Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

siku zote magufuli amekuwa akifanya kazi nzuri lazima apongezwe. Hata ile kashfa ya nyumba za serikali ilishinikizwa na mkapa na sumaye na yeye akaona achukue japo nyumba moja.

Nikweli anafanya kazi nzuri lakini ni fisadi mzuri tuu hasa katika swal la nyumba, na pale alipokuwa miundombinu. Magufuri aliforce mradi wabarabara kupita kijijini kwake japo kuwa upembuzi yakinifu ulikuwa hauruhusu kiwango hicho katika barabara hiyo. Of course kuna mengi, though kiutendaji nimchapakazi kama Mkapa
 
Tuipongeze serikali kwa jitihada zake, kitendo tu cha rais kuridhia timu ya pamoja iingie ktk msako wa maharamia hawa inatosha kuwapa pongezi, magufuli anahaki ya kupongezwa kwa ujasiri na misimamo ya wazi, alishawahi lalalmikia sana jambo hili pale jk alipomteua kukaa mifugo,uvuvi. Kabla ya operesheni hii alitupatia takwimu kuwa ziwa victoria linaiingizia nchi zaidi mapato kuliko bahari ya hindi, wakati ziwa linatupatio billions bahari inatupatia 800million.

Ame prove kuwa si mpiga debe tu bali msema kweli, kupongezwa ni haki yake, jk shukrani kuipa nguvu sekta hii moja kwa moja, maana kuiondoa uvuvi toka maliasili ameona mbali. Hongera sana
 
Maghufuli anafanya kazi nzuri sana, tumpongeze. Wamekuwa wakimfisadi kwa kumuhamisha idara ambazo ameonyesha ubunifu wa hali ya juu. Leo amethibitisha kuwa hata akipelekwa popote panainuka.

BIG UP MAGHUFULI
 
siku zote magufuli amekuwa akifanya kazi nzuri lazima apongezwe. Hata ile kashfa ya nyumba za serikali ilishinikizwa na mkapa na sumaye na yeye akaona achukue japo nyumba moja.
pamoja na mapungufu yake ya kibinadamu kama chuki na visasi.....john pombe magufuli ni mchapakaziii..

Anastahili pongezi na muungwana ampe support.. Kuwekwa pale kwenye vitoweo maadui zake walifanya komoa ila amebounce back mpaka anatamba uvuvi utaizidi sekta ya madini....

Anajua mkuu hawezi mpa wizara zenye mvuto kama madini na barabara.....

Big up john .p. Magufuli
 
Hivi bei ya moja ya zile boti za doria ni kiasi gani? Kama doria moja tu inaweza kukamata mali ya wizi ya thamani ya kukaribia shilingi bilioni moja kwanini tusinunue boti nyingi za doria ili tukamate wezi zaidi?

To put everything in perspective, I believe the sub national level administrative organ katika sehemu hii ya bahari ni manispaa ya Ilala, hawa walikusanya mapato ya bil 4.2 katika mwaka wa kifedha 07/08.
 
Hivi mpango ulianza baada ya Magufuli kuwa waziri wa wizara hii? Tuache kutoa credit zisizo na uhakika. Huu mpango ulianza tangia enzi za Mzee MKAPA wakati magufuli hayuko wizara hiyo. Ni sasa tu tunaanza 'kuonyeshwa" matunda yake....

omarilyas

Hata tuegemee wapi, Lazima tukubali kwamba uwezo wa waziri muhusika ni kigezo muhimu ktk utekelezaji wa mambo mbali mbali ktk Tz.

Sera zetu zinategemea initiatives za mtu binafsi. kuna mengi yameamuliwa na tukayakubali lakini hayajawahi kutekelezwa.

Magufuli anastahili PONGEZI popote alipowekwa ameonyesha initiatives, za utekelezaji wa sera zilizopo au mpya. Kumbuka Ujenzi, Ardhi, na sasa Uvuvi. Naweza nikamtetea matokeo yake ni mazuri.

Sasa linganisha na ubunifu wa akina Muramba ktk Elimu. Disaster! Kapuya ktk Ulinzi. Disaster! Zakia huko maliasili na Fedha. Disaster! Msolla na Magembe Elimu ya Juu mambo ya mikopo. Disaster! Endelea hivyo kwa mawaziri wooote mpaka huko Afya kwa akina Mwakyusa na inclination zao na Muhimbili badala ya Wizara. Hao akina Masha ndo htuhitaji kusema.

Linganisha pia mawaziri wengine walioshika wizara alizopitia Magufuli kabla yake. Kwani uliwahi kusikia chochote juu ya huu ulinzi? Waliotangulia kwa taarifa tulizonazo waliifanya Doria ni biashara ya kuwakamata na kuwatoza faini bharini na pesa kuingia mifukoni mwao.

Enzi za Mrema aliwahi kuonyesha ushuja kama huu wa Magufuli.
 
Bravo Magufuli...
Bravo... unajulikana sana kwa ubunifu na umahiri wako.
No matter what this man is performing beyond expectations.
 
