Mods tunaomba hadhi ya Chit Chat forum irudishwe!!

Mods tunaomba hadhi ya Chit Chat forum irudishwe!!

Status
Not open for further replies.
... Pole wana CC kwa kuvamiwa..., mkiona hivyo' elewakuwa watu wanalipenda Jukwaa lenu na kuwaonea wivu, ndiyo maana wanakuja huku kuleta fujo. Yawezekana hao wameshindwa huko kwenye majukwaa mengine, ndiyo maana wanakimbilia kwenu. Bilashaka wameelewa hawata wasumbua tena.
 
Kwa niaba ya wana Chitchat wote nawaomba Moderators wote watusafishie jukwaa letu pendwa kwani limevamiwa na Mamluki....

Hapo awali kabla ya mamluki hao tulienjoy sana jukwaa hili bila BAN zisizo na msingi, lakini sasa tunaingia jukwaa hili kwa wasiwasi wa kupigwa BAN za kusababishiwa...

Nahisi lengo la jukwaa hili lilikuwa zuri tu na ndio sababu likaanzishwa, kama lingekuwa jukwaa la Kipuuzi, kitoto, n.k (kama wasemavyo mamluki hao) Bila shaka lingefulitiwa mbali...

Kwa nini tukose raha katika jukwaa hili??????? Wanaoliona jukwaa la Chitchat haliwafai kwanini wanaingia huku???? Tunawasihi sana kwa Amani na Upendo waendelee kutembelea majukwaa mengine watuwachie jukwaa letu....

Si lazima kutembelea jukwaa hili as kuna majukwaa zaidi ya 50 yenye maana kuliko hili????? Tunakosa raha ya kuwa katika jukwaa hili kwa amani kisa MAMLUKI...

Nakala kwa wana Chitchat woooote!!!!

N.B. Mods msipeleke thread hii kwenye jukwaa la malalamishi ili kila mwanaCC asome na kutoa maoni yake.

Nawasilisha

tatizo sio kwenye red bali nyinyi wenyewe; mnaanzisha thread hovyohovyo(ashakum si matusi);

yani kwa kifupi kila mwana chit chat anapenda kuanzisha pasipo hata na ulazima.
 
Ni kweli kuwa kuna members kwa kukusudia wanapost chuki na kero hadi wengine wanakosa subira. Mfano hai kuna thread humu watu wameporomosheana mitusi mpaka aibu.

Ahsante charminglady kwa kuliona na kulisemea hili kwani kuna membes wengine dahh!!

yani toka watu waanze kutuletea fujo wengine hata kusalimiana tunshindwa maana imekuwa ni fujo mtindo mmoja.......nakusabahi swahiba hata katikati ya hii kadhia
 
Last edited by a moderator:
Heshima ya jukwaa haiwezi kamwe kuletwa kwa matusi na kejeli dhidi ya wale walio na mtazamo tofauti na mwingine anavyo fikiri!
 
dah ki ukweli inakera sana hali hii mi ninvyoona hakuna haja ya mods hapa kwani mods anahukumu kama member anakosa au karipotiwa. HADHI YA CC tuirudishe sisi wenyewe kwani wabaya tumeshawajua tutumie njia ya PM kujulishana nini cha kufanya hapo kama kampeni za miss cc zilivyokuwa zikiendeshwa.
 
... Pole wana CC kwa kuvamiwa..., mkiona hivyo' elewakuwa watu wanalipenda Jukwaa lenu na kuwaonea wivu, ndiyo maana wanakuja huku kuleta fujo. Yawezekana hao wameshindwa huko kwenye majukwaa mengine, ndiyo maana wanakimbilia kwenu. Bilashaka wameelewa hawata wasumbua tena.

Nakubaliana na wewe wivu unawasumbua huku stress free full kucheka
 
... Pole wana CC kwa kuvamiwa..., mkiona hivyo' elewakuwa watu wanalipenda Jukwaa lenu na kuwaonea wivu, ndiyo maana wanakuja huku kuleta fujo. Yawezekana hao wameshindwa huko kwenye majukwaa mengine, ndiyo maana wanakimbilia kwenu. Bilashaka wameelewa hawata wasumbua tena.

Mkuu hii ndo sababu haswaaaa!!!!
 
Heshima ya jukwaa haiwezi kamwe kuletwa kwa matusi na kejeli dhidi ya wale walio na mtazamo tofauti na mwingine anavyo fikiri!

Hivi mnalazimishwa kuingia humu?????? Kama sio viherehere vyenu na vimbelembele vinavyowawasha kuja huku ni nini????

Nendeni kwenye majukwaa yenu ya maana. Sisi tusio na kazi tuacheni mumu humu.......
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom