Mnielimishe: Ni kitu gani haswa Nyerere alikitaka kwenye Muungano, maana nachoona tunapigwa wazi wazi

Kiuhalisia bara ndio imeng'ang'ania mungano sana kuliko wazanzibar, kumbuka hata Nyerere ndie alieenda kumbebeleza Mzanzibar tuwe na muungano, ilibidi kumpa vitu vitamu tamu kama hivi viavyolalamikiwa ili muungano uwepo.
sio bara, bali viongozi wa bara, nao wanang'ang'ania kwa kuogopa, wanahofu hata ya kujadili. ila kama wangekusanya maoni ya wengi, ungeshangaa wananchi ambacho wangekisema.
 
Tengua kauli ni viongozi wenye maslahi binafsi ndio waliong'ang'ania muungano sisi wananchi wa bara hatuutaki muungano mpka kesho

Tunachukua jeshi letu tunawatoa wote wa wa Zanzibar kama wapo kwenye system na tunaliondoa.kule Zanzibar

Tunachukua umeme wetu

Tunachukua ardhi yetu

Kwenye utumishi, uongozi tunawatoa wajitegemee.wao

Tuwaone sasa na hayo ni machache
Kwa taarifa yako, Zanzibar wameshafanya mambo mengi sana kuzidi Tanganyika kwenye kuvunja muungano ikiwemo makongamano, vyama vya siasa kama cuf, kuomba msaada wa umoja wa mataifa, n.k Lakini kwa kuwa wengi wao hawana nguvu za kimadaraka, inakuwa ngumu

Hilo jeshi (JWTZ) ni jeshi la pande mbili Tanganyika na Zanzibar, kwa taarifa yako wapo wazanzibar wengi wa kutosha huko jeshini.

Jeshi lipo chini ya amiri jeshi mkuu ambae ni Raisi wa nchi, hio kauli yako ya kusema " tunachukua jeshi letu" haina mantiki.

Yaonekana hata elimu ya kawaida kabisa ya civics inakupiga chenga mkuu, Ni jambo inalowezekana kutamatisha muungano ila inabidi taratibu maalum zifatwe, sio kirahisi rahisi tu kama unavyofikiria.
 
ni mojawapo ya matokeo ya hovyo ya vita baridi. mabeberu wa magharibi waliona zenji inakwenda kuwa cuba katika bahari ya hindi, wakashinikiza muungano.
 
View attachment 2029458

Naombeni wenye jicho la ziada mnitoe ujinga maana huu ujinga nilionao ndio unanifanya niwe napatwa na hasira kwa maono mafupi yanayonifanga nione Zanzibar inatunyonya

Kwa upeo wangu mfupi najionea mambo haya, Naombeni mnipe maarifa, huenda mtazamo wangu haupo sawa.

Mambo ya huku bara lazima yawe na mchanganyiko wa mtanganyika na mzanzibari kuanzia ajira, uongozi, jeshini, mahakama, n.k kwenye uongozi kukiwa na msaidizi wa bara basi mkuu inabidi awe wa Zanzibar, kwenye ajira nako katika kila ajira 100 basi 21 za wazanzibar, jeshini huko wapo wengi pia sana sana polisi na jwtz, ila sasa huko kwao mambo yao ni ya wao hawataki mchanganyiko, hapa Tanganyika tunanufaika kivipi????

Ukija kwenye ardhi, wazanzibari kibao wanamiliki mashamba makubwa na viwanja huku bara lakini mtanganyika harusiwi kufanya hivyo, Je tunanufaika kivipi??

Ukija kwenye Power, hakuna kabila wala kundi linalowafikia wala kuwasogelea wazanzibar, yani si mchaga wala msukuma wala kabila lolote unaloweza kulifikiria, hawa wenzetu wapo wachache lakini wamesambazwa si mchezo kwenye vyeo vizito. kuna mawaziri, wakuu wamikoa, wakuu wa wilaya, ma rpc, vyeo vikubwa jwtz, mabalozi wa nchi za nje, majaji wa mahakama, maprofesa vyuoni, waajiriwa kwenye mashirika yenye mishahara minono kama bandarini, Bot, Tanapa, Tra, Nssf, n.k hii ni kwasababu muungano unahitaji mchanganyiko wa pande mbili.

