Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Nadhani ingekuwa ni kufumaniwa, lazima magazeti ya udaku yangeishupalia sana habari hii, kwani wao ndiyo kazi yao na wana watu wao karibu kila mji, ukizingatia kuwa habari za udaku wa wakubwa huwa zina mashabiki wengi sana.

Nakumbuka Mengi alipofumaniwa, gazeti la Sanifu (sasa halipo) liliandika! Nalaila Kiula alipofumaniwa magazeti kadhaa likiwemo Kasheshe yaliandika! Ditopile Ukiwaona Mzuzuri alipofumaniwa, magazeti yaliandika! Slaa alifumaniwa Dodoma, magazeti yaliandika! Kwa nini yasiandike habari hii iwapo mkuu alifumaniwa, tena wakati wa mwezi mtukufu? Kuhusu dereva ni kwamba, habari zinasema mheshimiwa sana Mudhihir, alikuwa anaendesha yeye mwenyewe hilo shangingi lake, dereva hakuwa kazini, mara mtu akakatiza mbele wakati mheshimiwa yuko katika spidi kubwa, na mkuu akafunga breki za ghafla. Gari ndipo ilipopinduka!

Off-course naungana na wengine kwamba, kwa mtu ambaye amepata ajali mbaya kiasi cha kukatika mkono lazima kuna maeneo mengine mwilini yangekuwa nyang'anyang'a kwa mzinga ule, sio mkono tu.

Aidha tungeona nyuzi kadhaa kichwani ama sehemu nyingine, kwa hiyo huenda ukweli wa kufumaniwa kwa mkuu na mke wa mtu na kukatwa mkono ukawa na mantiki fulani vile!
Lisemwalo lipo!
 
mmmhhh hapa patamu kweli, ila nadhani wenye details bado hawajaitembelea hii thread. MM uko wapi utumulikie hapa ili tuone vizuri? tunaona picha iko blurred!
 
Kama kuna mtu anaweza pata contact za m2 aliye Lindi... anaweza kuthibitisha kwa kiasi fulani..... ni kweli inatia shaka.
 
Would you sacrifice your hand to save your ass? That is a biggest question a man can answer!
 
aisee sikujua kuwa JF yaweza pia kuwa na mashushu humu humu!ila picha yaja kabsaaa kuwa it is impossible ajali itokee gari lisonekane,kwanza mheshimiwa aendeshe gari mwenyewe??haya basi tuonyeshwe na eneo ajali ilipotokea hata wasamaria **** help!alafu kweli ajali itokeee ukatike hadi mkono kabsaaa bila kuwa na michubuko hata usoni na other sehemu za wazi kuonekana!!
 
..kuna hoja ya kujibu hapa..kwani lindi hakuna wapiga picha..wakaenda kwa kamanda wa traffic mkoa kupiga hiyo picha?? pia tunatambua watu wa bima lazima wapige picha na polisi lazima wapige picha...kama picha ya gari lake haipo basi jamaa lazima atakuwa ameliwa kiboga na kukatwa mkono juu..unafikiri mke wa ntu nchezo kwa hao chiteme wala chimumunye hapo hapo ulipooo!!!
 
Kwa utafiti wangu nilioufanya kwa takwibani miaka 9 sasa nilipojingiza ktk udereva ili kutafiti kwa undani nimegundua 98% ya ajali ni uzembe wa madereva(a)kutokuwa na ujuzi wa kutosha(b)Uchovu(dereva asiendeshe zaidi ya masaa 6 bila kupumzika nashauri kwa safari ndefu wawe wawili(c)Madereva akijua kesho anasafiri asiende kulewa,dansi chochote kinachoweza kumchosha mfano mzuri marubani wako makini sana katika hili..Mungu awalaze mahali pema peponi na majeruhi wapone haraka amen
 
Barabara nyingi za Tanzania ni nyembamba sana. Wakati mwingine inakuwa shida hata kupisha, especially kama barabara iko kwenye tuta, kuna mteremko na mbele yako linakuja kwa kasi basi ambalo limekaa katikati ya barabara. Mara nyingi tu imenibidi nipunguze mwendo, au nisimame kabisa kuwapisha wehu hao!
 
Hivi Highway ya DSM-Moro-Tanga-Arusha/Moshi-Iringa Mbeya..tumeshindwa kuwe 4 ways tangu UHURU?...hadi sasa ni 2 way na bado Singida road
 
Pamoja na kuwa habari inaonekana ni ya kitambo kidogo, lakini ajali zinatisha, hakuna pa kukimbilia si kwenye reli wala majini.

1.Baada ya ajali kutokea, ni nani huwa anagharimia huduma za matibabu (eg kama wale walipelekwa kule mission)
2. Je huwa wanalipwa fidia? na wenye magari? au insurance policy haicover? je insurance policy zilizopo nyumbani zinaweza kutumika kucover medical bills na disabilities compansation e.g kama mtu akikatika kiungo 'anunuliwe kiungo cha bandia na insurance'
 
Labda niulize hapa kwa vile ndo imetokea, hivi wataalamu wa ICT hamna jinsi ya kuweka tarehe inayo onyesha mada imepostiwa lini? kama inawezekana, basi ikiwekwa kwa kila ukurasa ikawa inajionyeha automatik itasaidia sana hata kwa mchangiaji kujua hii habari ni ya sasa ama ya mwaka 47!
kama inawezekana please! kwani mie upande huo not richabo!
 
Jamani wanaJF especially waliochamgia leo kwenye hii mada.
Kwa nini tunakuwa kama Six, tusome kwa makini kwanzia mwanzo.

Hii post iliwekwa na Bubu M. Ovyo tarehe 8 Sept.2007.

Wakati mwingine nashawishika kukubali nadharia isemayo watanzania ni wavivu kusoma kama Six alivyodhihirisha mwenyewe.

Mimi bado naamini sisi (JF) na wengine siyo wavivu lakini hizi post za leo mhhhh.....
 
Nadhani kuna watu wanachanganya... kuna magazeti yameripoti leo habari kutoka Mbeya kuwa kuna ajali imetokea.. ngoja nicheki na Kamanda Kova nitawajulisha inawezekana ni magazeti yameandika habari ya mwaka 47 bila kujua kwani sijaona gazeti jingine lolote lenye habari hiyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom