Aina za wanaume ambao huwa changamoto kwa wake zao

Denis1729

Member
Sep 9, 2021
34
109
Kila ndoa ina changamoto zake,

na maana halisi ya ndoa ni ule uwezo wa wana ndoa kuvumiliana katika changamoto hizo. Kuna changamoto za kimungu ambazo wana ndoa hawawezi kuziepuka.

lakini kuna zile za kiu anadamua mbazo nyingi ni za ki makusudi na mtu huamua tu kuwa hivyo.
Katika kuangalia ndoa.

leo nimeona nichambue aina kumi za waume ambao wake zao wanakereka kuwa nao kama ifuatavyo;-

1.Wanaojiona Kama Wafalme (King Husband);

HIi ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa, Hawafanyi chochote ndani ya nyumba, kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo.

Mwanamke hana kauli ndani, na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea.

2.Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband);

Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote, Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui,
mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha.

Hajali kama ana mke,
na muda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake.

3.Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband);

Hawa hukasirika kila mara tena bila kuwa na sababu ya misngi,
mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida, ni kununa kutwa nzima, wanahasira na ni rahisi kumpiga mke.

4.Mume Wa Kila Mtu
(Genarel Husband);

Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wa kike wa mwanamke na wa kwao kuliko wanavyowajali wake zao.

Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela,
lakini rafiki akampa.
Wana marafiki wengi wa kike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida.

5.Wanaume Wanaojifanya Wagumu
(Dry Husband);

Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani.

Hakuna kuongea na hawajali hata hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua,
ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha weke zao.

6.Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao
(Panadol Husband);

Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke, wanapotaka mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta vizawadi, wanajua udhaifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai, kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama wana wake, hawajali tena.

7.Wanaume Ambao Hawataki Kukua
(Baby Husband);

Bado wana tabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na kile.

Yaani wakiongea kitu na mke ni lazima aulize ndugu kwanza ndiyo kipitishwe, na mke akifanya kosa kidogo kazi ni kulinganisha mke na ndugu zake, mbona fulani alifanya hivi, fulani anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo.

Kwa kifupi hawawezi kufanya maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa Mama yake anakuwa kama shememu ya ndoa.

8.Mume Mtalii
(Visiting Husband);

Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu, lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala, ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wa wiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja ambacho anafanya na mkewe au watoto wake, kila akiingia tu anakuwa na safari ya kutoka, yaani hata atoke akakae nje tu lakini si kukaa na mke au watoto.

9.Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu
(Stalking Husband);

Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu mwanamke anachofanya, na hawampi pumzi.

Akienda sehemu atachunguza anaenda na nani?na alikutana na nani?

huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti.

Kila mtu mwanamke anayeongea naye wa jinsia tofauti huhisi ni mchepuko, na hata marafiki wa mke wa kike pia huhisi wanamkuwadia, kwa kifupi hampi pumzi mwanamke.

10.Mwanaume Mbahili
(Miserly Husband);

Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu.

Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni. Sukari ikiisha anataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia hela labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela. Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa, na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake.

Hiyo ni baadhi tu ya aina ya wanaume ambao wanawake wengi wasingependa kuwa nao

Kama mwanaume upo hivyo jua mke wako hafurahii na anavumilia tu.

Ndoa ni furaha, amua kubadilika na usimfanye mke wako kuishi na wewe kwa kujilazimisha. Kama ni mume jiulize uko namba ngapi hapo, na kama ni mke mezea namba ya mumeo na jua hauko peke yako.
 
Mtoa mada hiyo point ya kwanza umesema mume hataki kufanya chochote ndani ya nyumba mfano alitakiwa kufanya nini??
Kama hamna maji bafuni apelekewe(hata kama kaamka kabla ya mkewe).
Kutoa takataka nje siku gari inapita,madai Sio kazi yake.
Mkewe hayupo hawez kujisevia msosi au kupika kakitu kadogo ale,ni bora amsubiri arudi,akale baa au alale njaa yani. Na hapo ka amepikiwa mke akatoka utakuta chombo kichafu palepale mezani au kwa sinki,no appreciation.
Vitu vidogo vidogo kama hivyo.
 
