Bwana Yesu asifiwe?

Bila shaka asilimia 70 ya watanzania wamchao Mungu, muda huu wenye tvs watakuwa live kufuatilia kongamano kubwa la VUKA NA CHAKO ikiwa ni maono ya mtumishi Boniphace Mwamposa yenye maudhui ya kuupokea mwaka mpya ukiwa tayari umeshapokea Baraka, uponyaji, Rehema na Mambo mengine kwa uweza wa Bwana Yesu.

Nimeona nikuwekee tukio hili kwasababu siyo kongamano dogo, uwanja umejaa kabisa. Kongamano hili lipo live kupitia channel ya ARISE AND SHINE TV. Jiungamanishe nawe uvuke na chako.

=========

Mpaka saa 22:42 apostle Mwamposa alikuwa hajapanda kwenye madhabahu yaliyoandaliwa katika uwanja wa mpira wa Benjamin Mkapa, ila kwaya na ahuhuda , sadaka na matangazo ya kawaida yalikuwa yanaendelea

======

23:10 Apostle Mwamposa aliwasili na kuanza ya Mkesha kwa kufugua na sala ya BABA YETU ULIYE MBINGUNI

View attachment 2449383View attachment 2449384View attachment 2449383
View attachment 2449385
Jana nimekutana na akina mama kadhaa wametoka nchi jirani wanasema wamekuja TZ mkeshani sikuelewa kama ni event kubwa hivi
 
Nimeona hilo na sio kwenye familia moja,
Na ukiona mkeo ameanza kuwasikiliza hawa jamaa kama mali zako uliziandika randomly kwa mtiririko wa kifamilia kaa chini tulia ziandikie vizuri maana muda wowote mnaweza kugawana vitu.
 
Hivi wanatoa sadaka? If so, kama level seat ni 60,000 na nilivyoona hapo ni kama Mkapa Stadium ipo full.

Just imagine kila mtu atoe walau 1,000 zidisha kwa watu 60,000...dadeq kweli mwenye nacho hupewa zaidi. A minimum of 60,000,000 Tsh.

Aliye nacho anazidi kuongezewa.
Makadirio ya chini ni 120000000.
Mafuta chupa 1. 60000000
Maji chupa 1. 60000000.
Ukitoa gharama za kuendesha kongamano milioni 30. Anabakiwa na milioni 90. Mfukoni
 
Mawazo yangu binafsi

Watu wanakejeli eti waliohudhulia huo mkesha ni wajinga na wanamtajirisha Mwamposa, lakini najaribu kuwaza, tatizo nikutoa kwa Mwamposa au nikwasababu wanatoa wengi? Maana hata wewe ambaye hujahudhulia, huko unakoabudu bado unatoa pesa, hata Kama uitafutie majina mazuri namna gani lakini bado unatoa pesa. Mwamposa amebarikiwa kuwa na Mvuto au kibali Cha watu, huenda wakati wake ukapita, lakini atabaki kwenye kumbukumbu za waamini Mungu kuwa, Mwamposa alikuwa na kibali. Mafundisho yake yapo OPEN Sana, anakuambia ukweli kabisa, kwamba, kuendesha kipindi Cha Tv LIVE kwenye station, ni gharama, anakuomba, Kama unaweza, changia elf 50, 20 au 10, lakini hakulazimishi Wala hakusimangi kwanini hujatoa. Wote wanaotoa, wanatoa kwa hiari yao. Na kusema ukweli tu, watu wanaotoa sadaka,popote, iwe msikitini, kanisani au kwa waganga ndiyo wanaofanikishwa zaidi, maskini ndiye mwenye tabia zakuona anaibiwa na bado hata hafanikiwi pamoja na ubahili wake.
Hayo ni maoni yangu binafsi
 
Bwana Yesu asifiwe?

Bila shaka asilimia 70 ya watanzania wamchao Mungu, muda huu wenye tvs watakuwa live kufuatilia kongamano kubwa la VUKA NA CHAKO ikiwa ni maono ya mtumishi Boniphace Mwamposa yenye maudhui ya kuupokea mwaka mpya ukiwa tayari umeshapokea Baraka, uponyaji, Rehema na Mambo mengine kwa uweza wa Bwana Yesu.

Nimeona nikuwekee tukio hili kwasababu siyo kongamano dogo, uwanja umejaa kabisa. Kongamano hili lipo live kupitia channel ya ARISE AND SHINE TV. Jiungamanishe nawe uvuke na chako.

=========

Mpaka saa 22:42 apostle Mwamposa alikuwa hajapanda kwenye madhabahu yaliyoandaliwa katika uwanja wa mpira wa Benjamin Mkapa, ila kwaya na ahuhuda , sadaka na matangazo ya kawaida yalikuwa yanaendelea

======

23:10 Apostle Mwamposa aliwasili na kuanza ya Mkesha kwa kufugua na sala ya BABA YETU ULIYE MBINGUNI

View attachment 2449383View attachment 2449384View attachment 2449383
View attachment 2449385
wapo waliyoenda kumrhangaa mwamposa na timu yake ya ukusanyaji pesa na wapo waliyoenda kwa imani .Lijamaa ni billionea haswa si yule shila hafikii hapo.
 
Mwaka jana shemeji mke wa mdogo angu alikuwa mjamzito,miezi ya mwisho mdogo wangu akaomba mkewe aje akae nyumbani kwangu kwa kuwa bi mkubwa yuko hapa pia.

Basi ikafka tarehe akajifungua salama, baada ya muda siku zile za kutoka,wakaanza kuja kuja watu kumtembelea mtoto na mama, mpaka wakati huo hakukufanyika lolote la ki mila,utamaduni wala desturi kama zile tunavyofanyaga kwa watoto wakizaliwa.

Baada ya watu kadha wa kadha, kuna siku alikuja mdada ni ndugu yake wa karibu na shemeji ambaye walikwaruzanaga sana mara kadhaa enzi mjamzito akawa hadi anamtia shuku baada ya kuona anapitia matatizo makubwa na hiyo mimba baada ya mikwaruzano na huyu ndugu ake wa karibu.

Mtoto alivyozaliwa alikuwa fresh hakukuwa na changamoto yoyote afya tele kwa mzazi na mtoto, basi baada ya huyo dada kuja, next day dogo akaanza kuwa anajinyonga nyonga tumbo huku analia sana sana,bi mkubwa akawa anajaribu kung’amua tatizo ni nini (mtu mzima dawa) basi wakaenda hospital mdogo wangu na binamu angu ni ma MD, shemeji angu mwenyewe na dada angu mkubwa ni Nurses,walifanya procedures kadha wa kadha za utaalam wao lakini dogo akawa bado na siku ya pili akawa sasa kama anapoteza nguvu.

Mama mtu (shemeji) akawa anaanza kulia, mida ya jioni saa kumi akaona isiwe shida akafungua hiyo radio ya mwamposa akaanza kufatilia ibada, ilipofika hayo maombi akachukua wese la kula na kufata maelekezo accordingly.

Mimi narudi zangu saa kumi na mbili kasoro nakumbuka ilikuwa jumatatu, ndipo ibada ipo hapo kwenye maombi, shemeji yupo chumbani na mtoto baada ya muda dakika kama 5-10 tangu nimefika nikasikia anaita kuwa mtoto alikuwa anajinyonga kama anajisaidia, akanyanyuka mdogo angu wa kike maana alikuja pia siku hiyo, akaingia kule chumbani.

Alipofika ndipo, ikabidi niitwe pia nikasogea maana waliogopa, Pale ndipo nilipoona yaliyotendeka yanayoshuhudiwaga na wafuasi wa huyu Mwamposa.

Ilinifikirisha, nikashangaa sana, bado nawaza sana kuhusu nikichokiona ingawa bado nabisha

Hizi imani na mambo ya kiroho, kama huna miongozo wala elimu ni bora kukaa kimya.
 
Back
Top Bottom