Wana chit chat mnaikumbuka hili saga lililochafua hali ya hewa chit chat miaka 2 iliyopita?

C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
5,070
3,718
Mnaikumbuka hili saga.Ilitokea miaka 2 iliyopita C.T.U VS Chit Chat.
images

Waraka wa kwanza wa C.T.U kwa wana Chit Chat wote;


Wakuu habari zenu poleni kwa majukumu ya siku nzima.


Leo sina nia ya kuigawanya chit chat wala sina nia ya kuipa msuko suko la hasha.Ila nia yangu ni kuwaambia wana chit chat wote kuwa mna maadui wawili wakubwa wako ndani yenu wanawatafuna.Wote nadhani mnakumbuka siku ya jumapili ya tarehe 20 mwezi huu muda wa saa nane jinsi nilivyochafua hali ya hewa ya chit chat kwenye thread ya Mzungumndali/ Marry hunbag.Niliwaponda sana chitchat kuhusu wao kuwa majobless, wasiokuwa na kazi wala elimu na wanawake niliwasema kuwa sio wazuri.Nadhani mnakumbuka

UHUSIANO WANGU NA CHIT CHAT

Kwanza napenda kuweka wazi mimi kama mimi chitchat niko against nao sana na napenda kuwa challenge sana watu hawa wa chitchat katika thread zao ila napenda tu niweke kuwa nina uhusino mzueri na members wa Chitchat
Kwani huwa tunashirikiana nao mambo mengi katika vitu mbalimbali katika forums mbalimbali zilizomo humu jamvini
Kwanza ieleweke kuwa sina inyongo chochote na wana chitchat.Ila napenda kuwa againts kwa baadhi ya mambo ambayo kwangu huwa nakuwa nina mtazamo tofauti na nitaendelea kuwa challenge… sitachoka… mnizoee

UHUSIANO NA MODS

Kwanza kabisa napenda kuwaambia kuwa mods wamekuwa fair kwangu kwa kipindi chote nilichokuwa ninajiingiza kwenye matatizo na chitchat kwani mods wanajua kabisa uhusiano wangu na wana chitchat kuwa ni mzuri I ndio maana huwa wanan iuliza mara kwa mara kuhusu hivi vitu ninavyopost na huwa navitolea ufafanuzi mzuri na namshukuru mungu kuwa modes wananielewa

WIMBI LA ID MBILIi
Wimbi hili la id mbili limekuwa likiitafuna sana chitchat ila kwa mimi naomba niseme tu wazi kuwa SINA ID MBILI mimi ni msafi ninatumia ID moja tu ya C.T.U. Kwani wapo watu wanaotumia ID mbili wao moja wanajifanya ni wapenzi wa mambo ya chitchat ila nyingine utakuwa yeye ni kuharibu tu. Na kuchafua hali ya hewaMimi naomba nieleweke wazi kuwa sina ID mbili nina double personality naweza kubadilika wakati wowote na kwa muda wowote kwenye post hii naweza kukushushua kwenye post nyingine naweza kukushauri , naweza ku act as a child, naweza kuact as a gentlemen… kwa kifupi my level of maturity ina depend na mtu nayeongea nae kwa wakati huo..sihitaji id nyingine kuongea negative na sihitaji id nyingine kuongea positive

MAADUI WAKUBWA WA CHIT CHAT
Hawa maadui wakubwa wawili wa chitchat wako humu siku nyingi sana na wote ni ma JF Seneor Expert Members mmoja ni mwanamke ambaye yuko huko Dar es salaam na mwingine ni mwanaume ambaye yuko huku MKOANI ila mkoa huo ni jiji hawa maadui ni wa siku nyingi na wako sana chitchat, ni maarufu kiasi kwamba thread nyingi zikianzishwa huwa watu wana wa mention sana.Na wao huanzisha thread zao wenyewe wameshiriki katika activities nyingi sana kama vile Miss chitchat,Kukutana kwenye mikutano mbali mbali kusafiri katika kuchangia, kuandaa na kufanikisha na hata kushiriki katika activities hizo.Hao wamekuwa ni mstari wa mbele sana katika kuchangia mambo mbali mbali ya chitchat ila ni maadui wakubwa sana wa Chit Chat na they work as a team

