Mkuu wa Mkoa azuia wananchi kuchukua mchanga kwenye kaburi la Maalim Seif, asema wataumaliza na kuacha shimo

Embu mnaokaa kwenye mambo mengi kuna hili linalotokea sasa Pemba sehemu alipozikwa Al marhoum Maalim Seif Sharif Hamad,inasemekana watu wanakwenda kuchota mchanga wa kaburini na sasa polisi wanalinda lakini hata hivyo bado watu wanavizia na kuuchukua japo kwenye mfuko wa shati.

Clip inayozagaa inamuonyesha mkuu wa Polisi Pemba akionya kuna hatari watu wakamaliza mchanga na kumfukua maiti na kugawana mifupa.ametoa onyo kali.
 
Waliochukua mchanga wanasema kweli unanukia na ndio sasa kila mtu aliethibitisha anakwenda kupata japo punje,sasa itakuwa dili wale walinzi wanaweza kutajirika,yaani ukitoa chai wanakuachia uchote.
 
Wangewaruhusu kwa shart wawe wanarudishia mchanga mwingine wa kubadilishana na huo.
 
Tunawaomba wanasiasa wengine waige mfano wa Hayati Maalim Seif angalia watu wanavyompenda

Nina imani kuna baadhi ya Mwanasiasa wako hai siku wakivuta kuna baadhi ya Wananchi wanaweza kunywa na kufurahia.

Hii Dunia ni mapito tu
Kmmmke!! sijui zitanyweka haswa
 
Back
Top Bottom