Mtanganyika hana nafasi kwenye serikali ya zanzibar kuanzia kwenye uongozi, ajira, mahakama, n.k Wana serikali yao kwajili yao kuanzia uraisi, makamu wa raisi, spika wa bunge, n.k hawa inabidi wawe wa zanzibar. pia wana taasisi zao kama Zff ambayo ni kama tff ya huku, Zrb ambayo ni kama Tra ya huku, Zssf ambayo ni kama Nssf ya huku, Jku ambayo ni kama jkt ya huku, yani taasisi zipo kibao kwakweli, hizo taasisi zinatoa ajira kwa wazanzibar tu, mtu wa Tanganyika huna sifa, lakini cha ajabu mzanzibar anaweza kupata ajira pande mbili za bara na huko kwao, vya bara ni vya wote ila vya zanzibar ni vya wao pekee, Patamu happ aisee 🤔🤔

Kwa maono yangu haya ambayo ni kwasababu ya kukosa maarifa, najionea tunapigwa nje ndani mbele ya macho yangu.

Wataalam wa haya mambo mnipe maelezo ili nipate ahueni.
Kuna jambo moja tu ambalo linafanya hali iwe ilivyo mpaka sasa:
1. Uwoga wa kufanya maamuzi- Katika awamu zote, jambo hili linaonekana wazi wazi kuwa na tatizo na malalamiko kibao, ila kila mtu anafikiri akifanya maamuzi yeye ndiye atakuwa kavunja Muungano.
2. Apparently, kelele ndogo toka upande wa visiwani inaogopwa kuliko kelele kubwa upande wa bara. Tumeaminishwa kwamba Zanzibar kulingana na nafasi yake kijiografia ni muhimu sana kwa nchi yetu, hivyo lazima tuwe na mamlaka ndani ya visiwa. Ukweli wa mambo ni kuwa mtazamo huu ni wa kizamani sana , kwani usalama wa eneo siku hizi unategemea teknolojia na weledi wa jeshi lako, na sio ukaribu
 
Tanganyika mlishoboka tu....ndo mkome. Na bado...kofia zote Zanzibar na kwenu tumezi hold

Ni mtu mjinga pekee ndio anafikiria hivyo. Unachokiona juu ya maji ni kitu kidog kuliko kilichojificha chini yake. Usalama ilikuwa issue muhimu sana wakati ule. Na bado ni issue muhimu mno.
Ardhi ya Zanzibar ni kidogo na watu wanazaliana mno. Usipofanya hivyo, kunaweza kukawa hakukaliki. Ila Tanganyika nayo inajaa. Hii hali ya sasa tusiichukue kimchezo mchezo. Kuna kesho yenye mambo yake kadhaa. Kwa watu wasiofikiria sana, kugombana ndio suluhisho bora kwao
 
Kwa taarifa yako, Zanzibar wameshafanya mambo mengi sana kuzidi Tanganyika kwenye kuvunja muungano ikiwemo makongamano, vyama vya siasa kama cuf, kuomba msaada wa umoja wa mataifa, n.k Lakini kwa kuwa wengi wao hawana nguvu za kimadaraka, inakuwa ngumu

Hilo jeshi (JWTZ) ni jeshi la pande mbili Tanganyika na Zanzibar, kwa taarifa yako wapo wazanzibar wengi wa kutosha huko jeshini.

Jeshi lipo chini ya amiri jeshi mkuu ambae ni Raisi wa nchi, hio kauli yako ya kusema " tunachukua jeshi letu" haina mantiki.

