witnessj
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 28,839
- 47,772
Bila kumbana hivo asingedadavua asee.....BTW hausahau mkuu..teh teh!Afadhali ulielewa maana ulimbana arudishe Mil.6 hewa mkuu
Bila kumbana hivo asingedadavua asee.....BTW hausahau mkuu..teh teh!Afadhali ulielewa maana ulimbana arudishe Mil.6 hewa mkuu
A lesson to learnWallah Ndoa haina RAHA tupu kuna na mitihani kama hiyo ni wajibu wetu tukiwa kama binadamu kuthibiti,sisemi kua ni rahisi lakini jitahidi sana kua mvumilivu na muelewa Mkuu,kwanza fikiria familia yako pili usi fanye maamuzi ukiwa na hasiri..
Mimi yalinikuta hayo niliambiwa nimeiba mil 12 za shemeji yangu wakati hata chumbani kwa shemeji siingi,wakunitetea alitakiwa awe mumewangu nnae lalanae na kuamka nae na yeye pia alijiunga na ndugu zake sikutegemea kama angeweza kunubadilikia,lakini niliepusha shari pesa niliwapa na Sorry nikaomba nikawa nanuka wizi kwenye ukoo mzima, baada ya siku 20 nikiwa naimba mungu sanaaa kwa vilio,kumbe mtoto wa yule shemeji ndio alie chukua hela akaenda South Africa kipindi kile cha kuzamia wakakamatwa njiani hela zikaibiwa na kupigwa juu,akaletwa nyumbani hoi kuulizwa ilikuwaje ndio akasema mwanzo mpaka mwisho,ebu vuta picha kama ungekua wewe ungefanyaje?
Kama kuna mtu alie simama na mimi kua siwezi kuiba ni Mkwe wangu mamake mume wangu ukweli ulipo julikana tuu,nilifungasha wanangu kwetu nikasema hiyo pesa mkinipa sawa na msiponipa pia nimesamehe Talaka yangu mr utaileta
nyumbani kwetu.....nisikuchoshe mkuu.... chamsingi vuta subra familia yako ni muhimu sanaaaaa..
[emoji23] [emoji23] kweli mjini shule shamba kilimo .....Bila kumbana hivo asingedadavua asee.....BTW hausahau mkuu..teh teh!
Tatizo lingine ninaloliona ni pale ambapo mtu amekopa pesa na amepata, say kama huyo 6mill au hiyo 10mill, unakuta pengine hajafanya maandalizi ya kuitumia hiyo pesa kwa siku mbili tatu, kwa nini asiiiache hiyo pesa benki mpaka atakapokuwa tayari?? why kubeba 10M cash kuileta home wakati pengine manunuzi yenyewe utayafanya kwa awamu au siku nyingine?? Kuna wafanyabiashara ukifika dukani kwake ukataka kufanya manunuzi mbona huwa wanakubali money transfer ??Mkuu pole sana, Mimi ni mkristo lakin napata shida sana kwa wachungaji wa kisasa, wamevunja ndoa nyingi kwa nabii za uongo na wameleta migongano mingi katka jamii kwa nabii uchwara Mara ooh unalogwa na Jirani Mara kazin umetegewa na Leo umeleta kisa hiki.
Nakushauri usishindwe na karibu Bali ulishinde karibu.
Kuwa uvumilivu muda niwalimu ukweli utajulikana Mungu ni wa haki, nakushauri usiende kinyume na agano la ndoa, kumbuka watoto wanakutegemea, hata huyo mkeo hili likipita naye atajutia,
Hata yeye yuko njia panda akijiuliza kama wew hujachukua nani kachukua?
Kuna kisa kama cha mkeo, alikopa pesa kufika home zikapotea 10,000,000/=
Uko sahihi wengi hawajajua madhara ya kutembea na cash, vema watu waelimikeTatizo lingine ninaloliona ni pale ambapo mtu amekopa pesa na amepata, say kama huyo 6mill au hiyo 10mill, unakuta pengine hajafanya maandalizi ya kuitumia hiyo pesa kwa siku mbili tatu, kwa nini asiiiache hiyo pesa benki mpaka atakapokuwa tayari?? why kubeba 10M cash kuileta home wakati pengine manunuzi yenyewe utayafanya kwa awamu au siku nyingine?? Kuna wafanyabiashara ukifika dukani kwake ukataka kufanya manunuzi mbona huwa wanakubali money transfer ??
