Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Mkuu Gembe,

Ufisadi wowote unaanzia kwenye mambo binafsi. Ni ngumu kutenganisha masuala ya wanasiasa na mambo binafsi.

zaidi ya asilimia 50 ya wanasiasa waliondolewa madarakani kwa kashfa, matatizo yao yanatokana na mambo binafsi.

Ukiingia kwenye siasa ni kwamba unaruhusu mambo yako binafsi kuanikwa.

Nafikiri unaelewa uhusiano wa money, power and sex. Hivyo vitu vitatu huwezi kuvitenganisha.
Mtanzania,

Mie nafikiri ni tabia ambayo inabidi tuioinge Vita,Juzi nilikuwa Dodoma katika shughuli zangu za hapa na pale,nimeona jindi wabungwa wanavyokula raha na mabinti wadogo..hii inasikitisha sana na ukizingatia wana eake na watoto,mie nadhani pale katika lile Jengo kuna pepo mbaya ambaye huwa anwapelekea hawa waheshimiwa kuingia katika lindi hii la uzinzi,na Nina uhakika AMama Rwakatale atawasaidia kwa kuwapa Semina na kuwafundisha jinsi ya kuwa na Imani.Kwa maana nyingine huu ni mpango wa Mungu kutuoakoa Watanzania.

wewe hauoni hata wabunge wameeanza kubadilika??
 
Muungwana amteue Mh.Zitto akaweke uzito pale Mahanga nooo ana kaharufu ka ufisadi
Mahanga alirudishwa pale Kwa huruma tu ya Jk,ila hakuwamo katikawale wateule waliotakiwa kuwamo katika barza la mawaziri.

Zitto,
Mwachenio kwanza ajenge chama.
 
Kwa walioko TZ

Hivi yule dada wa UDSM sheria, mwenye RAV4 aliekuwa anakaa MABIBO hostel ameshaolewa na MAGUFULI ? , kwa maana alikwa anajishau kuwa anazimaliza pesa za BARABARA zetu kipindi kile Mh. yuko Miundombinu.

nilidhani topic ilieleweka kumbe kuna watu wasioelewa topic inahusu nini? may I remain silent please!!!
 
Pamaja na vishutuma vidodgovidogo tunavyoambiwa kuhusu JPM, nafikiri katika awamu zote sijaona jamaa aliyeweza kuchapa kazi katika wizara ya ujenzi zaidi yake. Sijui kama kuna mabadiliko yametokea kifedha ktk ile wizara mpaka ikasababisha ujenzi wa barabara zetu zisimame. The way I see it ni udhaifu wa serikali ya Muungwana. Muunnwana alifikiri hii kazi ni rahisi ndiyo sababu alikuwa anatoa ahadi bila kufikiria na kukumbuka kuwa zile barabara zilikuwa zinajengwa kwa juhudi za watu fulani including Nkapa. Sasa yeye alifikiri akiweka ajikaji wake mambo yataendelea kama zamani. Nafikiri mpaka sasa BWM anampiga JK bao katika ufanisi (1-0). By 2015 itakuwa 5-0, beleave me!!!!
 
hilo ni swala la kujiuliza,ila mie sidhani kama Serikali haina Pesa,Pesa ya kuwalipa RDC ilitoka wapi?na Pesa ya Safari za Muungwana Je?au kasma inapewa pesa nyingi kuliko Pesa ya Bajeti ya Wizara ya Barabarara?

I believe Magufuli can make some more Changes,At least Mtu aweze kutoka Mtwara mpaka Mwanza kwa rami.hapo nitafarijika kidogo.Na pia From Dar to Musoma kwa Rami
 
Arudishe kwanza nyumba zetu walizouziana bei poa kwanza ndipo afikiriwe kuwa aliweza pale ama kuweza ni pamoja na kuuza nyumba zetu kwa vigogog na kwa bei poa na sasa wanabomoa na kujenga magorofa huku wafanyakazi wa serikali tukiteseka?

Hafai huyu naye ni fisadi tuu subirini kwenye updated list mtamwona na hakuna atakayekuja tena hapa kumpendekeza.
 
