Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Kama kweli Makani unataka tukuamini basi J5 uwe wa kwanza Mahakamu kuu na sisi tutachanga gharama za kesi hii .
 
Kama kweli Makani unataka tukuamini basi J5 uwe wa kwanza Mahakamu kuu na sisi tutachanga gharama za kesi hii .

J5 ni Boxing day (Public holiday) Mkuu check ur facts b4 being carried away...
 
Makani ongeza moto.

Masikini Mkapa sijui kama atapona kwa mambo yanavyomuandama ni lazima aseme tu. Naona sasa kila mtu avune alichopanda.

Kama alipanda miiba lazima aivune tuu.
 
J5 ni Boxing day (Public holiday) Mkuu check ur facts b4 being carried away...

Mkuu si unajua kila mtu yuko kijiji tofauti, nafikiri kwa taratibu za kijiji anachoishi J5 ni siku ya mzigo.

Tukumbushane tunapokosea,
Nakumbuka kuna mtu alipost thread kuulizia kesi ya kamanda Zombe inavyoendelea, wakati jina aliloquote lilikuwa 'Kombe'.
 
Mkuu si unajua kila mtu yuko kijiji tofauti, nafikiri kwa taratibu za kijiji anachoishi J5 ni siku ya mzigo.

Tukumbushane tunapokosea,
Nakumbuka kuna mtu alipost thread kuulizia kesi ya kamanda Zombe inavyoendelea, wakati jina aliloquote lilikuwa 'Kombe'.

Poa mkuu nimekupata lakini mara ya mwisho huyu mkulu (Lunyungu) alituma ripoti akiwa somewhere Musoma ambapo kwa jiografia yangu ya std 7 ipo Tz yenye kusherehekea boxing day

On serious note: Hivi huyu Makani haya si aliyasema abt 3 or 4 months ago mpaka leo kimya au ndio mambo ya kutishia mtu mzima nyau...
 
Hadi sasa niko Musoma na J5 naelekea Kamachumu then Uganda .Mimi ni mjasiriamali .Mimi J5 nitakuwa mzigo kama kawaida .
 
Hadi sasa niko Musoma na J5 naelekea Kamachumu then Uganda .Mimi ni mjasiriamali .Mimi J5 nitakuwa mzigo kama kawaida .

Safi kabisa ukifika Uganda tupe habari za kifo cha rebel leader wa LRA Koni. Aminia mkulu
 
Mkapa, is in a very big trouble kama anafikiri kuwa matatizo yake yatazimwa hivi hivi, yaani hiyo kwake ni ndoto ya mwendawazimu, mimi ningekuwa yeye ningeanza kuurudisha mgodi wa Kiwira, maana hataamini what is coming to him kuhusiana na huo Mgodi,

Makani, aendelee tu maana somehow somewhere atakutana na hii movemment inayotaka kurudishwa kwa Mgodi huo, besides ni bora kuliko kunyamaza kimyaaa!

Bravo Makani!
 
kinachonikera ni hii tabia yetu ya kiromo romo.

huyu naye keshasema sana hii kauli hamna matendo.

wasanii kila kona na ndio hapo watanzania mnawapa wakati mgumu wa kutofautisha maana sawa na hadithi alieuziwa dhahabu kauzewa feki na yeye katoa fedha feki kwa hiyo wote matapeli
 
hivi koni amekufa? ni lini? au unakusudia yeye amemuua yule msaidizi wake?


m7 (museveni) kamshutumu hadharani koni kwa kumuua msaidizi wake.
hii aliifanya wakati akiongea na wajumbe wa mkutano wa amani na akawa quoted na magazeti. lakini hii ni nje ya mada, tuendelee na mada husika
 
Hii kesi mimi niko tayari kutoa mchango wa kuwalipa mawakili. Lazima tuwaonyeshe viongozi kwamba wao sio miungu. Wanapochaguliwa na Watanzania basi waongoze kwa heshima na taadhima na kuhakikisha wanaongoza kwa kuheshimu maadili ya uongozi na sio kutumia muda wao kama viongozi kujitajirisha wao na familia zao. Hii kesi kama itafunguliwa itakuwa ni hatua kubwa sana kwa Tanzania katika kuhakikisha tunapambana na mafisadi bila woga. Na pia itawasababisha mafisadi wengine wafikirie mara mbili mbili kabla ya kuingia mtamboni ili wajitajirishe maana watajua Watanzania wananiangalia na wakianza kujiuliza kulikoni na utajiri wa huyu jamaa alioupata alipokuwa kiongozi basi watanifungulia mashtaka na mali zangu zote zitafilisiwa na mvua zitaninyeshea huko lupango. Umefika wakati Watanzania inabidi tuwaambie mafisadi, enough is enough. Nchi yetu ina utajiri wa hali ya juu ambao unawanufaisha mafisadi wachache sana wakati walio wengi wanaendelea kuishi katika dhiki iliyokithiri. It can be done let's play our part.
 
Kama habari hizi zina ukweli wowote basi Bob Makani atakuwa Mandela wa Tanzania...
Na hakika heshima zangu kwake zitakuwa hazina mfano pamoja na kwamba simfahamu vizuri background yake. yaani siwezi kuamini hadi kitu hii imefika kunakotakiwa....
 