Yaonekana hata elimu ya kawaida kabisa ya civics inakupiga chenga mkuu, Ni jambo inalowezekana kutamatisha muungano ila inabidi taratibu maalum zifatwe, sio kirahisi rahisi tu kama unavyofikiria.
Hii comment yako inaonyesha mahaba uliyo nayo kwenye nchi yako
 
Nyerere alikuwa anajaribu kuwatongoza ili baadae wakubali serikali moja au kuukubali muungano ndiyo maana aliwapa incentives kibao, lakini nao wakawa wajanja, hawakukubali kukiachia kilicho chao, matokeo yake leo Tanganyika lipolipo kama bwege linaliwa

Pili Nyerere alitaka aonekane kwa wenzie kuwa ni Pan Africanist, mtu wa unity kwa Africa

Ila kiukweli wazenji wanatupiga, tena wanatupiga huku wakijifanya kulalamika sana kuwa eti sisi ndo tunawaonea wao
 
Hii comment yako inaonyesha mahaba uliyo nayo kwenye nchi yako
Si afadhali ya huyu kaonesha mahaba na nchi yake kuliko wewe ulioshindwa kunyesha mahaba Kwa nchi yako,ukaonesha chuki kwa kuwaita machotara, karne hii unapanda basi la ubaguzi
 
Mkuu una uhakika mbara hawa ajiliwi?
Labda kwenye taasisi za muungano zilizopo Zanzibar kama Polisi, Air Tanzania, n.k. huko kwengine kwenye mambo ya serikali yao ni ngumu, wamewekwa wachache sanawanaohesabika ili kuzuga tu.

Matangazo ya ajira za Zanzibar, sifa ya kwanza ni lazima uwe raia wa Zanzibar.
 
Nyerere alikuwa na lengo moja tu kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara wa Zanzibar waje kuwekeza Tanzania bara uwekezaji mkubwa serikali ipate Kodi kwani wazawa kipindi kile wakiwemo wachaga matongitongo ya kufanya biashara kubwa yakikuwa yamejaa hayajaamka .Wachaga walikuwa migombani tu kulima kahawa wamelala fofo kibiashara.Akaona heri alete wazanzibari waje huku kwa wingi bara apate Kodi ya kuendesha serikali na alifanikiwa Hadi leo wafanyabiashara wakubwa Wenye biashara kubwa na viwanda vikubwa bara Ni wazanzibari kuanzia akina Bakhresa nk wameshika sekta kubwa ziwe usafiri,mafuta,viwanda nk

Wachaga Ni wachuuzi yaani machinga waliochangamka kuliko machinga wa makabila mengine

Kwa kulipa Kodi TRA wazanzibari walioko bara wanaoongoza kuliko waswahili wote watanganyika

Nyerere aliangalia zaidi TRA kuukubali huu muungano mnaouona umekaa mguu kushoto ukiwa kulia na wa kulia ukiwa kushoto.

Ukiwaangalia kiingiacho TRA Hadi leo Huwezi mtu kubali muungano uvunjike kirahisi hivi ukiuvunja halafu Bakhresa arudi kwao Zanzibar Mswahili yupi mtanganyika aweza kuwa na mtaji na uwezo wa kuendesha business chain kubwa za Bakhresa kuhakikisha TRA inapata chake bila athari? Wata take over Nani Hawa malofa akina Lisu wapiga Domo ambao hata kufuga kuku tu wa biashara watano hawawezi kazi kubweka tu kuwa muungano mbaya? Mkono mtupu haulambwi

Nyerere alikubali muungano wa aina ilyopo akijua mkono aulambao una kitu.Mfano tukisema tulambe mkono wa Chadema wasiotaka muungano una Nini? Mbowe ana Nini,Lisu ana Nini,Msigwa ana Nini? Chadema wengi choka mbaya wamepigika kimaisha wanaishi kwa kuchonga midomo tu
 
KUHUSU kuzidiwa akili Mpaka Leo hawajui kama walituzidi akili!Wanapambana wavunje muungano sidhani kama ukivunjwa kutakuwa na faida upande wowote
 
View attachment 2029458

Naombeni wenye jicho la ziada mnitoe ujinga maana huu ujinga nilionao ndio unanifanya niwe napatwa na hasira kwa maono mafupi yanayonifanga nione Zanzibar inatunyonya

Kwa upeo wangu mfupi najionea mambo haya, Naombeni mnipe maarifa, huenda mtazamo wangu haupo sawa.

