Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Huyo jamaa kachanganya habari. Habari ya ajali ya jana iko kwenye gazeti la mwananchi la leo, ambayo ni hii hapa chini:
___________________________________

Ajali Mbeya yaua wawili, yajeruhi 39
Na Brandy Nelson, Mbeya


WATU wawili walikufa jana papo hapo na wengine 39 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kushindwa kufunga breki na kudumbukia katika bonde la mahindi katika Kijiji cha Inyala mkoani Mbeya kwenye Barabara Kuu ya Mbeya- Iringa.

Ajali hiyo ambayo ilisababishwa na basi la Kampuni ya Sumry lilokuwa na namba za usajili T875 ANN ilitokea majira ya saa mbili asubuhi wakati likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam.

Waliokufa katika ajali hiyo ni wanawake wawili akiwemo mpitanjia, Mariam Burton na mwingine ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja na miili yao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Aidha, majina ya majeruhi mpaka jana hayakuwa yamepatikana, lakini idadi ya ambao wamelazwa 39 akiwemo kondakta wa gari hilo wakati majeruhi wengine walitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Kwa mujibu wa baadhi ya abiria waliokuwapo katika basi hilo walidai kuwa dereva alikuwa akiendesha gari akiwa katika mwendo wa kasi na kulazimisha kuyapita magari yaliyokuwa mbela yake yakiwemo malori matatu yaliyokuwa yameongozana hatua iliyowafanya abiria kumlalamikia wakitaka apunguze mwando.

Abiria hao waliendelea kudai kuwa dereva huyo alipofika katika eneo la tukio ambalo ni mteremko wenye kona hakupunguza mwendo wa basi hilo huku mbele yake kukiwa na gari aina ya Land Rover na kulazimisha kulipita bila kuangalia mbele kama kuna gari linalokuja.

Mara baada ya ajali, dereva wa basi hilo alitoroka, lakini askari polisi walifanikiwa kumkamata na sasa anashikiliwa kwenye Kituo Kidogo cha Polisi cha Inyala akisubiri kupelekwa kituo cha kati jijini Mbeya.

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limethibitisha kutokea kwa ajali na basi hilo lilifanikiwa kuondolewa kutoka bondeni.

Source: Mwananchi
 
Sidhani kama ni kweli, isingeweza fichwa kiasi hiki, itakuwa ni ajali iliyokuja kwake moja kwa moja, kama adhabu toka kwa maulana wetu tumuombaye, kwa kidomodomo chake cha kupinga watetezi wetu wanyonge na kuwatetetea mafisadi!

Ujue Mungu wetu yu hai, tukimuomba anasikia, malipo ni hapa hapa duniani, hilo ni fundisho kwake, na amini usiamini hata angekuwa na tray ya mayai mle kwenye gari lisingevunjika hata moja! Ni mkono wake tu uliotakiwa iwe kielelezo na kwa wengine wote wenye tabia hiyo!
 
sehemu ilipotoke ajali nilionyeshwa mwaka jana nilipokuwa Lindi kikazi,Ni karibia na mjini na ukiangalia kwa makini si sehemu ambayo ingetokea ajli kubwa sababu ni kwenye kona na kuna lama za barabarani kwamba lazima spidi iwe 50.sual la kujiuliza je Alichukuliwa hatua zipi baada ya kugundulika alikuwa anaendesha gari kwa kasi wakati kibao kinaonesha hairuhusiwi?
 
sehemu ilipotoke ajali nilionyeshwa mwaka jana nilipokuwa Lindi kikazi,Ni karibia na mjini na ukiangalia kwa makini si sehemu ambayo ingetokea ajli kubwa sababu ni kwenye kona na kuna lama za barabarani kwamba lazima spidi iwe 50.sual la kujiuliza je Alichukuliwa hatua zipi baada ya kugundulika alikuwa anaendesha gari kwa kasi wakati kibao kinaonesha hairuhusiwi?

Au alikuwa anafukuzwa???

1. Kwanini alikuwa anaendesha yeye mwenyewe?
2. What are the updates za masuala haya?
 
Niliwai kusikia,alifumaniwa na mke wa mtu,akapewa choice mbili,kukatwa mkono au kufanyiwa kitu mbaya na wanaume wenzie na kutangazwa kwenye magazeti akachagua kukata mkono wakasisitiza lazima uwe wa kulia ndo akakatwa.sijui kama ni kweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Watu saba wamefariki dunia na wengine 64 wajeruhiwa vibaya na baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la mizigo.

