Wakuu, tujaribu kuupitia utendaji wa Magufuli katika awamu ya nne na kwa kuanzia naanza na makala hii kutoka gazeti la Tanzania Daima
==========
JANA vyombo vya habari nchini vimechapisha taarifa za ajabu. Taarifa hizi zinasema Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Pombe Magufuli, ametishiwa kuuawa na waandishi wa habari.
Waandishi anaowatuhumu ni Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation, John Bwire, Mhariri wa Rai, Muhingo Rweyemamu na mwandishi wa Rai, Neophitius Kyaruzi. Ametoa taarifa polisi Dodoma Julai, mwaka huu na kupewa RB namba DO/IR/3085/2006.
Katika mashitaka yake, anasema wahariri hao na mwandishi huyo wamemtishia kwa kutumia SMS kuwa watamuua.
Wao katika utetezi wanasema waliwasiliana naye kupata ufafanuzi juu ya taarifa za barabara ya Usagara hadi Geita, zilizoonyesha kuwa kuna mahali hakutenda kwa usahihi, hali iliyoitia serikali hasara.
Magufuli ni waziri aliyepata heshima kweli katika utawala wa Awamu ya Tatu. Aliaminika kutokana na utoaji wa takwimu zilizowavutia wananchi kuona yu kiongozi makini mwenye kustahili heshima, kwani aliwatumikia wananchi kwa mujibu wa matakwa yao. Alipata kusema ametishiwa maisha katika awamu iliyopita na akapewa ulinzi.
Hata hivyo, kitendo cha Magufuli sasa kudai waandishi wa habari wanataka kumuua, sisi kimetutia wasiwasi. Kimetutia wasiwasi, na Magufuli kwa wadhifa wa ofisi ya umma anayoishikilia tunapaswa kumjadili na kuhoji, amekuwaje hadi anapata fikra na kutenda maajabu kama haya?
Magufuli amekuwa waziri wa kwanza duniani au pengine kiongozi anayepaswa kuingizwa kwenye vitabu vya historia kuthubutu, kudai na kutamka kuwa waandishi wanataka kumuua. Haijapata kutokea duniani mwandishi akataka kumuua kiongozi yeyote.
Waandishi ndio huuawa mara nyingi na takwimu na kumbukumbu zilizo katika fikra zetu sahihi zinaonyesha kuwa mwandishi hawezi kabisa hata kufikiri kumuua mtu, bali wao ndio wamekuwa wakiwindwa.
Hatuwezi kumhukumu moja kwa moja, lakini magazeti yameeleza walichofanya wahariri hao na kauli ya Magufuli na uamuzi wake.
Sisi tunapendekeza uchunguzi wa kesi hii usiishie kwenye kuchunguza SMS, Magufuli na waandishi tajwa, wote wafanyiwe uchunguzi wa akili pia, kuthibitisha kama wanao uwezo na wanaendelea kufanya kazi kwa matarajio ya jamii na taaluma wanazozitumikia; uandishi na siasa.
Bila hivyo, hatudhani kama tutapata jibu sahihi. Inawezekana kama waandishi hawa wemefikia hatua ya kumwinda waziri wamuue, basi wachunguzwe huenda wana matatizo ya akili. Wakibainika waondolewe katika kazi hii kabla hawajaliteketeza taifa, lakini pia Magufuli naye apimwe akili. Ikithibitika kuwa hajatishiwa, ametunga na ana akili timamu, aadhibiwe kwa mujibu wa sheria.
CHANZO: Tanzania Daima