Mkuu wa Mkoa azuia wananchi kuchukua mchanga kwenye kaburi la Maalim Seif, asema wataumaliza na kuacha shimo

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
14,093
2,000
Wajuzi watuambie hili la mchanga lina maana gani😥😥😥😥😥

Aendelee kulala salama Maalim Seif Sharif Hamad
===

Katika hali ya kustaajabisha inadaiwa kumeibuka watu ambao wanachukua mchanga katika kaburi la Hayati Maalim Seif. Baadhi ya wakazi wameeleza kuwa mchanga huo unachukuliwa kwa imani tofauti tofauti. Aidha wapo wanaodai kuwa mchanga huo unanukia harufu ya Miski.

Katika kufafanua zaidi tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Bi Salama Mbarouk Khatibu amewaonya watu wanaochukua mchanga huo. Katika hili amesema Watu wanachukua mchanga waendelee kuzuiwa kwa sababu hatujui wanapochukua mchanga huo wanaenda kuufanyia nini.

Naye, RPC wa Kaskazini Pemba Juma Sadi Khamis ameonya kwamba watu wanaokuja kufanya dua wanaruhusiwa isipokuwa hawatakiwi kuchukua mchanga huo. Amesisitiza kuwa mtu akifanya hivyo itakuwa ni kosa.

Pia soma > TANZIA - Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad afariki dunia
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,797
2,000
Mkuu wa Mkoa huko Pemba alikozikwa aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif amepiga marufuku wananchi kwenda kuchukua mchanga kwenye kaburi la Seif kwa imani za kinabii.

Mkuu wa Mkoa amesema mamia ya wananchi kila siku huenda kaburini hapo kuchukua mchanga na hivyo kuhatarisha usalama wa kaburi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,090
2,000
Mkuu wa mkoa huko Pemba alikozikwa aliyekuwa mwenyekiti wa ACT wazalendo maalim Seif amepiga marufuku wananchi kwenda kuchukua mchanga kwenye kaburi la rip maalim Seif kwa imani za kinabii.

Mkuu wa mkoa amesema mamia ya wananchi kila siku huenda kaburini hapo kuchukua mchanga na hivyo kuhatarisha usalama wa kaburi.

Maendeleo hayana vyama!
Duuhh . Haya mapenzi haya !!
 
Dumas the terrible

JF-Expert Member
Jan 20, 2021
1,762
2,000
Aisee sie wa bara ndo twasikia leo ya kwamba Maalim Seif alikua nabii wa Pemba yakhe basi Inshaalah
Mwenyezi Mungu amrehemu mja wake amwepushie adhabu ya kaburi aamin!
 
All TRUTH

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
4,908
2,000
Mkuu wa Mkoa huko Pemba alikozikwa aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif amepiga marufuku wananchi kwenda kuchukua mchanga kwenye kaburi la Seif kwa imani za kinabii.

Mkuu wa Mkoa amesema mamia ya wananchi kila siku huenda kaburini hapo kuchukua mchanga na hivyo kuhatarisha usalama wa kaburi.

Maendeleo hayana vyama!
Duh suala la IMANI Ni gumu
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
4,248
2,000
Mkuu wa Mkoa huko Pemba alikozikwa aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif amepiga marufuku wananchi kwenda kuchukua mchanga kwenye kaburi la Seif kwa imani za kinabii.

Mkuu wa Mkoa amesema mamia ya wananchi kila siku huenda kaburini hapo kuchukua mchanga na hivyo kuhatarisha usalama wa kaburi.

Maendeleo hayana vyama!
Hilo kaburi lijengwe na liwekwe tiles.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom