Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,187
- 671
mkuu mwanakijiji na wenzio kama mna sifa zilizotajwa jitupeni kuomba hio nafasi.
ili tuone huo uzalendo wenu vipi unaweza kusaidia kuleta changamotoza maendeleo tanzania.
Katika hatua nyingine, mwandishi wetu Grace Michael anaripoti kuwa Ikulu ya Dar es Salaam imetangaza nafasi mbalimbali za kazi zikiwemo nafasi nne za wanahabari ambao watafanyakazi mbalimbali katika ofisi hiyo.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Ikulu jana kwa vyombo mbalimbali vya habari na ambalo tumelichapisha katika ukurasa wa 24 na 25 wa gazeti hili, nafasi za wanahabari ni ile ya Ofisa Habari Mwandamizi ambazo ni nafasi mbili pamoja na Ofisa Habari Mkuu II nafasi mbili.
Kwa mujibu wa tangazo hilo waombaji katika nafasi ya Ofisa Habari Mwandamizi watatakiwa kuwa na umri usiozidi miaka 40 na raia wa Tanzania, wawe na shahada ya kwanza au stashahada ya juu ya uandishi wa Habari au sifa inayolingana nayo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali pamoja na uzoefu wa kazi kwa muda wa miaka mitano.
Kwa mujibu wa nafasi hii kazi zinazotakiwa kufanywa na wahusika endapo watapata nafasi hizi ni pamoja na kutoa ushauri katika masuala ya habari, kuendesha tafiti katika masuala ya habari na kazi zinginezo.
Katika nafasi ya Ofisa Habari Mkuu II waombaji wanatakiwa kwanza kuwa watumishi wa Serikali, awe raia wa Tanzania na umri usiozidi miaka 40, shahada ya uzamili ya uandishi wa habari pamoja na uzoefu usiopungua miaka saba.
Tangu alipoingia madarakani Desemba, 2004 Rais Kikwete aliahidi na hatimaye baadaye akatekeleza uundaji mpya wa idara ya mawasiliano kwa kuanzisha Kurugenzi ambayo inaongozwa na mwandishi wa habari veterani Salva Rweyemamu.
source: http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=6383