Mhasibu Hospitali ya Mt. Walburga Nyangao Januari, 2024

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
4,720
1,479
TANGAZO LA KAZI-LINARUDIWA

Hospitali ya Mt. Walburga Nyangao iliyoko Jimbo Katoliki la Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Mtama-Lindi inatangaza nafasi ya kazi kama ifuatavyo;

Nafasi: Mhasibu II - Nafasi 1

SIFA
- Wenye Shahada ya Uhasibu inayotolewa na Chuo/Taasisi ya Uhasibu inayotambulika na serikali

- Wenye cheti cha taaluma ya Uhasibu CPA (T) au sifa inayolingana nayo inayotambulika na NBAA

Kazi na Majukumu
1. Kuidhinisha hati za malipo
2. Kuandika taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi
3. Kusimamua wahasibu wasaidizi katika kazi zao za kila siku
4. Kusimamia shughuli za uhasibu kwenye kitengo cha idara
5. Kutayarisha na kurekebisha payroll pamoja na dasheets
6. Kujibu hoja za ukaguzi
7. Kusimamaia matumizi sahihi ya vifungu vyote vya fedha
8. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake

Sifa za Ujumla
  • Waombaji wawe ni raia wa Tanzania
  • Wawe na umri wa miaka 25-45
  • Waombaji waambatanishe cheti cha kuzaliwa
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi (CV) na picha ndogo za karibuni (passport size)
  • Waombaji wenye uzoefu waonyeshe taarifa za taasisi walizofanyia kazi pamoja na waajiri wao
  • Maoni yote yaambatanishwe na vyeti vya taaluma, vyeti vya sekondari na Baraza

Namna ya Kuomba
Waombaji waandike maombi yao kupitia anwani ifuatayo;

MGANGA MFAWIDHI,
HOSPITALI YA MT. WALBURGA NYANGAO,
S.L.P 1002,
NYANGAO, LINDI.

Maombi yanaweza wasilishwa kwa mkono kwa kuleta moja kwa moja au kupitia barua pepe; nyangaohospital@gmail.com

Mwisho wakupokea maombi ni tarehe 31/01/2024
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom