Mke anadai mimi nimemuibia pesa zake, amani imetoweka

Mke anadai mimi nimemuibia pesa zake, amani imetoweka

Dah,mkuu mchungaji anacheza na ndoa yako,possibly anashirikiana na mkeo na kashakuwa brain washed,inawezekana kabisa mkeo kampa pesa hizo mchungaji baada ya kukopa,mchungaji anajua mtu pekee mwenye uwezo wa kulipa 6m ni wewe,ndo maana wanataka utafute hizo pesa umlipe /fidie mkeo
Wachungaji wengi siku hizi ni wa ovyo kuliko maelezo na wanayoyafanya mara nyingine hawana tofauti na waganga wa kienyeji!
Ni wapenda fedha, wazinzi wa kutupwa (kwa siri), wezi, waongo, wazushi, walaghai, wenye kujikweza, wasingiziaji, wachonganishi na waharibifu wa amani na utulivu katika jamii. Wanajipa majina makuubwa ya Manabii, Mitume na Maaskofu kumbe ni wafuasi waaminifu wa Ibilisi! Bila shaka mkeo kakutana na mmojawapo.
 
Yaani hao wangesa wanawaamini hao chui ndani nje kondoo kwa asilimia zote. Huyo anatafuta sababu. Alafu umeshafuatilia kujua kama ni kweli amechukua mkopo
 
Alafu huyo ni mchungaji au mganga? Maana hapo inaonekana kapiga lamli.
 
Wewe ndoa yako inamatatizo tangu mwanzo, mke wako anaenda kuchukua mkopo hujui? itakua hamshirikiani kenye mambo ya kiuchumi kwanini akusingizie wewe nawakati wote mnatafutia lfamilia moja? au yeye ana mambo yake na wewe mambo yako. Inawezekana ana abudu kanisa ambalo hulitambui wala wewe huendi kwenye hilo kanisa. Then ml 6 kutembea nazo kwenye mkoba siku nzima si jambo linaloingia akirini.
 
mkuu tafadhali huwezi iondoa ile sehemu ya bastola yako ili story iendane
 
Pole mkuu. Hata namimi nimeathirika kwa namna moja au nyingine na post hii.Hata sijui nifanyaje sasa.
 
mkuu hilo liko wazi wapo japo wachache wanatafuna kondoo balaa, kuna mmoja alitia fora alitafuna wasichana karibu wote na baadhi za wake za watu mwishowe akakimbilia mkoa mwingine baada ya dili kujulikana
hahahaaa, kazi kweli kweli
 
Wachungaji wengi siku hizi ni wa ovyo kuliko maelezo na wanayoyafanya mara nyingine hawana tofauti na waganga wa kienyeji!
Ni wapenda fedha, wazinzi wa kutupwa (kwa siri), wezi, waongo, wazushi, walaghai, wenye kujikweza, wasingiziaji, wachonganishi na waharibifu wa amani na utulivu katika jamii. Wanajipa majina makuubwa ya Manabii, Mitume na Maaskofu kumbe ni wafuasi waaminifu wa Ibilisi! Bila shaka mkeo kakutana na mmojawapo.
sasahivi dini imekuwa business
 
Mwezi mmoja uliopita mke wangu alipata mkopo kutoka mahala fulani wa shilingi 6 million, lengo la mkopo huo ilikua ni kuimarisha biashara yake ya restaurant na kuipanua zaidi, mimi ndie nilitoa mtaji wa hiyo restaurant wakati inaanza.

Siku ya tukio alichukua pesa hizo benki na kuziweka kwenye pochi kubwa na kuanza kuzunguka nazo tangu asu ubuhi hadi jioni aliporudi, mimi nilirudi usiku mwingi kutoka kwenye pombe na nilimkuta ameshalala nilihudumiwa na hg chakula nikaenda kulala, asubuhi ndipo hakuziona pesa zake kwenye pochi.Mimi sikua najua hata kaja na hela hadi aliposema haoni pesa zake na kuangua kilio kizito sana.

Jioni akaenda kwa mchungaji wa kanisa lao na kufanya maombi kuhusu jambo hilo, eti katika maombi hayo mchungaji akaoneshwa kuwa ni mimi ndio nimechukua hizo pesa, usiku hatukulala aliongea usiku kucha tena sebuleni akipayuka kuwa nimrudishie hela zake la sivyo ndoa itaishia hapo na atanifungulia kesi, ni mwezi sasa tangu tukio hilo hatuongeleshani, hakuna tendo, usiku anakwenda kulala kwa watoto, ametoa ultimatum kuwa kama sijamrudishia pesa zake nisije nikamlaumu, nikamjibu sawa naisubiri hiyo ultimatum tuone,

Nimekataa vikao vyote vya usuluhishi kwa sababu ya maneno yake machafu, na nimeona ni udhalilishaji kwenda kujadili kuwa nimechukua hela pesa za mke wangu, kama hataki abebe vitu vyake aondoke, nimejiepusha kumpiga tangu mwanzo kwa kuzuia hasira zangu, lakini sasa inaenda kushindikana

Kuna yoyote kati yenu mwenye wazo jipya juu ya ufumbuzi wa mgogoro huu?

Maana nimeathirika kisaikolojia, watoto pia hawaelewi kwanini mama analala room kwao, wameathirika pia, lakini zaidi ya yote nina mwezi mzima sijapata haki yangu ya msingi (matrimonial right) na sasa nimeanza kufikiria njia mbadala iwapo mgogoro huu utaendelea.

Nahitaji mawazo yenu

1.Binafsi me kwanza siamini kama Mwanaume anaweza kumwibia mke wake
2.Lazima uelewe kabisa kwamba Wachungaji wa Show siku hizi wanavunja ndoa za watu
3.Tafadhali tulia kwanza usiisaliti ndoa yako hilo litakuja kuwa jipu mbeleni
4.Usimlipe Pesa yake kabisa kama noma na iwe noma, hili linauzi, vitu vya kusingiziwa huumiza sana
5.Endelea naye vivyo hivyo na akianza kuropoka wewe rekodi, lakini pia Mwambie aende mahakamani kama kaibiwa, sheria hazitambui maombi
6.Pole sana kwa hali unayopitia najua unayopitia.
 
unazo pesa , ndio maaana ukaweza kurudisha 12m ingawa hukuiba, unafikiri ungekuwa huna ungeweza ?
Alhamdulillah lakini kwa nilivyo hata dhahabu zangu ningeuza kwa walivyonibadilikia manake wakiingia wakitoka
Huna shukrani hupendi wenzio waendele we acha sitaki hata kukumbuka...
 
Inategemea kama unataka kuendelea kuwa na Mkeo au unataka kumtosa.Wazungu wanasema 'sometimes when you are dealing with a woman you have to show that she is the winner and you are a loser'. Hivyo tafuta namna ulipe hizo fedha lakini 'time will always tell'..
 
Alhamdulillah lakini kwa nilivyo hata dhahabu zangu ningeuza kwa walivyonibadilikia manake wakiingia wakitoka
Huna shukrani hupendi wenzio waendele we acha sitaki hata kukumbuka...
pole saana mamy, ungewambia msome albadir hapo home kabla haujalipa , uone wangesemaje ?
 
Hapo ndio ningeitwa mwanga kabisa,lakini bado moyo una jeraha na imani inapungua...
ok , kwa hali hiyo ni ngumu kulitibu hilo jeraha kwa muda mfupi,itachukua mda saana, maisha yana changamoto nyingi,ingawa naona ww ni kati ya watu wema sana
 
Huo si mkopo kuna mtu kampa ya kuanzia maisha baada ya kuvunja ndoa yenu. Huyo alikuwa na sababu zake mwanzo. Unganidha dots huyo mchungaji fake anaweza akawa ndo kikulacho chenyewe
 
Asee hii ni hataree....ina maana wewe hukuchukua pesa zake?

Na kama alirudi ucku na hizo pesa zake na mnalala wawili chumbani ni nani kazichukua sasa?

NB: kama mkuu alivyonena hapo juu, mlipe ankara yake amani irudi ndani ya nyumba bana!...mambo mengine ya kujitakia.
Nani ana uhakika kuwa kweli alirudi na hizo hela?
 
Back
Top Bottom