Mzee nafikiri uamuzi wa kuuza nyumba za serikali si wa wizara mmoja bali ni serikali kwa ujumla. Off course sina uhahika njinsi uuzaji ulivyofanyika lakini kwa kawaida nyumba huwa wanauziwa watu wanaoishi kwenye hizo nyumba. Tatizo nafikiri nyumba za serikali zinakaliwa na haohao vigogo. However, this guy so far has never been implicated anywhere with ufisadi pamoja na kukaa kwenye wizara nyeti na tajiri kuliko zote. Imagine kama Chenge, Karamagi, EL, etc wangekuwa pale kwa muda mrefu sijui mambo yangekuwaje??? Jamaa ilikuwa inaifanya ile kazi kwa moyo na alikuwa anaiweza, JK ilifanya janja ili ampunguzie umaarufu, 2010 atampiga chini.
 
hilo ni swala la kujiuliza,ila mie sidhani kama Serikali haina Pesa,Pesa ya kuwalipa RDC ilitoka wapi?na Pesa ya Safari za Muungwana Je?au kasma inapewa pesa nyingi kuliko Pesa ya Bajeti ya Wizara ya Barabarara?

I believe Magufuli can make some more Changes,At least Mtu aweze kutoka Mtwara mpaka Mwanza kwa rami.hapo nitafarijika kidogo.Na pia From Dar to Musoma kwa Rami

Gembe,

Before JK came into power everybody beleaved on that dream. Now things have changed. Wakati ametembelea mitaa ya bondeni nakumbuka JK alikuwa anataja barabara kwa majina na alitoa ahadi kuwa zitakamilika ndani ya miaaka miwili especially za Dar-Lindi na Dodoma - Mwanza. Nafikiri siku hizi hata hazizungumzii hizo barabara, anajua mambo yasha washinda wanapoteza muda tu ili uchaguzi uje watulize tena. JK aturudishie magufuri wetu, wengine wote wameshindwa kazi!!!!
 
Nilishangaa sana JK alipomtoa Magufuli Ujenzi. Nchi hii bila miundo mbinu imara hatutaenda kokote.............na tunahitaji mtu kama Magufuli au zaidi yake (ambaye bado sijamuona).

kuondolewa kwa Magufuli Ujenzi.......influence ya Rostam itakuwa imechangia sana.........and guess what.....angalia wote walioingizwa ktk hiyo position baada ya kutolewa Magufuli wakoje.........jiulize and watch!!

Magufuli ni mchapa kazi na kila atakapopelekwa utasikia vitu vyake........kwa kuwa suala la miundombinu ni sensitive kwa uchumi wetu tunahitaji watu wachapakazi na wenye ARI ya kutimiza yaliyokusudiwa.

.....CCM lazima mkubali kuwa kati ya nguzo zenu bora mlizo nazo moja ni Magufuli....hata Upinzani wanalikubali hilo.......na hii ni kutokana na track record yake akiwa Ujenzi.......

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.....si utani JK mpatie Magufuli Ujenzi uone vumbi lake........na kufikia huko 2010 angalau utakuwa na kitu cha kusemea........kwani mpaka sasa hakuna zaidi ya skandali moja hadi nyingine
 
Mahanga Makongoro atapandishwa

Kwa kulitafakari baraza la mawaziri la JK, kuanzia la kwanza na hili la pili; kuna mwelekeo wa kutoa uwakilishi wa MAENEO au KABILA. Kwa mantiki hiyo kwa kuwa aliyeachia ngazi ni MSUKUMA, basi tutarajie Chapa Ng'ombe mwingine. List ni ndefu, yaweza kuwa MAGUFULI, NGELEJA, MLINGWA etc. Yetu macho na masikio kuanzia leo hii.
 
Ndio,
kuna mtu alibaki,ni Raphael Chegeni..Possibly he might come to take over.Yes I said.
 
Ingawa Jpm Alifanya Upendeleo Kiasi Fulani Katika Ujenzi Wa Barabara Hasa Kujenga Zaidi Kule Kwake,ila Huyu Jamaa Ametulia Katika Ile Nafasi,mpaka Dakika Hii Bado Sijaona Kichwa Kinachoweza Kufuata Nyayo Zake,ila Swali Linakuja Ni Nini Kilimpa Nguvu Katika Kipindi Kile,maana Kipindi Kile,namaanisha Chini Ya Utawala Wa Mkapa,kulikuwa Na Kila Aina Ya Ufisadi,lakini Jamaa Akaonekana Anafanya Kazi Zake Juu Ya Kiwango.kipindi Hiki Cha Kuangamiza Mizizi Ya Ufisadi Jamaa Kazolota Huko Aliko,sioni Kabisa Cheche Zake,au Ndio Anataka Sehemu Ambayo Inaendana Na Fani Yake?ahh...lakini Haina Maana,mzee Wa Kaya Tuletee Huyu Mtu Katika Hii Wizara Iliyomshinda Mzee Wa Vijisent
 