Mambo ya huku bara lazima yawe na mchanganyiko wa mtanganyika na mzanzibari kuanzia ajira, uongozi, jeshini, mahakama, n.k kwenye uongozi kukiwa na msaidizi wa bara basi mkuu inabidi awe wa Zanzibar, kwenye ajira nako katika kila ajira 100 basi 21 za wazanzibar, jeshini huko wapo wengi pia sana sana polisi na jwtz, ila sasa huko kwao mambo yao ni ya wao hawataki mchanganyiko, hapa Tanganyika tunanufaika kivipi????

Ukija kwenye ardhi, wazanzibari kibao wanamiliki mashamba makubwa na viwanja huku bara lakini mtanganyika harusiwi kufanya hivyo, Je tunanufaika kivipi??

Ukija kwenye Power, hakuna kabila wala kundi linalowafikia wala kuwasogelea wazanzibar, yani si mchaga wala msukuma wala kabila lolote unaloweza kulifikiria, hawa wenzetu wapo wachache lakini wamesambazwa si mchezo kwenye vyeo vizito. kuna mawaziri, wakuu wamikoa, wakuu wa wilaya, ma rpc, vyeo vikubwa jwtz, mabalozi wa nchi za nje, majaji wa mahakama, maprofesa vyuoni, waajiriwa kwenye mashirika yenye mishahara minono kama bandarini, Bot, Tanapa, Tra, Nssf, n.k hii ni kwasababu muungano unahitaji mchanganyiko wa pande mbili.

Mtanganyika hana nafasi kwenye serikali ya zanzibar kuanzia kwenye uongozi, ajira, mahakama, n.k Wana serikali yao kwajili yao kuanzia uraisi, makamu wa raisi, spika wa bunge, n.k hawa inabidi wawe wa zanzibar. pia wana taasisi zao kama Zff ambayo ni kama tff ya huku, Zrb ambayo ni kama Tra ya huku, Zssf ambayo ni kama Nssf ya huku, Jku ambayo ni kama jkt ya huku, yani taasisi zipo kibao kwakweli, hizo taasisi zinatoa ajira kwa wazanzibar tu, mtu wa Tanganyika huna sifa, lakini cha ajabu mzanzibar anaweza kupata ajira pande mbili za bara na huko kwao, vya bara ni vya wote ila vya zanzibar ni vya wao pekee, Patamu happ aisee 🤔🤔

Tukubali kwamba wazanzibar WALITUZIDI AKILI na sasa wanafaidi dili nono la muungano
Kwa upeo wangu nimegundua Karume alimzidi akili Nyerere, Alipoona kwamba Nyerere anambembeleza sana kuwe na muungano, Karume akatumia nafasi hii kumbana Nyerere aipe Zanzibar upendeleo kama huu tunaouona ama sivyo hauna muungano, Pia akaongezea kipengere kwamba endapo kukiwa na muungano basi Zanzibar iwe kwajili ya Zanzibar lakini Tanganyika ibanwe iwe kwajili ya wote, Mhh naandika huku achozi yananilenga aisee!! Kwa lugha nyepesi "changu ni changu ila chako tutagawana" matokeo yake leo Tanganyika tunashuhudia inapigwa nje ndani na wazanzibar licha ya malalmiko kuwa eti wao ndo wanaonewa
Muulize Lukuvi atakujibu, alikwishalisema hilo kanisani
 
Back
Top Bottom