Maalim Seif hakuacha wosia kuhusu mrithi wake

Jamhuri ya Zanzibar

Senior Member
Jul 17, 2012
126
195
Katika muktadha wa historia ya Zanzibar kuna wanaoamini kuwa hata Marehemu Mzee Karume mwenyewe alijutia yale maamuzi yake ya kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na ukweli kwamba mambo yalikwenda kinyume na matarajio yake. Viongozi wakubwa wa serikali ya Zanzibar wa wakati huo, akiwemo Marehemu Mzee Aboud Jumbe, waliliweka bayana suala hili.

Wako wanaoamini kwamba kulingana na mazingira ya kimahusiano yalivyokuwa baina ya Mzee Karume na Hayati Baba wa Taifa, Mzee Kambarage katika kipindi cha mwisho cha uhai wa Mzee Karume, pengine leo kitu kinachoitwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kisingekuwepo tena. Mzee Karume alitamka kila mara “nchi hii ni ya Wazanizbri”, “Nchi hii ni yetu wenyewe”. “Tumeingia katika Muungano kwa hiari zetu kwa kuguswa na hisia za umoja wa Afrika”. Alisisitiza pia kuwa “tukigeukwa katika Muungano huu tutajitoa”.

Ukiweka pembeni vuta n’kuvute za siasa za ubaguzi na kimapinduzi za miaka ya 1950 na 60 zilizopelekea wazee wa kizanzibari kutofautiana, kuumizana na kuuwana, Mzee Karume kwa upande wake aliipenda sana Zanzibar na hakuwa tayari kuiuza kwa thamani yoyote. Aiuonesha msimamo wake huu hata wakati Zanzibar imeshaungana na Tanganyika na Nyerere akiwa hai. Hata hivyo mara tu baada ya kifo chake, warithi wake walimgeuka. Walighilibika na kuiuza Zanzibar kwa Nyerere jambo lililopelekea kupotea kabisa Zanzibar katika ramani ya ulimwengu. Umaarufu wake, heshima yake, utengamano wake, mvuto wake, neema zake na nguvu yake kama nchi kongwe sana katika Bara la Afrika vimebaki ni historia.

Wana ASP walimsaiti Mzee Karume. Wana CCM wa upande wa Zanzibar pia wa zama hizi wanaendeea kumsaliti Mzee Karume kwa nib ado wanaendelea kukiuza kipande cha Zanzibar kilichobaki bila kujali. Wakati Mzee Karume hakua tayari kupoteza mamlaka zaidi ya Zanzibar, baada ya kile alichokifanya 1964, waliomrithi wamekuwa tayari kuyatoa malka yote ya Zanzibar kwa thamani ndogo ya vyeo na ulwa na kuibakisha Zanzibar kama Municipality. Zanzibar imepotea na kuwa koloni la Tanganyika sawa tu na yalivyokuwa makoloni mengine katika zama za ukoloni.

Laana ya Mzee Karume imeipiga Zanzibar imepigika. Hakuna kilichobakia Zanzibar zaidi ya jina na ardhi isiyomvutia wa ndani wala wa nje. Kisiasa na kisheria, Zanzibar haina mamlaka ya kuanzisha jambo lolote lenye maslahi na Wazanzibar. Haiwezi hata kuanzisha bandari huru na ukanda huru wa kiuchumi kwa maslahi ya watu wake. Zanzibar imetiwa pingu na kukomelewa gerezani kama mfungwa. Inasubiri amri, maagizo na makemeo kutoka Tanganyika. Kiuchumi, kila mmoja analia njaa, si CCM, si ACT. Si mwenye kazi wala asie na kazi. Ukifanikiwa kuipata tonge ya siku moja na dagaa la kukausha umshukuru Mungu.

Hii ndio laana ya Mzee Karume ambayo inaendelea kuwala Wazanzibari wote hadi leo. Usaliti wa ASP na CCM dhidi ya uzalendo wake, mapenzi yake na dhamira yake kwa Zanzibar vimewagharimu. Baada ya hilo Wazanzbari wanaonekana bado hawajajifunza. Sasa ACT-Wazalendo nao ambao wameaminiwa na Wazanzibari kuwa ndio harakati na Chama mbadala cha kuwapigania tokea kuuwawa kwa Mzee Karume. Chama alichokuwemo Marehemu Maalim Seif hadi umauti unamfika, kinachopigania kurejeshwa kwa hadhi na heshima ya Zanzibar. Viongozi wa ACT-Wazaendo wanataka kurejea makosa ya ASP. Wao wanataka kumsaliti Maalim Seif na kuizisaliti legacy zake kwa maslahi ya vikundi na watu binafsi ndani ya Chama.

