Dr Matola PhD
Platinum Member
- Oct 18, 2010
- 61,429
- 108,580
Milioni na uhai wangu vina connection gani?Kukosa milioni sio mwisho wa maisha na wewe hapo una milioni si ajabu unatamani hata kesho ufe kwa stress ulizonazo ila mie naenjoy tu na kidogo nilicho nacho
Don't take me serious utajiumiza bure, kila jambo lina wakati wake na hata umri unamata pia.
Wakati nikiwa nikiwa kwenye umri wa late 20's nilikuwa na usongo sana na maisha ili nimiliki pesa nyingi, Babu yangu ni dealer wa mafuta nilikuwa nikikaa naye bar tunapiga kiraji aliniuliza nimtajie Tajili yeyote ambaye ni self made ambaye ana umri wangu.
Nilishindwa kumpa jibu maana matajili wote wanaanzia 40-50 kwenda juu.
Back to ur point inawezekana wewe pia bado ni mdogo upo kwenye umri wa mapito mengi lakini utakuja kuwa vile ungependa uwe.