Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Vipi kama walikuwa wanamzomea mmoja wa aliyekuwapo kwenye msafara na sio Mheshimiwa Mkapa?

HAPA HAKUNA KUZUNGUKA MKAPA NDIYE ALIYOZOMEWA KWASABB NI MWIZI NA KAMA YEYE SI MWIZI AKANUSHE.

naomba kuuliza nani ata washtaki wale vijana polisi au mkapa??
 
Nyani Ngabu,

Sikuhizi hapa Mbagala vijana humtania kila anayeendesha gari la thamani kama GX, VX etc kuwa ni FISADI. - ni utani tu.

Je unajuaje hakuwepo mtu wa aina hiyo jirani kapaki?

Wanajuaje kama haikuwa coincedence tu?

Kuna uwezekano mkubwa (ukizingatia uchumi wa Tanzania) mtu anayeendesha GX, VX, etc. kuwa fisadi. Sasa, hata katika ufisadi kuna viwango. Kuna mafisadi wa small scale, medium scale, na kina Mkapa na Chenge ambao hamna hata daraja la kuwaweka. Kwa hiyo sishangai kabisa kwa walalahoi wasukuma mikokoteni, watembea kwa miguu, waendesha baiskeli, na wapiga debe kuwaona waendesha magari ya thamani kuwa ni mafisadi. Disparity iliyopo ni ya ajabu sana kiasi kwamba huwezi kuamini mtumisha wa serikali kuwa tajiri kupindukia.

Halafu kama ni utani kwa nini sasa watu wakamatwe? Na kama walikuwa hawamzomei Mkapa, ina maana na mimi Ngabu nikikuzomea wewe Fikiraduni nitakamatwa? Or in other words siku hizi kuzomea limekuwa kosa linalo-warrant kukamatwa na polisi?
 
Kosa la kuhatarisha Amani.Mathalani kama wangempiga Risasi Rais mstaafu unaju Madhara yake ni yapi.

Gembe, majibu haya hapa, asante kwa mwanakijiji:

Mzee Mwanakijiji said:
a. Kama walikuwa kwenye msafara wakaona watu wanapiga kelele "Fisadi" "Fisadi" wanapoteremka na kufanya msako, wanajuaje walioawakamata NDIYO waliosema "fisadi"?

b. Je kama vijana hawa wangesimama na kupiga kelele "Mtukufu" "Mtukufu" ni hatua gani wangechukuliwa au zawadi gani wangepewa?

c. Uhuru wa maoni ni pamoja na uhuru wa maoni ya kijinga. Katiba haisemi mahali popote kuwa maoni yatakayotolewa na wananchi lazima yawe mazuri au yanayopendeza ili yakubaliwe.

d. HIvi wanazojela za kutosha? Maana tukianza hii movement ya "Fisadi" "Fisadi" wataweza kweli kuwasweka watu ndani au watalazimika kutumia njia "kali" zaidi... ?
 
au kama vipi atumie vijisenti vyake kununua chopper/'copter ya kumpingisha misele hapo mjini.......maana inaonekana huu ndio mwanzo tu, watu watazidi kumzomea kila aendako!!

Hata hivyo vijisenti sio vyake....kaiba au kajipatia kwa njia zisizo halali.
 
Naomba kuuliza wakuu:

Bara barani wana pita watu wengi na wengine wanakuwa wamekaa au kusimama, Polisi walijuaje kuwa anayezomewa ni Mheshmiwa Mkapa?. Vipi nikisema alikuwa anazomewa kijana mmoja aliyeketi au kusimama upande wa pili wa barabara na sio Mheshmiwa?

Ni kuuliza tu, NISAIDIENI majibu.

Jibu liko dhahiri, ingekuwa koinsidensi ya hali ya juu, fisadi kupita na msululu wake na ataniwe kijana mwingine upande wa pili, ndio maana wakawazoa vijana wenye uchungu wa kuibiwa utajiri wao.
 
au kama vipi atumie vijisenti vyake kununua chopper/'copter ya kumpingisha misele hapo mjini.......maana inaonekana huu ndio mwanzo tu, watu watazidi kumzomea kila aendako!!

kwi kwi kwi kwi mbavu zangu!
Poor Mkapa, sidhani kama aliwahi kufikiri hili wakati akifungua genge pale ikulu!
 
Kosa la kuhatarisha Amani.Mathalani kama wangempiga Risasi Rais mstaafu unaju Madhara yake ni yapi.

madhara ni kuwa angekuwa amepigwa risasi! haihitaji utaalamu wa kufikiria madhara ya mtu kupigwa risasi.

But, hatuwezi kuanza kukamata watu kwa mawazo yao. Kwamba labda wangefanya kitu fulani au wangefanya jambo fulani vinginevyo kuna watu wengi wenye mawazo machafu kweli kuhusu viongozi wao.

Hawa wamedaiwa kufanya jambo moja tu na tusianze kurundika possible crimes; wao walisikika wakizomea (even that is questionable) "fisadi"! Ni hilo tu ndilo liwe msingi wa majadiliano yetu kwani kujaribu kuingia kwenye mawazo yao ni kujaribu kufanya lisililowezekana. Walikutwa na silaha? walikutwa na maandishi ya kichochezi?

So far sijaona mahali popote kwamba walikuwa na lengo lolote la kumdhuru Rais mstaafu. Kama wangedaiwa kufanya jambo kama hilo bila ya shaka mimi ningekuwa wa kwanza kulaani vitendo vya kujichukulia sheria mikononi. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na mambo yanaweza kumalizwa kwenye sanduku la kura, mahakamani, au barazani!
 
Hapo nakubaliana na wewe kwa asilimia 25 tu!
 