Acheni kumbania magufuli kwani jamaa ni mchapa kazi kweli kweli,kama huu mpango ulibuniwa toka mkapa yuko madarakani kwanini kipindi hicho hawakukamatwa?

Wabongo acheni unafiki
 
....Nimekaa nikafikiria kwa upande mwingine wa shilingi......Roho itasuuzika sana nikiona mheshimiwa Rais akipeana mikono kwa "job well done" na watuwatakaowaburuza na kuwaegesha pale "magogoni" wezi wa rasilimali zetu za taifa.

.....bwana nani hii ni vigumu sana kutokea,kumbuka Pombe alipelekwa kule kama adhabu fulani hivi...hata kama mafanikio haya ni majumuisho ya tija mbaliX2,Pombe ana kila sababu binafsi ya kufurahi.it just proofs that when you are good U'r good,no matter the environment one is subjected to.
**pombe delivered on Ground,he's doin it on Water,i'm sure he can do the same on Air!!
 
Kwa hili la kukamata meli anasifiwa kwa lipi? Once upon a time mtu aliyejulikana kama Augustine Mrema, alikuwa anaenda kwenye vyama va ushirika na kuwanyima ruhusa kulipa malipo ya pili mpaka wamwambie, ikiwa wakimwambia siku ya malipo, yeye anatangaza kuwa kwa juhudi zake kuwa amewapigania wananchi mpaka wamelipwa mabaki ndivyo alivyojijengea umaarafu.

Operesheni ya kukamata meli haramu za uvuvi imeanzia South Africa, Mozambique, nk. Je, Magufuli alikuwepo huko Msumbiji na South Africa? Unaweza kuwa kiongozi mzuri bila kupayuka na wananchi wakaelewa kama Jackson Makweta na wengine.
 
Kwa kweli magufuli ni mchapakazi na matokeo yanaonekana!angalia wizara aliyokuweko ile ya ujenzi sasa hivi imedolola kweli tofauti na alivyokuwepo magufuli!Magufuli anatimiza wajibu wake!
 
Magufuli ni dume kama Mrema tu; hata umpeleke ambako wewe unadhani hakuna kazi ya kufanya, atapata kazi ya kufanya tu.

Tungekuwa na mawaziri kama hawa hata kumi tu, tungekuwa tunasogea mbele.

Kwenye kazi ni matendo, longo longo zingine hazitusaidii kabisa. Hongera mkuu Magufuli.

Kuna watu watasagia lakini ukiwauliza wao wamefanya nini? Hakuna cha maana!
 
sasa ana back up kubwa ya kugombea urais 2015 ndiyo mana mtandao wanampotezea kwa kila njia
 
Magufuli ni dume kama Mrema tu; hata umpeleke ambako wewe unadhani hakuna kazi ya kufanya, atapata kazi ya kufanya tu.

Tungekuwa na mawaziri kama hawa hata kumi tu, tungekuwa tunasogea mbele.

Kwenye kazi ni matendo, longo longo zingine hazitusaidii kabisa. Hongera mkuu Magufuli.

Kuna watu watasagia lakini ukiwauliza wao wamefanya nini? Hakuna cha maana!

Hebu tueleze amefanya kitu gani ? yaani mnakuwa kama mmelogwa au ndio wapiga debe ? Tuone samaki washuke bei ,hamna uwezo wa kuvua maji makubwa watu wanavua mnapiga makelele mnaibiwa, habari yenyewe uzushi mtupu ,maana wanaandika wamewakamata watu hata hawaelewi lugha wanayozungumza ,mara unaona kuna mmoja anaitwa Kombo sijui mwengine Ilenoi yaani ndani ya meli mna vibaka kibao wanatoa ushahidi.

Kazi gani mnasifu ,watu wanakwiba ng'ombe na kuvuka nao mipaka ,jamani hakuna hata bahari ni open land mnaenda kukamatiwa kimeli kibovu kina samaki tani tano mnasifu tumeua tembo kumbe nguluwe nchanga.Shahidi anasema kuna mimeli kibao tena mimeli ya kazi haya ndani ya wiki au mwezi tuone hizo nazo zimekamatwa.Kimeli kibovu tu ata rada hazifanyi kazi ,maana sijafahamu rada ya meli nyengine ilikuwa inawasaidiaje wao wakati kwenye bahari meli unaiona kwenye horizon ikitokeza mlingoti tu,na nyie mnalocate vitu vingine kwa kutumia rada yenu ,yaani wanapandikiza uongo na mijamaa inaona kazi kubwa wamefanya kweli wadanganyika hatuelewi hata tunapopakiwa.
 
Tutasema yoote, lakini jamaa anachapa kazi bwana! Pamoja na zengwe la kumuundia wizara ya kitoweo lakini aisee... labda wamground tu, make jamaa ni mbunifu ajabu! sasa hivi uvuvi wa kutumia sumu umepungua kwa sana tu na watu wenyewe wana salimisha hizo zana haramu..