Kila ndoa ina changamoto zake,
na maana halisi ya ndoa ni ule uwezo wa wana ndoa kuvumiliana katika changamoto hizo. Kuna changamoto za kimungu ambazo wana ndoa hawawezi kuziepuka,
lakini kuna zile za kiu anadamua mbazo nyingi ni za ki makusudi na mtu huamua tu kuwa hivyo.
Katika kuangalia ndoa,
leo nimeona nichambue aina kumi za waume ambao wake zao wanakereka kuwa nao kama ifuatavyo;-

1.Wanaojiona Kama Wafalme (King Husband);

HIi ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa, Hawafanyi chochote ndani ya nyumba,
kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo.
Mwanamke hana kauli ndani,
na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini,
wote kimya hakuna hata kuongea.

2.Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband);

Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote, Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui,
mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha,
na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha.

Hajali kama ana mke,
na muda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake.

3.Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband);

Hawa hukasirika kila mara tena bila kuwa na sababu ya misngi,
mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida,
ni kununa kutwa nzima, wanahasira na ni rahisi kumpiga mke.

4.Mume Wa Kila Mtu
(Genarel Husband);

Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wa kike wa mwanamke na wa kwao kuliko wanavyowajali wake zao.
Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela,
lakini rafiki akampa.
Wana marafiki wengi wa kike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida.

5.Wanaume Wanaojifanya Wagumu
(Dry Husband);

Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani.
Hakuna kuongea na hawajali hata hisia za mke,
mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua,
ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha weke zao.

6.Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao
(Panadol Husband);

Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida,
wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke, wanapotaka mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta vizawadi,
wanajua udhaifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai, kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama wana wake,
hawajali tena.

7.Wanaume Ambao Hawataki Kukua
(Baby Husband);

Bado wana tabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao,
mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na kile.
Yaani wakiongea kitu na mke ni lazima aulize ndugu kwanza ndiyo kipitishwe,
na mke akifanya kosa kidogo kazi ni kulinganisha mke na ndugu zake,
mbona fulani alifanya hivi,
fulani anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo.
Kwa kifupi hawawezi kufanya maamuzi na mkewe,
ndugu zake hasa Mama yake anakuwa kama shememu ya ndoa.

8.Mume Mtalii
(Visiting Husband);

Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile,
mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu,
lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala,
ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa,
hata mwisho wa wiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja ambacho anafanya na mkewe au watoto wake,
kila akiingia tu anakuwa na safari ya kutoka,
yaani hata atoke akakae nje tu lakini si kukaa na mke au watoto.

9.Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu
(Stalking Husband);

Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu
mwanamke anachofanya,
na hawampi pumzi.
Akienda sehemu atachunguza anaenda na nani?na alikutana na nani?
huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti.
Kila mtu mwanamke anayeongea naye wa jinsia tofauti huhisi ni mchepuko,
na hata marafiki wa mke wa kike pia huhisi wanamkuwadia, kwa kifupi hampi pumzi mwanamke.

10.Mwanaume Mbahili
(Miserly Husband);

Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu,
Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni. Sukari ikiisha anataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia hela
labda akajenge kwao,
huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela. Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa,
na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake.

Hiyo ni baadhi tu ya aina ya wanaume ambao wanawake wengi wasingependa kuwa nao,
Kama mwanaume upo hivyo jua mke wako hafurahii na anavumilia tu.

Ndoa ni furaha,
amua kubadilika na usimfanye mke wako kuishi na wewe kwa kujilazimisha. Kama ni mume jiulize uko namba ngapi hapo,
na kama ni mke mezea namba ya mumeo na jua hauko peke yako.
Sawa
 
Kuna Mwanaume atakosa hapo?, labda awe malaika cha muhimu mwanamke n kumpata anayeendana nae
 
Back
Top Bottom