Maalim Seif Sharif Hamad kwa wanaomjua vyema hakuwahi kuwa muumini wa kurithisha madaraka, wala itikadi yenyewe ya kurithisha madaraka hakuwahi kuikubali. Anaezungumza kinyume na hivi huyo pengine hamjui Maalim Seif au anamzulia uongo kwa makusudi. Nilikuwa nikipata fursa ya kumsalimia Maalim Seif kila anapofanya ziara kisiwani Pemba katika Wilaya ya Wete. Ninapopata tu utulivu wa kukaa nae basi huwa siachi kumuuliza chochote. Bahati njema Maalim nae hakuwa na kiburi au dharau au kuchoshwa na maswali yangu. Kila nilichomuuliza alinijibu kwa uchangamfu.

Siku moja nilimuuliza Maalim Seif, wakati huo bado akiwa Katibu Mkuu wa CUF; “hivi nyinyi CUF kama chama imara sana cha kushika hatamu za Dola mnayo succession plan?” (Yaami mpango na mkakati wa kuandaa viongozi warithi). Nilimuuliza tena; “kwanini msiandae viongozi kimkakati kama wanavyofanya wenzenu CCM? CCM wao anapomaliza Rais muda wake huwa inafahamika ni akina nani watachukua nafasi.” Niliendelea kumuuliza, Maalim na wewe ni binadamu ipo siku Allah atakuhitaji, umeshaandaa mpango wa nani watakuwa warithi wako?”

Nilishangazwa sana na jawabu ya Maalim Seif. Alinijibu kitu ambacho mimi muulizaji sikuwa nikielewa. Aliniambia; “sisi CUF hatuna utaratibu wa succession. Hatuandai warithi kwa namna yoyote. Hatusogezi watu mbele kimkakati ili wawe warithi wa uongozi wala sisi viongozi hatuamui nani awe kiongozi baada yetu.” Maalim aliendelea kuniambia; “ni hatari kubwa kufanya hivyo”. “Ni kuwatengenezea wenzenu vifo”. “Siasa ina wema na waovu”. “Wako ambao hawatatamani huyo anaeandaliwa awe kiongozi”. “Pengine hao wasiotamani Fulani awe kiongozi anaeandaliwa ni watu wenye nguvu na mamlaka. wakimjua tu wataamuua”. “Hapana hapana, sisi hatuko tayari kuwa na utaratibu wa succession plan”.

Tukio hili liltokea tukiwa tunaongea faraghani. Lakini Maalim Seif hakuonesha msimamo wake huu kuhusi succession faraghani pekee. Pia aliwahi kuweka msimamo wake huu hadharani alihojiwa na kituo cha televisheni cha AZM TV kule Dar es Salaam. Mtangazaji alimuuliza takriban sawa na nilivyomuuliza mimi. Jawabu ya Maalim Seif pia aliyompa mtangazaji haikutofautiana na yangu. Teknolojia ni shahidi wa kisasa. Ukisema uongo uogope teknolojia. Mahojiano haya baina ya Maalim Seif na kituo cha utangazaji cha AZAM TV yapo mitandanoni hadi leo.

Nilitosheka na jawabu ya Maalim Seif. Kuanzia siku hiyo nilianza kuamini kuwa kuandaa viongozi warithi sio utaratibu mzuri hasa kwa Bara la Afrika, Bara la wasioshiba madaraka na uongozi. Pia sikutegemea tena kama Maalim yeye mwenyewe angeteua mrithi wake. Halkadhalika sikutegemea kuwa baada ya kifo cha Maalim Seif atatokea mtu yoyote aseme Maalim Seif ameteua mrithi wake. Lakini jambo lililonishangaza sana ni mara tu baada ya Maalim kufukiwa na nusu tani ya kifusi pae Nyali Mtambwe, waandamizi wake wameanza kumzulia uongo. Wameanza kuivunja legacy yake kwa manufaa yao binafsi. Maalim ambae alikuwa haamini katika suala la kuweka mrithi tena akiwa na sababu na falsafa muhimu kwa msimamo wake huo eti leo anasimama mtu anasema tofauti.