Sasa tusiwe wachoyo wa pongezi, Barabara alizo acha amejenga ndo zinatutoa kimaso maso hadi leo, hata kama wakisema alikuwa akiiba, lakini walau kazi ilionekana! hawa wa sasa sijui hata wanalo lifanya.. sijui wanaiba ama wanaenda lala ofcn tu?

BRAVO MAGUFURI Mungu akupe afya njema uzidi litumikia taifa lako.
 
Hebu tueleze amefanya kitu gani ? yaani mnakuwa kama mmelogwa au ndio wapiga debe ? Tuone samaki washuke bei ,hamna uwezo wa kuvua maji makubwa watu wanavua mnapiga makelele mnaibiwa, habari yenyewe uzushi mtupu ,maana wanaandika wamewakamata watu hata hawaelewi lugha wanayozungumza ,mara unaona kuna mmoja anaitwa Kombo sijui mwengine Ilenoi yaani ndani ya meli mna vibaka kibao wanatoa ushahidi.

Kazi gani mnasifu ,watu wanakwiba ng'ombe na kuvuka nao mipaka ,jamani hakuna hata bahari ni open land mnaenda kukamatiwa kimeli kibovu kina samaki tani tano mnasifu tumeua tembo kumbe nguluwe nchanga.Shahidi anasema kuna mimeli kibao tena mimeli ya kazi haya ndani ya wiki au mwezi tuone hizo nazo zimekamatwa.Kimeli kibovu tu ata rada hazifanyi kazi ,maana sijafahamu rada ya meli nyengine ilikuwa inawasaidiaje wao wakati kwenye bahari meli unaiona kwenye horizon ikitokeza mlingoti tu,na nyie mnalocate vitu vingine kwa kutumia rada yenu ,yaani wanapandikiza uongo na mijamaa inaona kazi kubwa wamefanya kweli wadanganyika hatuelewi hata tunapopakiwa.

Mwiba,

Unaweza kutuita unachotaka, I really don't care. Ninasema ninachokiona, Magufuli hana longo longo na usanii ambao umewajaa wanasiasa na Watanzania walio wengi.

Magufuli ni mchapa kazi na sisi tulivyowajinga eti anachapa kazi ili awe rais, nonsense, hivi kweli mtu huwezi kutimiza wajibu wako bila kuwa na lengo la kuwa rais? Hata kama lengo ni kuwa rais mimi sawa tu ili mradi anatimiza wajibu wake.

Tanzania haiweze kusogea mbele kwa usanii wa majukwaani, lazima isogee mbele kwa vitendo, kwa kuchapa kazi. Mawaziri walio wengi hawana uwezo kabisa wa kuchakarika na kutatua matatizo kwenye wizara zao. Heri mkuu Magufuli anaonyesha njia.

Hayo maneno mnayoyasema sasa tulishayasikia kwa Mrema. Nchi inayumbishwa na waua Albino wachache, angekuwepo Mrema angekomesha hayo mauaji kwa muda mfupi mno.

Tatizo la Tanzania hatujui kuwaunga mkono wale wachache wanaoamua kuchapa kazi na badala yake tunaanza kuwaundia kashfa.
 
.....bwana nani hii ni vigumu sana kutokea,kumbuka Pombe alipelekwa kule kama adhabu fulani hivi...hata kama mafanikio haya ni majumuisho ya tija mbaliX2,Pombe ana kila sababu binafsi ya kufurahi.it just proofs that when you are good U'r good,no matter the environment one is subjected to.
**pombe delivered on Ground,he's doin it on Water,i'm sure he can do the same on Air!!

That was a very good one, we can draw attention to

"...pombe delivered on Ground,he's doin it on Water,i'm sure he can do the same on"
 
No one is 100% perfect! Tutaongea lolote lile tupendalo juu ya Magufuli kwani kuongea ni haki ya kila mtu, lakini ukweli utabaki palepale kwamba Magufuli ni mchapa kazi kwelikweli! Yaani anamsimamo mkali na haogopi mtu wala chochote! Tanzania inahitaji watu kama Magufuli ili ipate maendeleo endelevu!

Hongera Magufuli kwa kazi nzuri unayowafanyia watanzania! Mungu akujalie afya njema ili uzidi kuwatumikia watz, na wala usivunjwe moyo na maneno ya wale wote wanaokusakamasakama kwani wanalao jambo! Tunamuomba Mwenyezi Mungu awasamehe kwani hawajui walitendalo! Ameni!
 
Sam ,

Mimi wala sitaudhunika hata kidogo wakimwondoa huyo Magufuli . Ni nani asiyefahamu ya kuwa yeye ndiye aliye kuwa architect wa kuuza nyumba za serikali kwa bei ya chini kabisa pale oysterbay ? Ni nani asiyejua mpango wake wa kunya'nganya walala hoi viwanja vyao !

Mimi nikiwa mmoja wa victim wa policy mbovu za huyu bwana nitafurahi sana kama wanamtandao watamwondoa !

Muogope Mungu kaka yangu! maandiko matakatifu yanasema samehe saba x sabini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom