Mwawado
JF-Expert Member
- Nov 2, 2006
- 993
- 252
Hii tabia ya "UMUNGU MTU" ndio kitu kinachoniudhi kwa viongozi wetu,ni lazima sasa Utawala wa sheria uchukue nafasi yake,haiwezekani kutoa maisha ya mtu kwa sababu ya kuharibu taa ya gari (prado) ambayo hata haizidi Tshs 30,000.Nimekwishasikia habari za watu kuua na baadaye unawaona kwenye mabaa na mabarabarani wakiwa huru,ati kwa sababu tu wana influence na watu waliopo madarakani!!Sasa hapa sheria ikipindwa tutapigana mawe,kama silaha wanapewa wenye uwezo tu!!Hainiingii akilini kuona mtu anatumia silaha kwenye mgogoro ambao unaweza kutatuliwa kwa mjadala.Hiyo ni kashfa na inabidi "AJIUZULU" Nyadhifa zote hata kama nae ni Mwanamtandao.Ni lazima sasa tujali Utawala wa Sheria,na sio kujiamulia mambo kama Gang Groups!!.