MMU hot talk

MMU hot talk

unaikumbuka MOTEL AGIP??? nakumbuka burger zao na chicken chips!

Ah hiyo yeyote aliyezaliwa na kukulia Dar lazima aijue.

Bila kusahau Oysterbay hotel (haipo tena siku hizi), Palm Beach na kadhalika.
 
Halafu nimeona mlikuwa mnamzungumzia marehemu Mwinuka yule b-baller. Alikuwa anaitwa Henry au Hope Mwinuka.

Najua A level alisoma SRSS

Hope Mwinuka ndiye alikuwa na nickname ya Dudu (R.I.P) na ni kaka mkubwa wa Henry...
 
Henry huyu alicheza sana Savio enzi hizo inatamba kwa ligi ya b-ball, nafikiri sasa hivi ni coach...
 
Hope Mwinuka ndiye alikuwa na nickname ya Dudu (R.I.P) na ni kaka mkubwa wa Henry...

Okay, najua Hope alikuwa ni dunker mzuri sana (kwa wakati ule). Na najua alisoma SRSS intake ya kina Jump Around
 
Ah hiyo yeyote aliyezaliwa na kukulia Dar lazima aijue.

Bila kusahau Oysterbay hotel (haipo tena siku hizi), Palm Beach na kadhalika.

Palm beach ndio pekee imefanikiwa kuwemo kwenye kizazi hiki cha digital..... hahahah ni sawa na sisi tulivokomaa JF na watoto wa digitali LOL

Komredi una kumbukumbu ya hatari... Bush Trekker..... duh!!
 
kweli kabisa hiyo embassy hotel ilikuwaga wapi?

Embassy Hotel ndio sasa imepata mdau inakarabatiwa, zamani tulikuwa tunaenda kumuona muigizaji wa nyimbo za papa wemba na mwanzilishi wa bendi ya Diamod sound wana kibinda nkoi, hapo mwenge kufika ilikuwa sh. 100 tu watoto wa papa Fred Rwegasira walikuwa wakiturusha roho kwa kucheza pichu za boxer , enzi hizo kibinda hakuwepo bendi inafuata hapo, wakian diana astoni villa, kamuke sukari, elly rogomba, liliani internet, safu ra rapa, mulumba kashama, mpiga soro elly kinyama, walikuwa wakipiga pamba balaa. Wengi tumeikumbuka Motel agip waanzilishi wa andaz za donati, ukila moja hakuna kula mchana, sasa hivi jengo linafanana na la kufugia kuku.
 
Back
Top Bottom