Ajali hiyo iliyotokea jana kati ya saa 4.30 na saa tano usiku katika Kijiji cha Utaho,tarafa ya Ihanja,wilaya ya Singida vijijini ililihusisha basi la Adventure lenye namba za usajili T.576 ABL aina ya Scania lililokuwa likisafiri kutoka Dar-es-Salaam kwenda Mwanza kugongana uso na lori la mafuta.

Marehemu wawili tu ndiyo mpaka sasa waliokuwa wametambuliwa kwa majina ambao ni Edita Elisha na mwingine ametambulika kwa jina moja tu la mzee Kipara.

Hata hivyo habari zaidi zimesema kati ya majeruhi hao waliolazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu,31wapo kwenye Hospitali ya Mkoa wa Singida wakati kwenye hospitali ya misheni ya Mtakatifu Maria kuna majeruhi 33.

Majeruhi ni pamoja na Amina Twalibu(41) mkazi wa Kigoma,Robert Wilsoni (37)mkazi wa Kigoma,Lameck Habibu (48) mkazi wa Kigoma,Samsoni Shadrack(40),mkazi wa Kigoma,Huseni Simoni (38)mkazi wa kigoma,Toda Jumanne(26) mkazi wa Kigoma,Mary Lotenga(18) mkazi wa Kigoma,Olbert
Ernesti(15) mkazi wa Kigoma,Mwanahawa Twalibu (18)mkazi wa Kigoma na Ramadhani Hassani(41) mkazi wa kigoma.

Wengine ni Maguno Bakari (28) mkazi wa Kigoma,Haruna Juma(54) mkazi wa
Kigoma,Michaeli Julius(23) mkazi wa Kigoma,Phenusi Jonathani(32) mkazi wa Kigoma,Hamadi Milongo(43) Kigoma,Roxima Protasi (26) mkazi wa Ujiji,Benard Francis (32) mkazi wa Kigoma,Muhile Emanueli(32) mkazi wa Kigoma,Nestory Salumu (48) mkazi wa Kigoma na Jeraldi Marcel (34) mkazi wa Kigoma.

Kwa mujibu wa Bi Kaluba wengine ni Revocatus Philibert (20) mkazi wa Kigoma,Elia Ntinyaku (31) mkazi wa Kigoma,Eliasi Eliudi (20) mkazi wa Kasulu,Renatus Mkarunga (44) mkazi wa Kigoma,Mikidadi Kongwe(23) mkazi wa Kigoma,Jumanne Mtaba (30) mkazi wa Kigoma,Husseni Yasini (34) mkazi wa Kigoma,Musa Danieli (34) mkazi wa Kasulu,Mwimbwa Ladiscaus (53) mkazi wa Kigoma,Bestina Methew (16) mkazi wa Kigoma na Walivyo Athumani (17) mkazi wa Kigoma.
 
Mola azilaze roho za marehemu pahala pema!

Hivi haya mabasi bado yanaruhusiwa kusafiri usiku?
 
Watu saba wamefariki dunia na wengine 64 wajeruhiwa vibaya na baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori la mizigo.

Ajali hiyo iliyotokea jana kati ya saa 4.30 na saa tano usiku katika Kijiji cha Utaho,tarafa ya Ihanja,wilaya ya Singida vijijini ililihusisha basi la Adventure lenye namba za usajili T.576 ABL aina ya Scania lililokuwa likisafiri kutoka Dar-es-Salaam kwenda Mwanza kugongana uso na lori la mafuta.

Poleni wakazi wa kigoma,
Sijui nani wa kulaumiwa, Abiria, Dereva, Trafic wa usalama barabarani.
Serikali iangalie umuhimu wa kuanzisha insurance kwa ajili ya matibabu yatokanayo na ajali.
Dereva au mwenye gari wanatakiwa wagharimie matibabu pamoja na fidia ya hao abiria.

Kwa njia ile jinsi mabasi yanavyojaza, hiyo idadi ya abiria inawezekana iko underestimated.
 
Mungu awalaze mahali pema peponi wale wote waliofariki kwenye ajali hiyo, na pia nawaombea majeruhi wapone haraka.

Huu ni uzembe mwingine wa Madereva wetu na kwa mara nyingine Roho za watu wasio hatia zimepotea bure. by the way huo muda mabasi hayaruhusiwi kusafiri kwa sheria zetu au ilishafutwa?
 
Jamani Bongo!!! Poleni sana wafiwa na Mungu awape rehema.
The ishu na nchi yetu ni barabara....we need 2-way traffic na sio hizi one way,A'fu pia si Bongo tu bali hata hizi nchi jirani mambo ni hayo hayo tu ya one way.nani kashasafiri toka Tanga hadi Dar?Ile Bararbar is an accident waiting to happenall through.Ile briji ya pale mto Wami mnaionaje?Ama tunasubiri mpaka ajali ya kukata na shoka itokee?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom