dedan kimathi
Member
- Dec 5, 2015
- 42
- 24
Mwezi mmoja uliopita mke wangu alipata mkopo kutoka mahala fulani wa shilingi 6 million, lengo la mkopo huo ilikua ni kuimarisha biashara yake ya restaurant na kuipanua zaidi, mimi ndie nilitoa mtaji wa hiyo restaurant wakati inaanza.
Siku ya tukio alichukua pesa hizo benki na kuziweka kwenye pochi kubwa na kuanza kuzunguka nazo tangu asu ubuhi hadi jioni aliporudi, mimi nilirudi usiku mwingi kutoka kwenye pombe na nilimkuta ameshalala nilihudumiwa na hg chakula nikaenda kulala, asubuhi ndipo hakuziona pesa zake kwenye pochi.Mimi sikua najua hata kaja na hela hadi aliposema haoni pesa zake na kuangua kilio kizito sana.
Jioni akaenda kwa mchungaji wa kanisa lao na kufanya maombi kuhusu jambo hilo, eti katika maombi hayo mchungaji akaoneshwa kuwa ni mimi ndio nimechukua hizo pesa, usiku hatukulala aliongea usiku kucha tena sebuleni akipayuka kuwa nimrudishie hela zake la sivyo ndoa itaishia hapo na atanifungulia kesi, ni mwezi sasa tangu tukio hilo hatuongeleshani, hakuna tendo, usiku anakwenda kulala kwa watoto, ametoa ultimatum kuwa kama sijamrudishia pesa zake nisije nikamlaumu, nikamjibu sawa naisubiri hiyo ultimatum tuone,
Nimekataa vikao vyote vya usuluhishi kwa sababu ya maneno yake machafu, na nimeona ni udhalilishaji kwenda kujadili kuwa nimechukua hela pesa za mke wangu, kama hataki abebe vitu vyake aondoke, nimejiepusha kumpiga tangu mwanzo kwa kuzuia hasira zangu, lakini sasa inaenda kushindikana
Kuna yoyote kati yenu mwenye wazo jipya juu ya ufumbuzi wa mgogoro huu?
Maana nimeathirika kisaikolojia, watoto pia hawaelewi kwanini mama analala room kwao, wameathirika pia, lakini zaidi ya yote nina mwezi mzima sijapata haki yangu ya msingi (matrimonial right) na sasa nimeanza kufikiria njia mbadala iwapo mgogoro huu utaendelea.
Nahitaji mawazo yenu