NIMEJUAJE
Wiki kama tatu zilizopita nilipost kwenye thread moja iliyokuwa ikisema "chitchat inashusha hadhi ya jf" kama sikosei
Nilivyopost kukawa kuna majibizano na member mmoja hapa anayeitwa watu08. Baada ya majibizano haya nikaona kuna mtu amenitumia message kwenye email yangu (nilishawahi kumpa email yangu huyu mdada kipindi fulani nilivyokuwa kwenye jukwaa la business niliweka thread moja na akawa ana interest ya kufanya biashara na mimi nikampa email yangu na tukawa tunachat japokuwa hatukuonana kwani bei ya kitu nilichomwambia kuwa nitamfanyia kilimkimbiza.

Kufungua nikakuta ni yule Member anayetumia jina la kike wa DAR nikashtuka nikihisi amenichamba kwani anasifika kwa kuchamba watu humu ambao wanakuwa against na chitchat.Kufungua nikakutana na ujumbe huu "mkuu nimeona post yako kuhusu chitchat nimependa sana ulivyowapa makavu hawa chit chat,sometimes wanaboa"Mimi nika reply nikasema
"Mkuu ila wewe si mmoja wao tena ulishiriki kumchamba member mmoja wa chitchat (nikamtaja jina) miezi kadhaa iliyopita member huyo nadhani mna kumbukumbu nzuri member aliyechambwa ni yule member ambae AVATAR yake kwa kipindi hiko ilikuwa ni jamaa kavaa kofia huku amenuna kwa kupindisha mdomo wake. Akacheka sana na kusema ile geresha tu mkuu hawa mburura huwa nakuwa nao sana tu ila siwafagilii wala ninibasi tu nitafanyaje

Tuliendelea kuchat kwa muda mrefu ila kuna neno lilikuwa lina ring bell kichwani mwangu
"basi tu nitafanyaje". Nilijiuliza maswali mengi huyu ni nani?
Anataka nini kwa chit chat?
Je ni mwandishi wa habari?
Je ni muuza sukari.
Je ni mwanausalama?
Target ni chitchat?
Je kuna mwanajf anamfuatilia?

Mbona yeye anakuwa ndio yuko mstari wa mbele kwenye kuanzisha ma events mbali mbali?
Anakuwa kama analazimisha kukutana fulani na members wa chitchat.Je kama ni mwana usalama kuna member yeyote wa chitchat alishawahi kuchafua hali ya hewa kule siasani? Nikawa najiuliza.

Kama ni mwandishi wa habari je ni za udaku? Chitchat kuna ma celeb?Au anataka nini huyu mwanamke?Nilishindwa kupata majibu na binafsi sikutaka hata kukutana nae nikaishia tu kumkwepa.Baada ya kuchat kwa muda wa takribani wiki moja aliniandikia message kuwa kuna member mwingine atakutumia message jinsi ya kuwalipua chitchat maana nimependa wewe jinsi ulivyokuwa unawa challenge.Mie nikasema haina shida nitumie then mie nitafanya maujanja yakaisha hapo.