Lazima au mparee washenzi sana haya makabila wabinafsi ajabu...Aisee mchaga au
mchungaji mama mchungaji, kafanya manyanga yake akaonekana mume kachukua.mko wa3 kwanini akomae kuwa wewe ndo umechukua?
hu story inaniumaaaHakuna pahala niliposema karudi napesa in fact kagundua asubuhi kwamba hana pesa, alivyorudi hakuangalia pochi yake hadi asubuhi
Ndio maana asubuhi hakunituhumu mm, tulishauriana kwa pamoja uwezekano wa wapi kapoteza shida ni jioni alipokwenda kwa mchungaji na kuaminishwa kuwa mchungaji kaona maono
Hivyo msingi wa ushahidi wake ni maono ya mchungaji
Kama kweli angekiri aliziona hizo pesa ndani ya pochi aliporudi basi hata mm ningeshtuka sana huenda tuna majini ndani lakini anakiri mwenyewe hakuangalia pochi usiku
Hivyo possibility kaibiwa hajafika home
Huyo ni pastor au mpiga ramli????Huyo Pastor naye ni wakupiga makofi..Wife inaonekana hajui kazipoteza kwenye mazingira gani..Sema maneno ya Pastor ndo yamemjaza ujinga
poa vipi mamy?Mambo mrembo
Alichowaza ni wewe usiingie kuitegemea hyo 6M yake ila mbinu alotumia ndo ya kishenzi,sasa wewe kua mshenzi zaidi yake.vaa sula ya beberu mpaka aikimbie nyumba,na huko atakakoenda hzo 6M zake zikiisha utamuona anarudi kabeba biblia mkononi kawa mhubili,atakua amekuja kavaa ngozi ya kondoo.fukuza kama nyoka.Karibu tenaMwezi mmoja uliopita mke wangu alipata mkopo kutoka mahala fulani wa shilingi 6 million, lengo la mkopo huo ilikua ni kuimarisha biashara yake ya restaurant na kuipanua zaidi, mimi ndie nilitoa mtaji wa hiyo restaurant wakati inaanza.
Siku ya tukio alichukua pesa hizo benki na kuziweka kwenye pochi kubwa na kuanza kuzunguka nazo tangu asu ubuhi hadi jioni aliporudi, mimi nilirudi usiku mwingi kutoka kwenye pombe na nilimkuta ameshalala nilihudumiwa na hg chakula nikaenda kulala, asubuhi ndipo hakuziona pesa zake kwenye pochi.Mimi sikua najua hata kaja na hela hadi aliposema haoni pesa zake na kuangua kilio kizito sana.
Jioni akaenda kwa mchungaji wa kanisa lao na kufanya maombi kuhusu jambo hilo, eti katika maombi hayo mchungaji akaoneshwa kuwa ni mimi ndio nimechukua hizo pesa, usiku hatukulala aliongea usiku kucha tena sebuleni akipayuka kuwa nimrudishie hela zake la sivyo ndoa itaishia hapo na atanifungulia kesi, ni mwezi sasa tangu tukio hilo hatuongeleshani, hakuna tendo, usiku anakwenda kulala kwa watoto, ametoa ultimatum kuwa kama sijamrudishia pesa zake nisije nikamlaumu, nikamjibu sawa naisubiri hiyo ultimatum tuone,
Nimekataa vikao vyote vya usuluhishi kwa sababu ya maneno yake machafu, na nimeona ni udhalilishaji kwenda kujadili kuwa nimechukua hela pesa za mke wangu, kama hataki abebe vitu vyake aondoke, nimejiepusha kumpiga tangu mwanzo kwa kuzuia hasira zangu, lakini sasa inaenda kushindikana
Kuna yoyote kati yenu mwenye wazo jipya juu ya ufumbuzi wa mgogoro huu?
Maana nimeathirika kisaikolojia, watoto pia hawaelewi kwanini mama analala room kwao, wameathirika pia, lakini zaidi ya yote nina mwezi mzima sijapata haki yangu ya msingi (matrimonial right) na sasa nimeanza kufikiria njia mbadala iwapo mgogoro huu utaendelea.
Nahitaji mawazo yenu
Safi bibie,sijakuona mida. Shem kabana ninipoa vipi mamy?
Teh teh..Hakuna tofauti MpendwaHuyo ni pastor au mpiga ramli????