maalim ikulu.jpg

Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad alipokula kiapo kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa mara ya pili, Ikulu Zanzibar​

ACT-Wazalendo msichokoze laana na radhi za Maalim Seif. Mzee huyu ameyatoa kafara masiaha yake yote kwa ajili ya Zanzibar na watu wake. Tusitumie jina lake vibaya itatugharimu. Tusimzulie uongo ili kutimiza ndoto na malengo yetu binafsi ya kisiasa. Nilipowasikia baadhi ya viongozi wanasisitiza kuwa Maalim kabla hajafariki aliwacha wasia wa jina la mrithi wake hata sikushtuka sana, nilitabasamu na nikajiambia moyoni kuwa zama za Maalim zimeisha sasa wacha tupelekwe tunapopelekwa. Nilishangaa kuisikia kauli hiyo ikitoka katika kinywa cha Mama yetu, Mjane wa Maalim Seif, Mama Awena Sanani. Nikajiuliza Mama huyu madhubuti alievumilia mikiki mingi katika maisha yote aliyoishi na Maalim Seif anawezaje kukubali kulishwa maneno ya fitna na yaliyo kinyume na legacy ya mumewe anayoifahamu? Tuwache hapo.

Viongozi hufa wao tu lakini legacy zao hubaki, ziwe mbaya au nzuri. Hazihitaji kuchongwa upya, kupakwa rangi wala kurekebishwa. Kumbukumbu, itikadi, falsafa, imani na misimamo ya Maalim Seif isibadilishwe bali iwachwe kama ilivyo ili kizazi na kizazi itumie kama somo na historia kujifunza. Tusibadili chochote kinachohusiana na Maaim Seif kwa faida zetu binafsi za kisiasa.
 
Zungumzia kidogo wakati Maalim alipomshtaki Aboud Jumbe kwa Mwalimu Nyerere kuwa anataka kuvunja muungano
Kutokuwa na succession plan kumepelekea kuwa na kiongozi asiyekuwa hata na nusu ya haiba na mvuto wake na chama sasa kipo kipo tuu.
 
Maalim Seif Sharif Hamad kwa wanaomjua vyema hakuwahi kuwa muumini wa kurithisha madaraka
Na bila kupepesa macho hii ni shida sio tu ACT ila vyama vyote vya upinzani hata sisi Chadema. Kwa mfano sipendi hii tabia mtu ni mbunge hapo hapo ni mwenyekiti wa Kanda ama mwenyekiti wa mkoa wa chama, Sasa unategemea wengine wataongoza Nini?

Ni vizuri tuwe na utaratibu wa kuachiwa wengine space ya kuonyesha uwezo kuliko kuhodhi madaraka yote. Ukiwa mbunge Baki bungeni, ukiwa mwenyekiti wa chama mkoa Baki kwenye chama otherwise madhara yake ndio kama haya ya ACT ameondoka Seif na chama kinafubaa.

Pia nitoe rai kwa Mbowe, amefanya makubwa na hakuna kiongozi wa upinzani Tanzania amewahi fikia mafanikio yake ila it's time Sasa aandae successor otherwise siku akifariki ghafla itatokea power struggle kubwa mnoo ambayo inaweza kipasua chama pasu kwa pasu.
 
Hiyo succession plan kwa vyama vyote hakuna na nakubaliana na Maalim Seif kuwa ni kumtengenezea mtawala mtarajiwa mizengwe ya kutolewa roho yake mapema, aidha kwa bunduki au kwa ndumba.

Tuangalie CCM: Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, JPM... kuna aliyepata uraisi hapo kwa kuwa alitayarishwa kabla? Kila mmoja ameupata kivyake vyake.

Ukisoma historia utakuta enzi za utawala wa ufalme duniani, ilikuwa ni kizaa zaa kuweka mtawala mtarajiwa hata kwa ndugu wa damu kabisa. Akichaguliwa mmoja basi wengine ni uhasama na kuuwana au kuwekeana sumu.

Achaguliwe mtu kwa mujibu wa uwezo wake baada ya kushindanishwa na wengine. Kila mtawala anakuja na mambo yake wala hayatabiriki.
 
Back
Top Bottom