Mnaopenda kuomba Namba za Simu za Wanawake ndani ya Daladala muwe mnachunguza kama Madume zao tupo nao au hatupo

Yaani hakuna Kitu Mwanamume wa Mkoani Mara hakipendi kama Mwanamke wake Mweupe Kutongozwa hovyo Mitaani.
Udhaifu uko kwa mwanamke wako. Mwanamke yeyote anayejitambua hawezi kuwa approached mpaka ikakera bila yeye kutaka. Najua ni kweli wanawake wengi hasa wazuri huwa wana-attract sana ''maombi'' kwa wanaume lakini mwanamke yeyote mwenye kujielewa kama hataki ni rahisi sana ku-react kwa namna ambayo itamfanya mwanaume akomee hapo hapo anapoanza. Ila kama ni hawa wanawake akina ''mbona leo sijasemeshwa nimeamka na mkosi gani'', kama inavyoonekana wa kwako yuko kwenye hilo kundi, watafanya kitu ambacho mwanaume atapata moyo wa kuendeleza mapambano.
 
Ni hivi hakuna mwanamke ambaye ana lebo au amepigwa chapa kubwa huyu ni mwanamke wa Flani mimi nikikuta mwanamke nimevutiwa nae natongoza vizuri tu, na kingine mwanamke ambaye ntamuacha ni Yule mwenye pete ya ndoa tu maana najua huyo yuko kwenye taasisi takatifu lakini mwanamke kuniambia ana mtu na hajaolewa mi naruka nae.

AF sio kila mtu wa Kupiga maana wengine unaweza shangaa unataka kumpiga ukapigwa wewe, sasa Siku jichanganye uingie pasipoingilika
 
Atakua ishengoma huyo wanaume wa muleba wana matatizo sana, Juzi nilikutana na Kyaruzi ananilazimisha nimpe namba mbele za watu nilijiskia fedheha mno.

Waha nao wana tabia hizo hizo sijui wakoje.
Mbona wa muleba unawaonea BossLady ulikuwa unatoka muleba unaenda wap
 
Alhamdullilahi namshukuru Mola Muumba wa vyote kwa kunijaalia mafanikio ya kutunukiwa Degree ya Pili (2nd Dan) ya Sanaa ya Kujilinda kwa Mikono Mitupu ama Karate mtindo wa Jundokan Goju Ryu kutoka kwa Mwalimu wetu Mkuu wa @jundokan_tanzania Sensei @fundi_romi_ siku ya Ijumaa Juni 17, 2022.

ANGALIZO: Jamani ndugu zangu sanaa hii ni ya kujilinda kiafya, kiakili, kinidhamu na ki-utii na sio kupigana na mtu au watu. Ndio maana nina miaka takriban 40 nafanya Karate lakini hadi sasa ni wachache kweli waliojua nacheza sanaa hio.

Ni kweli kabisa sikupenda na sikuwa najionesha hadharani kwamba mimi ni Karateka, na hii kutoka hadharani sasa ni kuwatia moyo na hamasa watu wa umri wowote ama jinsia yoyote kwamba Karate ni sanaa ya kujilinda kiafya, kiakili na kinidhamu. Mie imenisaidia sana kwa kweli!

Ukikuta Karateka mbabe au mpenda shari basi tambua kuwa huyo jamaa ni aidha feki au hajaiva kisawasawa.

Kwa mwenye nia ya kujiunga nasi karibu DM kwa maelezo kamili.

Sanaa nzuri sana hii kwa afya ya mwili na akili.
 
Kwahiyo nyie na Minyege yenu mkipanda tu Dala Dala na kuona Wanawale wazuri (warembo) wamepanda (wapo) mnadhani kuwa pembeni zao au nyuma zao tunaowamiliki kwa Kutukuka hatupo hivyo mnaona ni njia nyepesi ya Kuwaomba Namba zao za Simu?

IGP Sirro kuna Raia wako Mmoja leo asubuhi ndani ya Dala Dala nimemuonyesha ni kwanini Marehemu Bruce Lee alipokufa aliniachia Urithi wake na kwa nilichomfanya Matumaini yangu ni kuwa kwa muda huu lazima atakuwa amepumzisha ICU au huenda hata Ndugu zake wanasikilizia kama waanze Kuweka Oda za Sanda na Maturubai Kwao.

Yaani unapanda Dala Dala unamlazimisha kabisa Mwanamke akupe namba yake ya Simu na kila akikataa na kukuambia kuwa ana Mtu wake (tena hadi Jina kakutajia kuwa anaitwa GENTAMYCINE wa JamiiForums) halafu Wewe humuamini na unaendelea tu Kumlazimisha huku ukimshika shika tu unategemea Mwanamume wa Mkoani Mara (Musoma) nikuchekee huku nikiwa namiliki Mkanda wangu Mweusi huu?

Na najua hata akipona atakuwa anawaona Wanawake wote tu kama Kituo cha Polisi huku akiwaheshimu zaidi. Halafu sijui hata kwanini nilisahau kumuuliza anatokea Kabila gani (lipi) ila kwa mwonekano wake ni lazima tu atakuwa ama ni Mhaya au Mnyiramba au Muha au Mnyaturu au Mrangi au Mkara au Mnyamwezi kwani ndiyo Wanaume na Makabila yenye huu Upuuzi.

Ninatumai kabisa kuwa wana JamiiForums nyote leo mmeamka Salama. Ninawapenda na muwe na Siku Njema nyote.
kwa kweli inakera, kutongoza mimi ishanishinda.
natengeneza mtego mtu anase, yeye ndo aniombe namba
 
Back
Top Bottom