Mnielimishe: Ni kitu gani haswa Nyerere alikitaka kwenye Muungano, maana nachoona tunapigwa wazi wazi

Mbaya zaidi likitoka tangazo la ajira huku bara, basi waombaji wa huku bara watachujwa kwa vigezo kama ufaulu, experience, hadhi ya chuo, n.k. na kiukweli wahitimu wapo wengi sana na ushindani ni mkubwa sana.

Ila kwa upande wa wenzetu huko kwanza wapo wachache, kigezo kikubwa kinakua uraia ili ajira nao wapate ionekane kuwa zimetolewa kimuungano zaidi.
si nilisikia juzi wazanzibar kuanzia sasaivi watapewa asilimia kubwa kweli ya ajira kuliko wabara, tena hukuhuku bara? yaani wao wilaya yenye watu hata milioni 3 hawajafika wanataka wapate ugali sawa kwenye sahani na nchi yenye watu zaidi ya 55 million. kwanini tunawalea sana hivi? Watanganyika tutaamka lini?
 
binafsi najua hili litaibuka tu kwenye kampeni za uchaguzi 2025, ni madukuduku yamekaa mioyoni mwa wabara miaka mingi, na ukweli ni kwamba pamoja na kwamba wazenji wanalialia kila wakati, kwa jinsi walivyojiwekeza huku bara, muungano ukifa wao watapata hasara na maumivu makubwa kuliko hata sisi. naisubiri sana hiyo siku watembee kwa mguu hadi zanzibar.
 
Mzee mihangwa alidai kwenye makala zake kwenye Rai kipindi kile kwamba marekani na uingereza walimuogopa mjaa babu kule zenji,ili zenji isiwe Cuba ya afrika mashariki palikua na machaguo mawili,iunganishwe na bara idhibitiwe,au ishambuliwe,alhamdulillah ikaunganishwa,baada ya kitisho Cha ujamaa nadhani tukawa na hofu ya uislam,maana kipindi hicho palikua na msemo ngoma ikipigwa zenji,afrika mashariki yote inacheza
 
Naombeni wenye jicho la ziada mnitoe ujinga maana huu ujinga nilionao ndio unanifanya niwe napatwa na hasira kwa maono mafupi yanayonifanga nione Zanzibar inatunyonya

Kwa upeo wangu mfupi najionea mambo haya, Naombeni mnipe maarifa, huenda mtazamo wangu haupo sawa.

Mambo ya huku bara lazima yawe na mchanganyiko wa mtanganyika na mzanzibari kuanzia ajira, uongozi, jeshini, mahakama, n.k kwenye uongozi kukiwa na msaidizi wa bara basi mkuu inabidi awe wa Zanzibar, kwenye ajira nako katika kila ajira 100 basi 21 za wazanzibar, jeshini huko wapo wengi pia sana sana polisi na jwtz, ila sasa huko kwao mambo yao ni ya wao hawataki mchanganyiko, hapa Tanganyika tunanufaika kivipi????

Ukija kwenye ardhi, wazanzibari kibao wanamiliki mashamba makubwa na viwanja huku bara lakini mtanganyika harusiwi kufanya hivyo, Je tunanufaika kivipi??

Ukija kwenye Power, hakuna kabila wala kundi linalowafikia wala kuwasogelea wazanzibar, yani si mchaga wala msukuma wala kabila lolote unaloweza kulifikiria, hawa wenzetu wapo wachache lakini wamesambazwa si mchezo kwenye vyeo vizito. kuna mawaziri, wakuu wamikoa, wakuu wa wilaya, ma rpc, vyeo vikubwa jwtz, mabalozi wa nchi za nje, majaji wa mahakama, maprofesa vyuoni, waajiriwa kwenye mashirika yenye mishahara minono kama bandarini, Bot, Tanapa, Tra, Nssf, n.k hii ni kwasababu muungano unahitaji mchanganyiko wa pande mbili.

Mtanganyika hana nafasi kwenye serikali ya zanzibar kuanzia kwenye uongozi, ajira, mahakama, n.k Wana serikali yao kwajili yao kuanzia uraisi, makamu wa raisi, spika wa bunge, n.k hawa inabidi wawe wa zanzibar. pia wana taasisi zao kama Zff ambayo ni kama tff ya huku, Zrb ambayo ni kama Tra ya huku, Zssf ambayo ni kama Nssf ya huku, Jku ambayo ni kama jkt ya huku, yani taasisi zipo kibao kwakweli, hizo taasisi zinatoa ajira kwa wazanzibar tu, mtu wa Tanganyika huna sifa, lakini cha ajabu mzanzibar anaweza kupata ajira pande mbili za bara na huko kwao, vya bara ni vya wote ila vya zanzibar ni vya wao pekee, Patamu happ aisee 🤔🤔

Kwa maono yangu haya ambayo ni kwasababu ya kukosa maarifa, najionea tunapigwa nje ndani mbele ya macho yangu.

Wataalam wa haya mambo mnipe maelezo ili nipate ahueni.
Mlikataa katiba ya warioba Serikali 3 acheni kulia lia chukueni hatua
 
Mzee mihangwa alidai kwenye makala zake kwenye Rai kipindi kile kwamba marekani na uingereza walimuogopa mjaa babu kule zenji,ili zenji isiwe Cuba ya afrika mashariki palikua na machaguo mawili,iunganishwe na bara idhibitiwe,au ishambuliwe,alhamdulillah ikaunganishwa,baada ya kitisho Cha ujamaa nadhani tukawa na hofu ya uislam,maana kipindi hicho palikua na msemo ngoma ikipigwa zenji,afrika mashariki yote inacheza
eti East Africa yote inacheza,
 
Tatizo nyie vijan hamuelewi...........nyerere aliona mbari sana for security reasons kwasababu hata leo hii zanzbar wakijitenga hawata survive coz watakua week kijeshi................kitendo cha nyerere kuleta muungano ni kutaka ku access eneo kubwa la bahari ya hind
Kumbe Nyerere alikuwa amelenga bahari lakini mbona kama mijamaa inaufaidi muungano kuliko siye
 
Tatizo nyie vijan hamuelewi...........nyerere aliona mbari sana for security reasons kwasababu hata leo hii zanzbar wakijitenga hawata survive coz watakua week kijeshi................kitendo cha nyerere kuleta muungano ni kutaka ku access eneo kubwa la bahari ya hind
Hii sababu ni kwa mujibu wa ulivyoambiwa na hao wahenga, tueleze leo kwa akili zako mwenyewe nini maoni yako?
 
Naombeni wenye jicho la ziada mnitoe ujinga maana huu ujinga nilionao ndio unanifanya niwe napatwa na hasira kwa maono mafupi yanayonifanga nione Zanzibar inatunyonya

Kwa upeo wangu mfupi najionea mambo haya, Naombeni mnipe maarifa, huenda mtazamo wangu haupo sawa.

Mambo ya huku bara lazima yawe na mchanganyiko wa mtanganyika na mzanzibari kuanzia ajira, uongozi, jeshini, mahakama, n.k kwenye uongozi kukiwa na msaidizi wa bara basi mkuu inabidi awe wa Zanzibar, kwenye ajira nako katika kila ajira 100 basi 21 za wazanzibar, jeshini huko wapo wengi pia sana sana polisi na jwtz, ila sasa huko kwao mambo yao ni ya wao hawataki mchanganyiko, hapa Tanganyika tunanufaika kivipi????

Ukija kwenye ardhi, wazanzibari kibao wanamiliki mashamba makubwa na viwanja huku bara lakini mtanganyika harusiwi kufanya hivyo, Je tunanufaika kivipi??

Ukija kwenye Power, hakuna kabila wala kundi linalowafikia wala kuwasogelea wazanzibar, yani si mchaga wala msukuma wala kabila lolote unaloweza kulifikiria, hawa wenzetu wapo wachache lakini wamesambazwa si mchezo kwenye vyeo vizito. kuna mawaziri, wakuu wamikoa, wakuu wa wilaya, ma rpc, vyeo vikubwa jwtz, mabalozi wa nchi za nje, majaji wa mahakama, maprofesa vyuoni, waajiriwa kwenye mashirika yenye mishahara minono kama bandarini, Bot, Tanapa, Tra, Nssf, n.k hii ni kwasababu muungano unahitaji mchanganyiko wa pande mbili.

Mtanganyika hana nafasi kwenye serikali ya zanzibar kuanzia kwenye uongozi, ajira, mahakama, n.k Wana serikali yao kwajili yao kuanzia uraisi, makamu wa raisi, spika wa bunge, n.k hawa inabidi wawe wa zanzibar. pia wana taasisi zao kama Zff ambayo ni kama tff ya huku, Zrb ambayo ni kama Tra ya huku, Zssf ambayo ni kama Nssf ya huku, Jku ambayo ni kama jkt ya huku, yani taasisi zipo kibao kwakweli, hizo taasisi zinatoa ajira kwa wazanzibar tu, mtu wa Tanganyika huna sifa, lakini cha ajabu mzanzibar anaweza kupata ajira pande mbili za bara na huko kwao, vya bara ni vya wote ila vya zanzibar ni vya wao pekee, Patamu happ aisee

Kwa maono yangu haya ambayo ni kwasababu ya kukosa maarifa, najionea tunapigwa nje ndani mbele ya macho yangu.

Wataalam wa haya mambo mnipe maelezo ili nipate ahueni.
Wanasema eneo la kimkakati reference China na Taiwan, Spain na Cataluna Barcelona.
 
Kuna mawazo yanaweza kuwa sawa leo lakini miaka ya mbele ukitafakari kwa kina unaona kabisa hayakuwa sawa
Nyakati zinabadilika na fikra za binadamu zinabadilika pia
Mtazamo wa leo unaweza kua bora lakini kesho ukawa tofauti kulingana na ukuwaji na upanukaji wa fikra za binadamu .

Mwalimu Nyerere na karume waliweza kuonekana mawazo yao yalikuwa bora kipindi kile lakini leo yanaonekana kuwa na kasoro kubwa kutokana na kukua kwa fikra na mtazamo wa wananchi wa leo.
Umewahi kudadisi kabla Karume hajatangulia mbele za haki huo mwaka alikuwa na mawazo gani kuhusu Muungano? Nimesikia aliwahi kusema haya "Muungano ni kama koti likikubana unalivua"...
 
Kiuhalisia bara ndio imeng'ang'ania mungano sana kuliko wazanzibar, kumbuka hata Nyerere ndie alieenda kumbebeleza Mzanzibar tuwe na muungano, ilibidi kumpa vitu vitamu tamu kama hivi viavyolalamikiwa ili muungano uwepo.
Tengua kauli ni viongozi wenye maslahi binafsi ndio waliong'ang'ania muungano sisi wananchi wa bara hatuutaki muungano mpka kesho

Tunachukua jeshi letu tunawatoa wote wa wa Zanzibar kama wapo kwenye system na tunaliondoa.kule Zanzibar

Tunachukua umeme wetu

Tunachukua ardhi yetu

Kwenye utumishi, uongozi tunawatoa wajitegemee.wao

Tuwaone sasa na hayo ni machache
 
Back
Top Bottom