Kuna uwezekano mkubwa (ukizingatia uchumi wa Tanzania) mtu anayeendesha GX, VX, etc. kuwa fisadi. Sasa, hata katika ufisadi kuna viwango. Kuna mafisadi wa small scale, medium scale, na kina Mkapa na Chenge ambao hamna hata daraja la kuwaweka. Kwa hiyo sishangai kabisa kwa walalahoi wasukuma mikokoteni, watembea kwa miguu, waendesha baiskeli, na wapiga debe kuwaona waendesha magari ya thamani kuwa ni mafisadi. Disparity iliyopo ni ya ajabu sana kiasi kwamba huwezi kuamini mtumisha wa serikali kuwa tajiri kupindukia.

Halafu kama ni utani kwa nini sasa watu wakamatwe? Na kama walikuwa hawamzomei Mkapa, ina maana na mimi Ngabu nikikuzomea wewe Fikiraduni nitakamatwa? Or in other words siku hizi kuzomea limekuwa kosa linalo-warrant kukamatwa na polisi?

Nyani..huwa hatuonani eye to eye kule kwenye ile "thread nyingine" lakini hapa kaka ume drive point nyumbani. Tatizo ni kwamba Polisi wetu wamezoea ku abuse haki za wananchi, na wananchi japokuwa wameanza kuamka sasa hivi, wengi hawajui haki zao. Watanzania kwa kipindi kirefu tumejengwa kwenye tamaduni za kuwa submissive, obedient, na "shikamoo mzee" towards viongozi wetu. Nafikiri huko kwenye Police Academy wabadilishe curriculum..waanze kuwa train Police kutumia akili zaidi kuliko misuli.
 
Tatizo linalo-compound tatizo ni polisi wenyewe kutokujua job description yao na ku-operate kutokana na nidhamu ya woga.
 
Hii kesi nzuri sana, na haiwezi kufika kokote.

Kwa sababu hawa vijana wakipelekwa mahakamani tu hapo hapo ndipo mitandao yote ya Civil Society inayojali maendeleo ya Tanzania inapotakiwa kuwatetea, na kumuita Mkapa mahakamani ajibu shutuma za vijana.

I would love Slaa on their defence and Mkapa on the stand.

Mkapa anaweza kuwaambia wawaachie tu kwa kuua soo mambo yasije yakawa mabaya zaidi in a popular uprising.

Hawa vijana hawafungiki, wakiwafunga watawafanya kuwa martyrs na popularity ya Mkapa itaanguka chini zaidi, ataonekana siyo tu fisadi bali ni fisadi mkandamizaji.

Hawa polisi nao wanajishaua tu huenda hawakutumwa wala nini, njaa zao tu na kujifanya vijibwa vya wakubwa, hawana principle wala nini.

Speaking of incidents za maskani na polisi,I will never forget kitambo niko maskani waiting for my results siku polisi walipokuja kwenye kijiwe chetu Upanga kutaka kutu harass, wakaanza zao.

Polisi- "Nyinyi mnafanya nini hapa"

Sie "tumepumzika nyumbani"

Polisi "Wewe unakaa wapi?"

Kijana1 "Hapo nyuma"

Polisi "Na wewe?" (arrogantly)

Kijana2 "Hapo Nyuma"

Wakamfikia mtoto wa kishua mwenyewe sasa

Polisi "Na wewe?"

Mtoto wa kishua "Mimi nakaa kwa Ben"

Polisi "Kwa Ben, Ben gani huyo"

Mtoto wa kishua "Ben huyo huyo wa Jamhuri ya muungano, kwani kuna Ben wangapi tena"
Polisi (attitude imebadilika katika U Turn ya 180 degrees "Haa hapana wazee, siyo hivyo unajua ni katika kujuana tu, eenh ni katika kujuana tuu"
Jamaa kuanzia siku hiyo maskani hawakuigusa, hamna sheria hamna morals hamna principles, ni uonevu na upendeleo tu.
 
Problem ya kesi kama hii ni kama ile kesi ya waandamanaji Buzwagi 3 weeks ago. Wataswekwa rumande, kupoteza hela za walipa kodi bure, kisha baada ya miezi miwili kuachiwa huru.

What a waste of resources and human rights violation!
 
Si watu walitaka mkapa aende mahakamani?

Naona sasa anaweza kujipeleka mwenyewe. Vijana wakitaka kuprove kuwa ni FISADI data ziko za kumwaga tu.
 
Problem ya kesi kama hii ni kama ile kesi ya waandamanaji Buzwagi 3 weeks ago. Wataswekwa rumande, kupoteza hela za walipa kodi bure, kisha baada ya miezi miwili kuachiwa huru.
What a waste of resources and human rights violation!

Dang! That would be harsh....
Miezi miwili jela kwa kuzomea....I hope they won't even spend a minute in custody...
 
Kwa anayejua ratiba ya Ben, please nipatieni, na mimi nataka kutia timu kwenye msafara wake nipayuke MKAPA FISADI!

Niende mahakamani ku-prove yeye ni FISADI, vielelezo vyote ninavyo, na yeye (ANBEN) aitwe kuja kukanusha, akisaidiwa na rafikize vijisenti, yona, pesambili, tluway!!
 
kwi kwi kwi,

Kuanzia leo Mkapa atabadili ratiba baada ya kilichotokea! Nadhani the best way ni kufanya shtukizo hadi yeye na walinzi wake washangae. Unasubiria akiwa kwenye good moments zake (hasa kwenye ile hotel .....x..... anayotembelea ijumaa jioni kuchati na mafisadi wenzake) kisha unatokea na bonge la bango limeandikwa fisadi fisadi fisadi na kutumia vipaaaza sauti ukicheza muziki wa I work it out ... i work it out... i work it out....
 
Back
Top Bottom