Watu 8,476 kusaka nafasi 42 za ajira zilizotangazwa na Bunge

Covax

JF-Expert Member
Feb 15, 2021
6,276
21,453
Hii habari iko kwenye gazati la Nipashe, kama ni kweli hiyo hali anatupa taswira gani katika soko la ajira? Hi ni timing bomb, kuna haja ya vyuo kubadili mitaala ya kozi zisizokuwa na soko kwenye market yetu.

======
Tume ya Utumishi ya Bunge imetangaza ajira za kada mbalimbali ambapo walioitwa kwenye usaili wako zaidi ya 8,000 kati ya nafasi za kazi 42 zilizotangazwa, huku kada zinazoongoza kwa idadi kubwa ni uchumi, udereva, sheria na uhasibu.

Kwa mujibu wa tangazo la kuitwa kwenye usaili lililotolewa Mei 19, mwaka huu na Katibu wa Bunge jijini Dodoma, liliorodhesha jumla ya majina 8,476 ya waliovuka hatua va kwanza ya mchujo na kuitwa kwenye usaili kwa kada 21 za ajira kwenye Bunge la Muungano wa Tanzania.

April 21, mwaka huu Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitangaza nafasi za kazi 42 katika kada 21 mbalimbali ili kuim arisha utendaji wake.

Juzi, Bunge lilitoa tangazo lililosomeka: "Katibu wa Bunge, kwa niaba ya Sekretarieti ya Bunge anapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia Mei 27, 2023 hadi Juni 03, 2023 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo."

Kwa mujibu wa tangazo hilo, kada zinazoongoza kwa waombaji wengi ni uchumi, sheria, udereva na uhasibu, huku kada zenye waombaji walio chini ya 100 ni afya na maktaba.

Tangazo hilo liliainisha kada hizo na idadi ya walioteuliwa kwenye usaili ikiwa kwenye mabano, ofisa hesabu daraja la II (538), msaidizi wa kumbukumbu daraja la II (279), udereva daraja la I (984), mhandi-si umeme daraja la II (234), ofisa usimamizi wa fedha daraja la II (492), mwandishi wa taarifa rasmi za Bunge darala la II (413), mchumi daraja la II (904), ofisa sheria dara-ja la I (302).

Nyingine ni ofisa Tehama daraja la II (310), msaidizi wa maktaba daraja la II (98), katibu msaidizi wa Bunge daraja la II Sheria (831), katibu msaidizi wa Bunge daraja la II uchumi (1,208), katibu msaidizi wa Bunge daraja la II (afya ya jamii/menejimenti ya huduma za afya) 47


Pia soma: Bunge limetangaza nafasi 42 za kazi kwa Watanzania wasiozidi miaka 45
 
Kwanoni wale.wa zamani wapewe intavyuu sawa na walimaliza mwaka jana, tume ya ajira muangalie teena maswali ya darasani aisee.
 
Hi habari iko kwenye gazati la nipashe, kama ni kweli hiyo hali anatupa taswira gani katika soko la ajira, hi ni timing bomb kuna haja ya vyuo kubadili mitaala ya hizi zisio kua na soko kwenye Market yetu.
Nitajie nchi moja duniani ambayo ina wasomi wengi na wameajiriwa ,Yaani hakuna tatizo la ukosefu wa ajira.
 
Kumbe mtu ana ajira af anatafuta ajira inaleta sense kweli? Mkuu anajua hizi terminology za uchumi
1. Under employment
2. Dispised Eployement
Zote hizo ni aina ya unemployment au ukosefu wa ajira mkuu.
Kuna watu kibao mimi nawajua ambao wanafanya kazi kwenye makampuni binafsi na mshahara karibu 2mil. , lakini wakisikia TRA katangaza ajira wote wanaomba kazi, kama sio uroho wa kuiba pesa huko ni nini? Hao wote wana ajira, ila watafuta ulaji mkubwa zaidi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom