Mnielimishe: Ni kitu gani haswa Nyerere alikitaka kwenye Muungano, maana nachoona tunapigwa wazi wazi

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
10,911
2,000

Naombeni wenye jicho la ziada mnitoe ujinga maana huu ujinga nilionao ndio unanifanya niwe napatwa na hasira kwa maono mafupi yanayonifanga nione Zanzibar inatunyonya

Kwa upeo wangu mfupi najionea mambo haya, Naombeni mnipe maarifa, huenda mtazamo wangu haupo sawa.

Mambo ya huku bara lazima yawe na mchanganyiko wa mtanganyika na mzanzibari kuanzia ajira, uongozi, jeshini, mahakama, n.k kwenye uongozi kukiwa na msaidizi wa bara basi mkuu inabidi awe wa Zanzibar, kwenye ajira nako katika kila ajira 100 basi 21 za wazanzibar, jeshini huko wapo wengi pia sana sana polisi na jwtz, ila sasa huko kwao mambo yao ni ya wao hawataki mchanganyiko, hapa Tanganyika tunanufaika kivipi????

Ukija kwenye ardhi, wazanzibari kibao wanamiliki mashamba makubwa na viwanja huku bara lakini mtanganyika harusiwi kufanya hivyo, Je tunanufaika kivipi??

Ukija kwenye Power, hakuna kabila wala kundi linalowafikia wala kuwasogelea wazanzibar, yani si mchaga wala msukuma wala kabila lolote unaloweza kulifikiria, hawa wenzetu wapo wachache lakini wamesambazwa si mchezo kwenye vyeo vizito. kuna mawaziri, wakuu wamikoa, wakuu wa wilaya, ma rpc, vyeo vikubwa jwtz, mabalozi wa nchi za nje, majaji wa mahakama, maprofesa vyuoni, waajiriwa kwenye mashirika yenye mishahara minono kama bandarini, Bot, Tanapa, Tra, Nssf, n.k hii ni kwasababu muungano unahitaji mchanganyiko wa pande mbili.

Mtanganyika hana nafasi kwenye serikali ya zanzibar kuanzia kwenye uongozi, ajira, mahakama, n.k Wana serikali yao kwajili yao kuanzia uraisi, makamu wa raisi, spika wa bunge, n.k hawa inabidi wawe wa zanzibar. pia wana taasisi zao kama Zff ambayo ni kama tff ya huku, Zrb ambayo ni kama Tra ya huku, Zssf ambayo ni kama Nssf ya huku, Jku ambayo ni kama jkt ya huku, yani taasisi zipo kibao kwakweli, hizo taasisi zinatoa ajira kwa wazanzibar tu, mtu wa Tanganyika huna sifa, lakini cha ajabu mzanzibar anaweza kupata ajira pande mbili za bara na huko kwao, vya bara ni vya wote ila vya zanzibar ni vya wao pekee, Patamu happ aisee

Tukubali kwamba wazanzibar "WALITUZIDI AKILI" na wanafaidi mno muungano bila kujijua.

Kwa upeo wangu nimegundua Karume alimzidi akili Nyerere, Alipoona kwamba Nyerere anambembeleza sana kuwe na muungano, Karume akatumia nafasi hii kumbana Nyerere aipe Zanzibar upendeleo kama huu tunaouona ama sivyo hakuna muungano, Pia akaongezea kipengere kwamba endapo kukiwa na muungano basi Zanzibar iwe kwajili ya Zanzibar lakini Tanganyika ibanwe iwe kwajili ya wote, Kwa lugha nyepesi "changu ni changu ila chako tutagawana" matokeo yake leo Tanganyika tunashuhudia inapigwa nje ndani na wazanzibar, haya malalamiko kutoka Zanzibar kwamba wananyonywa yaliwekwa kimkakati ili iwe silaha kwa wazanzibar kuridhika na kujitapa kwamba wametuzidi akili, ingekuwa hivi muungano ungekufa mapema. lakini pia haya malalamiko yapo kimkakti kuizubaza Tanganyika idhani kwamba Zanzibar ni kama mkoa wake kumbe kiukweli wazanziba ndio wanaonufaika.
Nyerere alikuwa na roho nzuri,alisaidia nchi nyingi,kuzikomboa,hakujali Rangi,dini,ukabila,hata wapalestina aliwasaidia,na mpaka leo wanamkumbuka kwa mema yake.
 

Escrowseal1

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
2,976
2,000
Mkuu 'Escrowseal1', umegusia habari ya "KERO ZA MUUNGANO".

Kwa ufahamu wangu najuwa kero zote hadi hii leo zinatoka upande mmoja wa muungano.

Kwa hiyo unaposema "hao vichwa vinavyoangalia kero upande wetu havioni kuwa hiyo ni kero", ujuwe kwamba hakuna vichwa vya upande wetu (bara). Hakuna kero hata moja iliyokwishawasilishwa kutoka upande wa bara.

Nadhani sasa ni wakati mwafaka kabisa kuanza kuwasilisha hizi kero zinazolalamikiwa mara kwa mara toka upande huu, ili nazo zianze kushughulikiwa na hivyo vichwa.
Dah huu ni ubwege Kwa hiyo miaka yote kumbe Kero za muungano zinaelea Ndani ya Mashua tu. Hii si haki hata kidogo
 

RAISI AJAYE

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
3,762
2,000
Muungano haukuwa Takwa la nyerere bali takwa la nchi za kibepari kama uingereza wakihofia nchi za ujamaa zisije zikaichukua Zanzibar na kuwa koloni la ki -socialist!!!!Nyerere kama kijana Mwaminifu alitumwa kuichukua Zanzibar iwe chini ya himaya ya kibepari!!Hata Neno Tanzania Lilitengenezwa na wao mabepari!!!
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
12,922
2,000
Muungano haukuwa Takwa la nyerere bali takwa la nchi za kibepari kama uingereza wakihofia nchi za ujamaa zisije zikaichukua Zanzibar na kuwa koloni la ki -socialist!!!!Nyerere kama kijana Mwaminifu alitumwa kuichukua Zanzibar iwe chini ya himaya ya kibepari!!Hata Neno Tanzania Lilitengenezwa na wao mabepari!!!
EeenHeee!
Wewe una ufahamu wa kipekee kabisa.
Hebu andika kitabu cha historia hiyo mkuu, tutakisoma.
 

Escrowseal1

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
2,976
2,000
Mbona hatusikii wazanzibari kulalamika tena kero zao za muungano kama ilivyo kawaida yao, wamenyuti kimyaa safari hii , waje walalamike wapewe nchi huru kamili ijitegemee kama walivyokua wanadai zamani haki yao, sie wabara tutakua pamoja nao kwa hilo kuwasupport
Haaaa haaaa support ya kufungua minyororo
 

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
4,014
2,000
Asilimia kubwa ya wanaharakat na wanasiasa wa zanzibar wenye ushawish nyakat hizo walikua ni wasomi walioelimika kutoka nchi za kikomunist na misimamo yao ilikua ni muelekeo huo ukizingati kwa nyakat zile presha ilikua kubwa mno kati ya ukomunist na umagharib na ndio maana ukatumika muungano ili kuwapiga pini ref;kwa heri Uhuru kwa heri ukoloni by Ghassany km sijakosea
Kama ingekua hivo .....unazan why Tz ili adopt socialism
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom