Polisi kuwakamata wamiliki wanaoingiza magari mabovu barabarani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema kuwa litawakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto wanatumia kigezo cha mwisho wa mwaka kuingiza vyombo vyao ambavyo vinachangamoto za kiufundi na kutumia kigezo cha mwisho wa mwaka kusafirisha abiria maeneo mbalimbali hapa nchini.

Hayo yamesemwa mapema Disemba 03,2023 na Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi Jirani huku akibanisha kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wamiliki kutumia kigezo cha wingi wa abiria na mwisho wa mwaka kuingiza magari mabovu barabarani.

SSP Zauda ameongeza kuwa Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha usalama Barabarani Mkoani humo hakitowafumbia macho wamiliki watakao bainika kuingiza magari mabovu barabarani huku akisema kikosi hicho kitaendelea kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto mara kwa mara na kutoa elimu kwa madereva na abiria wanaotumia vyombo hivyo.

Aidha amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kumaliza kabisa ajali ambazo zimekuwa zikisababisha ulemavu na kuwaacha wananchi wakiwa na ulemavu wakudumu ambapo amewataka madereva ambao wamekuwa wakiendesha umbali mfupi kuwatumia madereva wazoefu kuwaendesha kama wanakwenda safari ndefu.
d42d69cf-7569-4f12-97da-cdd55246a869.jpeg

Sambamba na hilo ametoa wito kwa wazazi wanatumia kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kuwasafirisha watoto wadogo Kwenda kuwasalimia ndugu na jamaa maeneo tofauti tofauti kuhakikisha watoto hao wanakuwa na uangalizi wa karibu ili kupunguza vitendo vya kupotea kwa Watoto kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Kwa upande wake Mchungaji Getruda Kyando ambaye anatumia usafiri wa mabasi yanayokwenda maeneo tofauti tofauti hapa nchini Pamoja na kuwaomba Jeshi hilo kufanya kaguzi za mara kwa mara amekipongeza kikosi hicho kwa kutoa elimu na mawasiliano ya moja kwa moja kwa abiria ambayo yatasaidia kutoa taarifa kwa wakati pindi madereva wanapokiuka sheria za usalama Barabarani.
44b11154-b01a-4fe3-89a0-2699fe85a179.jpg

8d854b7e-0fca-44b1-94f6-d46860f81a0b.jpg

Nao baadhi ya madereva wanaofanya safari zao ndani na nje ya nchi wamesema kumekuwepo na ongezeko la magari kipindi hiki cha mwisho wa mwaka huku wakiwataka madereva wenzao wasiofuata sheria za usalama barabarani kuhakikisha wanafuta sheria hizo ili kupunguza ajali hapa nchini.
 
Wafanye kweli, uchafu wote utoke barabarani. Hayo magari mabovu wayapeleke mashambani kugeuzwa kuwa zana kulimia, kupukusua nafaka na kuvunia. Wasisahau na zile pikipiki za kihuni zinazopigia watu kwa kutoa mlio mbaya wa kelele
 
View attachment 2832031
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema kuwa litawakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto wanatumia kigezo cha mwisho wa mwaka kuingiza vyombo vyao ambavyo vinachangamoto za kiufundi na kutumia kigezo cha mwisho wa mwaka kusafirisha abiria maeneo mbalimbali hapa nchini.

Hayo yamesemwa mapema Disemba 03,2023 na Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani na nchi Jirani huku akibanisha kuwa kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wamiliki kutumia kigezo cha wingi wa abiria na mwisho wa mwaka kuingiza magari mabovu barabarani.

SSP Zauda ameongeza kuwa Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha usalama Barabarani Mkoani humo hakitowafumbia macho wamiliki watakao bainika kuingiza magari mabovu barabarani huku akisema kikosi hicho kitaendelea kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto mara kwa mara na kutoa elimu kwa madereva na abiria wanaotumia vyombo hivyo.

Aidha amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kumaliza kabisa ajali ambazo zimekuwa zikisababisha ulemavu na kuwaacha wananchi wakiwa na ulemavu wakudumu ambapo amewataka madereva ambao wamekuwa wakiendesha umbali mfupi kuwatumia madereva wazoefu kuwaendesha kama wanakwenda safari ndefu.
View attachment 2832027
Sambamba na hilo ametoa wito kwa wazazi wanatumia kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kuwasafirisha watoto wadogo Kwenda kuwasalimia ndugu na jamaa maeneo tofauti tofauti kuhakikisha watoto hao wanakuwa na uangalizi wa karibu ili kupunguza vitendo vya kupotea kwa Watoto kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Kwa upande wake Mchungaji Getruda Kyando ambaye anatumia usafiri wa mabasi yanayokwenda maeneo tofauti tofauti hapa nchini Pamoja na kuwaomba Jeshi hilo kufanya kaguzi za mara kwa mara amekipongeza kikosi hicho kwa kutoa elimu na mawasiliano ya moja kwa moja kwa abiria ambayo yatasaidia kutoa taarifa kwa wakati pindi madereva wanapokiuka sheria za usalama Barabarani.
View attachment 2832029
View attachment 2832030
Nao baadhi ya madereva wanaofanya safari zao ndani na nje ya nchi wamesema kumekuwepo na ongezeko la magari kipindi hiki cha mwisho wa mwaka huku wakiwataka madereva wenzao wasiofuata sheria za usalama barabarani kuhakikisha wanafuta sheria hizo ili kupunguza ajali hapa nchini.

Inasubiriwa kwa hamu serikali ya wananchi isiyoendekeza rushwa uchwara, itakayopiga chini majukumu haya yasiyo na tija yoyote kutokea polisi.

Tangu lini polisi wakawa na weledi wa kukagua magari? Ajali ya Manyoni au ipi ingezuiliwa na ukaguzi uchwara huu?
 
Back
Top Bottom