirika la umma/Wizara anayoiongoza pindi zinapohitajika kwa kazi maalum/nyeti!Maghufuli hawezi, anajikusanyia yeye mwenyewe tu.Baada ya kuimulika sana Benki Kuu, zimebaki Wizara na Taasisi chache za UMMA zinazoweza kuifanya kazi hiyo.Baadhi yake ni: Miundombinu,Kazi(NSSF),Maji,n.k.Hivyo ni lazima watafutwe watu "makini na mahiri" kwa kazi hiyo.
 
nilienda kulipa kodi ya kiwanja changu mwaka 2001 wizarani, nilirudi na pesa zangu mkononi bila kulipa foleni ilikuwa ni kubwa mno. Lakini nimeenda mwaka jana nimetumia dakika 10 kukamilisha ulipaji wa viwanja vitatu.
Viwanja vinne! Mwenzetu nawe ni fisadi wa ardhi nini?
 
1.Ninyi nyote hamjui TEUZI za viongozi wa CCM na Serikali yake zinazingatia kigezo gani kikubwa.

Ngoja niwajuze;
1.Ni lazima anayeteuliwa awe tayari kutafuta/kukusanya fedha toka kwenye Taasisi/shirika la umma/Wizara anayoiongoza pindi zinapohitajika kwa kazi maalum/nyeti!Maghufuli hawezi, anajikusanyia yeye mwenyewe tu.

2.Baada ya kuimulika sana Benki Kuu, zimebaki Wizara na Taasisi chache za UMMA zinazoweza kuifanya kazi hiyo.Baadhi yake ni: Miundombinu,Kazi(NSSF),Maji,n.k.Hivyo ni lazima watafutwe watu "makini na mahiri" kwa kazi hiyo.

wewe unajua nini sasa hapa,Karibu sana hapa JF,Kwanza naomba urekebishe usemi wako niliopigia mstari hapo juu.

Kwa taarifa yako,Sie ndiyo tulikuwa wa kwanza kusema Pius Msekwa atakuwa Makamu mwenyekiti wa CCM.

Sie ndiyo tulikuwa wa kwanza kusema Pinda ndiye atakayechukua nafasi ya Lowassa.

Sie ndiyo tulisema majina kama George Mkuchika yatakuwamo katika cabinet.

Yes We said coz we know everything you dont know.Changia maada na acha kuleta viroja,

Je Waziri wa Nishati na madini,William Heleja alitoka katika wizi huko unakosema??

Je Masha alitoka huko??au specluation zako baada ya kuona Mkulo kaingia basi na wewe umepata la kusema..

Kata ishu na karibu hapa JF.
 
Katika Mawaziri hakuna waziri mchapakazi na anayejua nini anachofanya kwa manufaa ya watanzania kama Magufuli. Magufuli sio malaika, ila anajitahidi kwa kiwango cha ubinadamu unavyomruhusu.

Na mengi ya mapungufu yake yanachangiwa na mabosi wake ambao ni Mashetani. Hii nchi hivi sasa inahitaji mtu kama Magufuli kuwa rais,Yuko tayari kuchukua maamuzi mazito bila kusita wala kumwogopa mtu.

Mambo ya vikamati kamati kwenye wizara anazopitia havipo. Umefanya kosa ushahidi upo, anaangalia maandishi yanasemaje unakwenda na maji.

Hatuihitaji Mr. "kutaka kupendwa" tunahitaji mchapakazi

Kama nakumbuka kampeni za Kikwete vile, huyu Magufuli ni fisadi tu. Inamaana mmeshasahau ya kumuuzia ndugu yake nyumba kinyemela? kweli hamwogopi mtu!
 
wewe unajua nini sasa hapa,Karibu sana hapa JF,Kwanza naomba urekebishe usemi wako niliopigia mstari hapo juu.

Kwa taarifa yako,Sie ndiyo tulikuwa wa kwanza kusema Pius Msekwa atakuwa Makamu mwenyekiti wa CCM.

Sie ndiyo tulikuwa wa kwanza kusema Pinda ndiye atakayechukua nafasi ya chenge.

Sie ndiyo tulisema majina kama George Mkuchika yatakuwamo katika cabinet.

Yes We said coz we know everything you dont know.Changia maada na acha kuleta viroja,

Je Waziri wa Nishati na madini,William Heleja alitoka katika wizi huko unakosema??

Je Masha alitoka huko??au specluation zako baada ya kuona Mkulo kaingia basi na wewe umepata la kusema..

Kata ishu na karibu hapa JF.

Nasahihisha: Neno hamjui lisomeke "hamjui".Naomba kuwasilisha.
 
wote tunasema kwa kauli moja, LAZIMA WAWAJIBIKE' but how?
tafadhali tutoe sasa njia ya kutumia ili wahusika wawajibike, this is now too much talk, too much much useless information, if it does not commit us to anything.
Katika JF kuna makundi wawili au matatu hivi,
moja dogo la wenye kutafuta information at their own spare time na kutuletea hapa,
mbili, la wenye kuzishabikia na kuzipamba kwa lugha mbalimbali humu na kutia pilipili kupandisha wenzao presha
na tatu (kama) wapo wenye kufanyia kazi hizi habari na kuplan way forward.
Kundi la mwisho naomba liwe makini na kubwa, lipate viongozi wenye busara na nasi tulifuate kujinasua kwenye hii maze.
 
Hata Mkuu wa kaya alishakuwa kiongozi toka 1975,Mbona ameendelea kurudi kuwa kiongozi??Raila Odinga alikuwa kiongozi katika kipindi cha Moi na sasa karudi tena kuwa kiongozi..Je tungeweka damu mpya??vya kale ni dhahabu.Tusiwe na mawazo mgando ya kupend avbitu vipya tu,tunahitaji kuwa na vitu vya zamani ili tuwe na mchanganyiko ulio bora.

Hizi sio Kampeni ila ni kujaribu kuangalia hatma ya barabara zetu na nchi yetu.Toka Magufuli ametoka Wizara ya Miundombnu zamani Ujenzai na Mawasiliano,hakuna mradi mpya wa barabara ulioanzishwa.

Huyu si ndio alikuwepo pale na akawa na ile issue ya Nyumba/kiwanja Ubungo? Samahani kama nimekosea au kufananisha lakini kama ndio yeye basi mnataka kumpa Ulaji amalizie alichokianza alipokuwa pale huku huko Mifugo aseme nako. Hata yeye anajua kwamba hawezi kupata Urais wala Uwaziri Mkuu kitakachofuatia ni kama Mzee wa Vijisenti a.k.a Mzee wa Full Shangwe.
 
Tusubiri hitimisho la mswaada wa leo.tutajua ni nani anahuska
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom