Hii ndio sababu ya Rais Samia kuambatana na Rostam Azizi kwenye baadhi ya Ziara zake

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu Watanzania,

Nimekuwa nikishangaa sana kwa baadhi ya watanzania wenzangu kuhoji ama kushangaa kwanini ndugu Rostam Azizi anaonekana katika ziara nyingi za Mheshimiwa Rais nje ya nchi. Lakini pia ningependa kusema kuwa siyo Rostam Azizi pekee anayekuwa katika ziara za Mheshimiwa Rais wetu bali huwa wapo na wafanyabishara wengine ama wawakilishi wao.

Ikumbukwe na kufahamika ya kuwa Rostam Azizi ni mfanyabiashara mkubwa sana hapa barani Afrika na mwenye uzoefu mkubwa na wa muda mrefu sana katika masuala ya biashara na uwekezaji.ni mlipa kodi mkubwa na ni mtu aliyetoa ajira kwa vijana wengi kupitia biashara zake. ieleweke ya kuwa mahusiano ya nchi na nchi siyo kwa ajili ya kupiga stori za hapa na pale au kwa ajili ya kutembeleana tu na kunywa vinywaji na kupiga picha au kupeana zawadi za picha za wanyama.

Ziara za mkuu wa nchi na maongezi ya wakuu wa nchi na nchi ni ziara za kutafuta fursa,kujenga mahusiano mazuri ya kuchochea fursa mbalimbali za kibiashara,kiuchumi na kiuwekezaji.ni ziara za kutafuta namna ya kuipatia nchi yako faida katika sekta mbalimbali,ni ziara za kuhakikisha unapata wawekezaji,watalii, wafanyabiashara wakubwa, wataalamu katika masuala mbalimbali,uzoefu wa vitu mbalimbali na mambo mengine mbalimbali.

Ifahamike ya kuwa nguvu ya nchi ipo katika ukubwa wa uchumi wake na siyo katika ukubwa wa eneo lake au wingi wake wa watu. kuwa na rasilimali pekee yake bila kujuwa namna ya kuzitumia bado huwezi kuwa tajiri. Ili uwe mwenye nguvu ni lazima uwe na nguvu ya kiuchumi itakayo kuwezesha kufanya mambo mbalimbali.ukiwa na nguvu ya uchumi utakuwa na sauti,uhuru,amani,furaha,maamuzi na hata kujipangia mambo yako mwenyewe.

Kwa hiyo unapokwenda nje ya nchi unakojuwa unakwenda kujadili na kutafuta fursa za masuala ya biashara, uchumi na uwekezaji ni lazima uende na kuambatana na watu wenye uzoefu wa mambo hayo,ni lazima uwe na watu wenye akili kubwa ,wenye kujuwa namna ya kucheza na lugha ,wenye kujuwa namna ya kuzisaka na kuzimulika fursa kuzileta nchini,wenye kujuwa namna ya kujenga na kushawishi mamlaka za nchi husika,wenye akili na upeo wa hali ya juu,wenye kuishi mbele ya wakati ,wenye kuona fursa kwa jicho la tatu ,wenye kuvuta fursa kama sumaku na wenye kuwa na shabaha kwa kila eneo wafikalo kuwa walenge kupata nini na kurudi na nini.

Huendi na kuambatana na watu wanaokwenda kuzurura tu na kushangaa magorofa au kufanya shopping au kujirusha mitandaoni au kwenda kujifunza kwa kila kitu na kufundishwa kila kitu. Ni lazima uende na watu wenye uzani mkubwa na wenye kukaa mezani na watu wa aina yoyote ile katika mazungumzo ya kibiashara na wakatoka ngoma droo bila kuonyesha unyonge katika majadiliano. Ni lazima kama Rais wa nchi uhakikishe kuwa pamoja na kuvutia uwekezaji na wawekezaji lakini ni lazima watu wako wahusike katika uwekezaji huo ,ni lazima uhakikishe uchumi wa Taifa lako angalau unakuwa mikononi mwa watu wako wenyewe.ni lazima ujuwe kama ni ma miradi makubwa basi na watu wako nao wanakuwa washirika ili pesa zingine zibaki hapa nchini na kuingia katika mzunguko mitaani pale utakapokuwa unafanya malipo.

Ni hatari sana kuweka uchumi wako katika mikono ya wageni pekee yao ,maana siku wakiamua kuondoka na kufungasha virago vyao na kwenda na madolari yao kwao utabaki ulie na kusaga meno ,maana watakomba hazina yao yote kwenye mabenki,watafunga na kupunguza ajira na hivyo kupunguza kodi ambayo ilikuwa inalipwa na wafanyakazi,watapunguza mzunguko wa pesa mitaani,watasababisha kuadimika kwa dola ya mmarekani mitaani na hivyo kupunguza uwezo wako wa kuagiza bidhaa kutoka nje n.k. ni lazima watakutikisa kiuchumi na kukudhoofisha.

Hivyo ili kuepuka haya kutokea ndio maana viongozi wenye akili kubwa na wenye kuona miaka mia mbele kama Rais Samia wanaweka mikakati ya kuhakikisha kuwa uchumi wetu unakuwa mikononi mwa Watanzania Wenyewe ,lakini pia kuhakikisha kuwa fursa zinazopatikana mahali popote pale Duniani basi zinanaswa katika rada ya Tanzania. na hapa hadi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama hususani idara yetu ya usalama wa Taifa lazima ihusike katika kunusa fursa na kuwaunganisha watu wetu ili wazipate kwa uharaka na wepesi.

Hapo sasa ndio inapokuja umuhimu wa watu kama akina Rostam Azizi kuwepo katika ziara za Mheshimiwa Rais pamoja na wafanyabishara wengine wengi wakitanzania ,katika kuhakikisha kuwa tunapata fursa za kibiashara ,masoko ya bidhaa zetu nje ya nchi n.k. tuelewe ya kuwa tupo katika Dunia ya ushindani ambapo kila mtu anapambana kupata fursa kwa ajili ya Taifa lake.kwa hiyo ukibweteka tu kwako basi utaishia kuwa msindikizaji. ukikosa kuwa na mipango basi utaishia kupangiwa kila kitu na kuongozwa kwa kila kitu. Ni lazima uwe na jicho la mbali na kali sana la kupenya popote pale. Ni lazima uwe na akili na shabaha ya kujuwa mahali fulani nataka nikapate kitu fulani ili kuondoa changamoto fulani nchini mwangu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
IMG-20240116-WA0009.jpg
IMG-20240208-WA0009.jpg
IMG-20240125-WA0013.jpg
IMG-20240208-WA0006.jpg
 
M

0742-676627.View attachment 2904739View attachment 2904740View attachment 2904741View attachment 2904742
Sema kwamba CCM na serikali ya CCM ni mateka wa FiSaDi badala ya kuleta blahblah zako hizo.
 
Back
Top Bottom