Nilishangaa sana JK alipomtoa Magufuli Ujenzi. Nchi hii bila miundo mbinu imara hatutaenda kokote.............na tunahitaji mtu kama Magufuli au zaidi yake (ambaye bado sijamuona).

kuondolewa kwa Magufuli Ujenzi.......influence ya Rostam itakuwa imechangia sana.........and guess what.....angalia wote walioingizwa ktk hiyo position baada ya kutolewa Magufuli wakoje.........jiulize and watch!!

Magufuli ni mchapa kazi na kila atakapopelekwa utasikia vitu vyake........kwa kuwa suala la miundombinu ni sensitive kwa uchumi wetu tunahitaji watu wachapakazi na wenye ARI ya kutimiza yaliyokusudiwa.

.....CCM lazima mkubali kuwa kati ya nguzo zenu bora mlizo nazo moja ni Magufuli....hata Upinzani wanalikubali hilo.......na hii ni kutokana na track record yake akiwa Ujenzi.......

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.....si utani JK mpatie Magufuli Ujenzi uone vumbi lake........na kufikia huko 2010 angalau utakuwa na kitu cha kusemea........kwani mpaka sasa hakuna zaidi ya skandali moja hadi nyingine

Kimsingi Magufuri ni mchapakazi, ninaweza kusema ni waziri aliyeonyesha mabadiliko makubwa ktk wizara ya miundombinu. kwa wale wanaosafiri mikoa ya Singida, shinyanga na Mwanza watakubaliana kuwa kazi ya magufuri imeonekana. Tukija Ardhi napo amefanya mabadiliko makubwa mno. nilienda kulipa kodi ya kiwanja changu mwaka 2001 wizarani, nilirudi na pesa zangu mkononi bila kulipa foleni ilikuwa ni kubwa mno. Lakini nimeenda mwaka jana nimetumia dakika 10 kukamilisha ulipaji wa viwanja vitatu. Utendaji pale Ardhi ni safi kuna madirisha mengi mengi kama benki ktk lile jengo jipya ukifika utafurahi. Hata wizara aliyoko sasa ataprove kuwa yeye ni mtendaji bado anasoma sheria zinazohusu uvuvi na ndio anavyofanya kazi.
 
Katika Mawaziri hakuna waziri mchapakazi na anayejua nini anachofanya kwa manufaa ya watanzania kama Magufuli. Magufuli sio malaika, ila anajitahidi kwa kiwango cha ubinadamu unavyomruhusu.

Na mengi ya mapungufu yake yanachangiwa na mabosi wake ambao ni Mashetani. Hii nchi hivi sasa inahitaji mtu kama Magufuli kuwa rais,Yuko tayari kuchukua maamuzi mazito bila kusita wala kumwogopa mtu.

Mambo ya vikamati kamati kwenye wizara anazopitia havipo. Umefanya kosa ushahidi upo, anaangalia maandishi yanasemaje unakwenda na maji.

Hatuihitaji Mr. "kutaka kupendwa" tunahitaji mchapakazi
 
Jakaya tulimwambia kabla ya baraza la juzi kuwa wale wote wanaohisiwa kuwa wala rushwa watupwe nje ya baraza.

Magufuri ni kama Mrema ni mla rushwa na hilo JK analijua.

Magufuri amehusika kwenye ufisadi wa kuuza nyumba na aliomba rushwa ili boti za spidi ziende Mwanza.

kwangu mimi Magufuri kuendelea kuwa waziri ni katika kuyalinda mafisadi.

mliokuja hapa kumpigia debe tuambieni nyumba za serikali alivyafanya kuwa mradi wake binafsi. ktk mawaziri wanaotakiwa kuchunguzwa ni huyu Magufuri ili baraza libaki safi.

ndio maana Chenge akasema hivi ni vijisenti kwani anajua Mramba, Magufuri, Mkapa, Yona na Mungai wana mabilioni ya mapesa.
 
Back
Top Bottom