Watu saba wamefariki dunia na wengine 64 wajeruhiwa vibaya na baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la mizigo.
Ajali hiyo iliyotokea jana kati ya saa 4.30 na saa tano usiku katika Kijiji cha Utaho,tarafa ya Ihanja,wilaya ya Singida vijijini ililihusisha basi la Adventure lenye namba za usajili T.576 ABL aina ya Scania lililokuwa likisafiri kutoka Dar-es-Salaam kwenda Mwanza kugongana uso na lori la mafuta.
Marehemu wawili tu ndiyo mpaka sasa waliokuwa wametambuliwa kwa majina ambao ni Edita Elisha na mwingine ametambulika kwa jina moja tu la mzee Kipara.
Hata hivyo habari zaidi zimesema kati ya majeruhi hao waliolazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu,31wapo kwenye Hospitali ya Mkoa wa Singida wakati kwenye hospitali ya misheni ya Mtakatifu Maria kuna majeruhi 33.
Majeruhi ni pamoja na Amina Twalibu(41) mkazi wa Kigoma,Robert Wilsoni (37)mkazi wa Kigoma,Lameck Habibu (48) mkazi wa Kigoma,Samsoni Shadrack(40),mkazi wa Kigoma,Huseni Simoni (38)mkazi wa kigoma,Toda Jumanne(26) mkazi wa Kigoma,Mary Lotenga(18) mkazi wa Kigoma,Olbert
Ernesti(15) mkazi wa Kigoma,Mwanahawa Twalibu (18)mkazi wa Kigoma na Ramadhani Hassani(41) mkazi wa kigoma.
Wengine ni Maguno Bakari (28) mkazi wa Kigoma,Haruna Juma(54) mkazi wa
Kigoma,Michaeli Julius(23) mkazi wa Kigoma,Phenusi Jonathani(32) mkazi wa Kigoma,Hamadi Milongo(43) Kigoma,Roxima Protasi (26) mkazi wa Ujiji,Benard Francis (32) mkazi wa Kigoma,Muhile Emanueli(32) mkazi wa Kigoma,Nestory Salumu (48) mkazi wa Kigoma na Jeraldi Marcel (34) mkazi wa Kigoma.
Kwa mujibu wa Bi Kaluba wengine ni Revocatus Philibert (20) mkazi wa Kigoma,Elia Ntinyaku (31) mkazi wa Kigoma,Eliasi Eliudi (20) mkazi wa Kasulu,Renatus Mkarunga (44) mkazi wa Kigoma,Mikidadi Kongwe(23) mkazi wa Kigoma,Jumanne Mtaba (30) mkazi wa Kigoma,Husseni Yasini (34) mkazi wa Kigoma,Musa Danieli (34) mkazi wa Kasulu,Mwimbwa Ladiscaus (53) mkazi wa Kigoma,Bestina Methew (16) mkazi wa Kigoma na Walivyo Athumani (17) mkazi wa Kigoma.