Siku ya jumapili tarehe 20 sina hili wala lile nikatumiwa message kufungua akawa ni yule sasa MEMBER WA KASKAZINI Ujumbe unasema hivi"mkuu (…..) anamtaja yule member wa kike kanituma nikutumie hii message upost kwenye thread ya mzungumndali iko sasa hivi kwenye chitchat. Kufungua ndio ile thread ya mzungumndali na mimi nikapost ambayo mimi niliandika siku ile,kwanza kabisa nilichokifanya ni kupigiga picha ile message kwani device ninayoitumia ina uwezo wa kupiga picha kilichopo kwenye display nadhani watumiaji wa tablets za kisasa watakuwa wanajua hivyo basi;

HIVYO USHAHIDI NINAO:
Ndicho nikapost ile kitu siku ile na baada ya hapo nadhani mnaona upepo wa chitchat ulivyoyumbaSasa swali langu likawa ni hivi huyu mzungumndali ni nani kati ya wale wawili.Kwanini nitumiwe message saa hiyo hiyo mzungumndali kaweka thread yake? wakati najiuliza vile baada ya post yangu ile nilipata pm nyingi sana.Mojawapo ni watu ambao walikuwa wananilaumu kwa ku post vile na wengine walikuwa wananisema vibaya sana mimi niliendelea kuwajibu wale ambao walikuwa tunajibizana kwenye thread ile

Mimi nilikuwa nafanya utani ila kuna watu ambao wali take serious nikajiuliza nini kimetokea? Nikawa sielewi kwani haikuwa mara yangu ya kwanza kuwasema CC vibaya na wana cc wote wanajua kuwa mimi ni Against nao japokuwa tunacheka nao na kushirikiana nao nadhani BABA V NA WATU08 wanajua hili fika.Sasa nikawa najiuliza kuna nini?

Nikafanya utafiti mdogo mdogo na nikagundua kuna message zinatembea PM za baadhi ya member kuonekana kuwa mimi na mzungumndali ni wabaya Hizo message chanzo chake bado sijakijua ila nasikia kuwa ni the same two members
Hao hao nikakaa chini nikaanza kucheka.Jina langu sawa ila na la mzungumndali? Why nikawa sielewi kama either ni one of them au na yeye alitumiwa tu kama nilivyotumiwa mimi

Then nikapata thread kutoka kwa mkuu zebedayo michuzi kusema kuwa niombe msamaha.Nikafikiria nikasema anyway ngoja niombe msamaha kwa sababu kuu kadhaa
1.kuwa piss off members wa cc wakati mimi nilichukulia kama utani
2.kuwafanya baadhi ya members wapate ban kitu ambacho mie sikutaka kabisa.
Nilifanya hivyo wapo walinisamehe wapo ambao hawakunisamehe.


Ila kazi ya wale members 2 ikawa imekamilika KUVURUGA CHITCHAT

SAKATA LA MZUNGUMNDALI KUKATAA KUOMBA MSAMAHA
Nikajiuliza mara mbili mbili huyu mzungumndali ni nani?
Nilijua from the beginning kuwa ni mtu mwenye multiple ID na kweli kesho yake akaumbuka ila nilishtuka kuwa alikuwa ni MARRYHUNBAG ndio alikuwa mwenye id ya mzungumndali ila sasa;
1.kwanini hakuomba msamaha
2.kwanini Yule jamaa wa Arusha alinitumia cha kuandika kwenye ile thread ya marry hunbag?
3. ina maana wao ndio wanacontrol id ya marry hunbag?
4 . au wao walikuwa wanafanya kazi na marryhunbag?
5. ina maana wako wengi humu sio hao tu
6. marryhunbag alikuwa ni mtu mzito humu na hao members wengine wawili ni wazito je kuna wengine wengie ambao ni wazito humu? wako wangapi mie sijui
7. wana mpango gani na cc?

Kwa uelewa wangu ni kuwa hawa jamaa wana mtandao mkubwa sana humu tena sana na wanajichanganya na nyie kila siku na wanawatafuna kimya kimya, wanatoa siri zenu huku, na inawezekana ni watu wa usalama au waandishi wa habari na wanawajaribu kuwasoma baadhi ya members.Kwa manufaa binafsi.Ni kwa habari zilivyotufikia hivi punde zinasema yule wa kike alikuwako WhiteParty.
 
Back
Top Bottom