Mliokuwa mnauliza kazi ya Rostam Aziz kwenye ziara ya Rais Samia ya Marekani, hili ndio jibu lenu!

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Intelejensia ya Dunia katika karne ya 21 imebadilika sana! Nchi nyingi duniani sasa zinafanya kazi kutengeneza nguvu na ushawishi kwenye uchumi!

Kupata nguvu na ushawishi kwenye Uchumi kunahusisha kutengeneza matajiri wakubwa wenye pesa wanaoweza kuwekeza, kushawishi uwekezaji, kuongeza ajira na mapato ya nchi kupitia ushawishi kwenye uwekezaji

Ukienda Misri kuna Nasser Sawaris anaemiliki viwanda vingi vya cement na shareholder wa kampuni kubwa zaidi ya vifaa vya michezo ulaya Adidas

Ukienda Afrika kusini Kuna Patrice Motsepe
anaemiliki shares nyingi kwenye makampuni mbalimbali ya madini

Ukienda Nigeria kuna Aliko Dangote mwekezaji mkubwa kwenye uzalishaji wa cement , Sukari na mafuta na sasa anatengeneza refinery ya kwanza ya mafuta katika Bara la Africa

Tanzania tunae Rostam Aziz mmiliki wa kampuni ya Caspian, Taifa Gas, Tigo na Zantel! Huyu kuaminika kwake kunafanya kuwa mtu ambae Tanzania tunamtegemea sana kwenye kishawishi uwekezaji mkubwa unaotengeneza fursa za ajira na kukuza mapato na Uchumi wa nchi yetu

Urusi wanao wengi akiwemo Roman Abramovich aliyekuwa mmiliki wa club ya Chelsea

Marekani ndo usiseme wanao wengi na wanazidi kuzalisha wengi kila siku kama Jeff bezoz, Bill Gates, Warren Buffet, Elon Musk na wengineo wengi

Mfano wa kazi nzuri za Rostam Aziz kwa Tanzania ni huu! Katika ziara aliyoambatana na Rais Samia Marekani, ameweza kushawishi uwekezaji mkubwa katika kilimo hapa Tanzania kupitia Benki ya maendeleo Afrika.

Hongera Rais Samia, naiona akili kubwa sana kwako inayoenda kuibadili haraka sana Tanzania kiuchumi


0A9CB2F5-59F9-4AE9-959B-B14012BD094F.jpeg
 
Kuwa na matajiri wengi kunachochea sana R&D na kuharakisha industrialization process.... vyuo vyetu vikuu vimechoka na think tanks zenyewe wanakimbilia reseach zinazowaridhisha wafadhili...

Tunatakiwa na Akina Elon Musk, Bill Gates, Mark Zuckerberg wa kwetu ili kuharakisha maendeleo...
 
Dalali mwenye asili ya Iran wakala wa CIA. Mmoja wa miliki wa CCM anaeiuza nchi yetu bila huruma kwa sisi wananchi.
Shida kubwa ni kwamba umepewa akili ya kimaskini!

Tupe ushahidi wa nchi kuuzwa? Imeuzwa kwa Nani kwa mkataba upi na shs ngapi?
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Kaiba nini na wapi?
Rostam Aziz ndiye aliyekuwa Archtect wa wizi wa fedha kule BoT enzi ya Mkapa wakati huo marehemu Daudi Balali akiwa Gavana. Alifanikisha mpango wake kwa kumuingia Rais Mkapa nakuwa karibu nae kwa kumtumia aliyekuwa Balozi Ruhinda . Amefanikiwa kumuingia Samia kwa kupitia Kikwete hivyo tutegemee ufisadi mkubwa!
Hela yote ya uchaguzi mkuu 2025 itaibwa Kutoka serikalini na kumpelekea ccm kupitia makampuni ya Rostam.
 
Back
Top Bottom