Ziara ya Kitaifa ya Rais Samia katika Jamhuri ya Indonesia tarehe 24-26 Januari 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
ZIARA YA KITAIFA YA RAIS SAMIA KATIKA JAMHURI YA INDONESIA TAREHE 24-26 JANUARI 2024

Taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba kuelezea ziara za Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nchi za Indonesia.

Snapinsta.app_419606311_7477187485633155_8307359584493371805_n_1080.jpg

Dkt. Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya Kitaifa nchini Indonesia kuanzia tarehe 24 – 26 Januari 2024, kufuatia mwaliko wa Joko Widodo, Rais wa Jamhuri ya Indonesia. Ziara hii ya Kitaifa inafuatia ziara ya Kitaifa ya Rais Joko Widodo aliyoifanya nchini mwezi Agosti 2023.

Ziara hii inalenga kukukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Indonesia kupitia sekta mbalimbali za biashara na uwekezaji, kilimo, nishati, madini, mifugo, uvuvi, uchumi wa buluu, elimu, utalii na ulinzi.

MAENEO YA USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA INDONESIA

Tanzania na Indonesia zina uhusiano wa muda mrefu na wa kihistoria ambao umetimiza miaka 60 tangu kuanzishwa mwaka 1964. Uhusiano huo uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Indonesia Mheshimiwa Sukarno.

Indonesia ilifungua Ubalozi wake nchini mwaka 1964 na kuwa miongoni mwa nchi za kwanza kabisa kufungua Ubalozi wake nchini miaka michache baada ya uhuru. Aidha, Tanzania ilifungua Ubalozi wake nchini Indonesia Agosti, 2022.

Maeneo ya ushirikiano kati ya Tanzania na Indonesia ni kama ifuatavyo:

Snapinsta.app_420411893_1674285966432356_5383330328428724369_n_1080.jpg

Kilimo
Tanzania na Indonesia zimekuwa zikishirikiana katika sekta ya kilimo, ambapo mwaka 1996 Indonesia ilianzisha Kituo cha Mafunzo ya Kilimo kwa Wakulima Vijijini (Farmers’ Agriculture and Rural Training Centre-FARTC) kilichopo Mikindo mkoani Morogoro. Kituo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo mbalimbali kwa wakulima yenye kuwaongezea kuhusu kilimo na kuwaongezea uzalishaji

Elimu
Aidha, Tanzania na Indonesia zinashirikiana katika sekta ya elimu ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazonufaika na nafasi za masomo zinazotolewa na Serikali ya Indonesia. Idadi ya nafasi hizo (scholaships) iliongezeka na kufikia 200 mwaka 2018 kutoka nafasi 106 kwa mwaka 2015.

Biashara na Uwekezaji
Katika biashara, Tanzania inauza nchini Indonesia bidhaa mbalimbali ikiwamo pamba, tumbaku, karanga, kakao, matunda, kahawa, chai, njugu mawe, mbegu za mafuta, bidhaa nyingine za kilimo kama mafuta ghafi na mafuta ya mawese, mashine za viwandani na vipuri vyake, sabuni, samani, garment, instant noodles, stationery, palm stearin na apparel.

Katika uwekezaji, tunajivunia kuwa Indonesia imewekeza nchini miradi mitano yenye thamani ya Shilingi Bilioni 6.5 katika sekta za kilimo, uzalishaji wa viwandani na ujenzi.

Takwimu.JPG

Matarajio ya ziara (Outcomes)
Ziara hii itaimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano wa nchi hizi mbili. Aidha, Wakati wa ziara hii tunatarajia Hati za Makubaliano zitasainiwa.

Ziara ya Rais Joko Widodo Nchini Tanzania: Rais Samia ampokea Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo - Ikulu, Dar, leo Agosti 22, 2023

Kujua safari nyingine soma Safari/Ziara za nje ya Nchi za Rais Samia Suluhu tangu awe Rais wa Tanzania 19 Machi, 2021
 
ZIARA YA KITAIFA YA RAIS SAMIA KATIKA JAMHURI YA INDONESIA TAREHE 24-26 JANUARI 2024

Taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba kuelezea ziara za Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nchi za Indonesia.

Dkt. Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya Kitaifa nchini Indonesia kuanzia tarehe 24 – 26 Januari 2024, kufuatia mwaliko wa Joko Widodo, Rais wa Jamhuri ya Indonesia. Ziara hii ya Kitaifa inafuatia ziara ya Kitaifa ya Rais Joko Widodo aliyoifanya nchini mwezi Agosti 2023.

Ziara hii inalenga kukukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Indonesia kupitia sekta mbalimbali za biashara na uwekezaji, kilimo, nishati, madini, mifugo, uvuvi, uchumi wa buluu, elimu, utalii na ulinzi.

MAENEO YA USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA INDONESIA

Tanzania na Indonesia zina uhusiano wa muda mrefu na wa kihistoria ambao umetimiza miaka 60 tangu kuanzishwa mwaka 1964. Uhusiano huo uliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Indonesia Mheshimiwa Sukarno.

Indonesia ilifungua Ubalozi wake nchini mwaka 1964 na kuwa miongoni mwa nchi za kwanza kabisa kufungua Ubalozi wake nchini miaka michache baada ya uhuru. Aidha, Tanzania ilifungua Ubalozi wake nchini Indonesia Agosti, 2022.

Maeneo ya ushirikiano kati ya Tanzania na Indonesia ni kama ifuatavyo:

Kilimo
Tanzania na Indonesia zimekuwa zikishirikiana katika sekta ya kilimo, ambapo mwaka 1996 Indonesia ilianzisha Kituo cha Mafunzo ya Kilimo kwa Wakulima Vijijini (Farmers’ Agriculture and Rural Training Centre-FARTC) kilichopo Mikindo mkoani Morogoro. Kituo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo mbalimbali kwa wakulima yenye kuwaongezea kuhusu kilimo na kuwaongezea uzalishaji

Elimu
Aidha, Tanzania na Indonesia zinashirikiana katika sekta ya elimu ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazonufaika na nafasi za masomo zinazotolewa na Serikali ya Indonesia. Idadi ya nafasi hizo (scholaships) iliongezeka na kufikia 200 mwaka 2018 kutoka nafasi 106 kwa mwaka 2015.

Biashara na Uwekezaji
Katika biashara, Tanzania inauza nchini Indonesia bidhaa mbalimbali ikiwamo pamba, tumbaku, karanga, kakao, matunda, kahawa, chai, njugu mawe, mbegu za mafuta, bidhaa nyingine za kilimo kama mafuta ghafi na mafuta ya mawese, mashine za viwandani na vipuri vyake, sabuni, samani, garment, instant noodles, stationery, palm stearin na apparel.

Katika uwekezaji, tunajivunia kuwa Indonesia imewekeza nchini miradi mitano yenye thamani ya Shilingi Bilioni 6.5 katika sekta za kilimo, uzalishaji wa viwandani na ujenzi.

View attachment 2879279

Matarajio ya ziara (Outcomes)
Ziara hii itaimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano wa nchi hizi mbili. Aidha, Wakati wa ziara hii tunatarajia Hati za Makubaliano zitasainiwa.

Ziara ya Rais Joko Widodo Nchini Tanzania: Rais Samia ampokea Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo - Ikulu, Dar, leo Agosti 22, 2023
Anaenda ziara anaiacha nchi inaongozwa na wakimbizi? Huyu mama sio mzima aisee!
 
Back
Top Bottom