Mkandara,
Bob Makani ni lawyer na pia mwanauchumi. I hope he means what he says.
 
Jasusi na dogo,
Shukran sana, mnajua lakini kuwa Tanzania vyeti vyetu hutumika kwa kusema sana.. nataka kuona vitendo, wamesema wengi akina Salim, Mwinyi, Prof. Shivji yaani list ni kubwa mno hawa wote maneno mazito lakini matupu!....kila mtu hulisukuma mbele file.
 
Jasusi na dogo,
Shukran sana, mnajua lakini kuwa Tanzania vyeti vyetu hutumika kwa kusema sana.. nataka kuona vitendo, wamesema wengi akina Salim, Mwinyi, Prof. Shivji yaani list ni kubwa mno hawa wote maneno mazito lakini matupu!....kila mtu hulisukuma mbele file.

Sasa ni nani atamvalisha paka kengere????
 
Sounds like another mkwala mbuzi to me, ntu nzima ka Nkapa atishiwi nyau, lets wait and see kama aliyoyasema yalikua sio ya kufurahisha baraza tu.
 
Hapo kumshitaki rais mstaafu atapigwa danadana hadi achoke mwenyewe. Kesi ya kwanza itabidi aombe mahakama imfutie "immunity" ya kutoshitakiwa, na hii itasikilizwa kwa miaka 5, halafu watatoa uamuzi kwamba hawezi kufutiwa. Atakata rufaa kwa miaka mingine 5. Halafu ndipo ije kesi ya msingi. Unadhani hadi hapo bado watakuwa na nguvu za kuendelea na kesi hiyo? Wote mwenye kushtaki na mshtakiwa watakuwa weshajichokea kwa uzee! Ndipo upande wa utetezi utakapokuja na hoja za kudai mteja wao ni mzee sana au ni mgonjwa, hawezi kuhimili mashtaka. Hiyo itaendelea kusikilizwa tartiiiibu hadi mzee wa watu atakaporejea kwa Mola wake peacefully!

Kwa kujikumbusha tu, jaribuni kutafuta habari ya kesi ya Gen Augusto Pinochet wa Chile, ambaye hadi anafariki akiwa na miaka 87, bado kesi yake ilikuwa katika "danadana", walianza kudai kikatiba hawezi kushtakiwa, ana "immunity", ikachukua miaka mingi tu kusikiliza hiyo kesi ya immunity na hatimaye kutamka ana kesi ya kujibu. Kisha mawakili wake wakaja na madai ya "senility and ill health", kwamba mzee Pinochet is "too ill to stand trial", nayo ikawa na lots of legal wrangle. Hadi anafariki at 87, kesi ya msingi ilikuwa haijasikilizwa.

Ushauri kwa nd Makani na wenzie wenye mawazo hayo ni kwamba badala ya kupoteza muda kupambana na mtu mmoja (ambaye dalili zinaonesha wazi kuwa kwa mfumo uliopo haiwezekani kumshinda), ni bora kuelekeza nguvu katika kuubadilisha mfumo huo ili huko mbeleni watu wasiwe na nafasi ya kufanza hayo madudu wanayomtuhumu nayo Mkapa, na pia kuwezesha hatua rekebishi kuchukuliwa dhidi ya watakaokiuka.
 
Mwana CHADEMA huyo ambaye ni mjumbe wa kudumu katika kamati ya utendaji ya Taifa ya chama hicho, alitangaza kusudio hilo juzi alipokuwa akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Shinyanga katika viwanja vya shule ya msingi Jomu.
...hii ni staili ya wanasiasa kutafuta njia ya kutokea. Mtu makini huwezi kumsikia anaongelea suala kama hili kwenye mikutano tena ya wazi; tungepaswa kusikia vyombo vya habari vikiripoti toka mahakamani kuwa Bw. Makani amefungua kesi dhidi ya BWM. (he should borrow a leaf from Mtikila)

...apelekwe mahakamani akashitakiwe, na kama hawana wa kumshitaki, mimi najitolea nitakwenda kumshitaki,” alieleza Bw. Makani.
Nashindwa kuelewa hapa alikuwa anamueleza nani? Kama ni $erikali tayari anajua hawana mpango wa kumshitaki BWM; sasa alikuwa anamwambia nani? Hii ni wazi alikuwa anatafuta namna ya kuufurahisha mkutano kama ilivyo kwa viongozi wengine wengi wa kisiasa. Alikuwa anataka kutumia issue iliyoko midomoni mwa wananchi wengi ili aonekane bado yu hai kisiasa.

Tunasubiri tuone vitendo lasivyo ipo siku tutamuuliza alikuwa anamaanisha nini! CHADEMA msaidieni, kinyume na hapo mtaonekana wote ni wababaishaji kwani ameshasema wazi kuwa CHADEMA kama chama inatafsiri tofauti ya kifungu kinachotoa kinga kwa Rais. Msipochukua maamuzi ya kimatendo tutawaona nanyi ni wahujumu nchi kwa sababu theoretically mmeshatuonyesha ukweli ila mnaendelea kumlinda BWM. Mnadhani nani wa kuifanya hii kazi kama si ninyi kwa niaba ya wanachama na wapenzi wenu?
==============
 
Back
Top Bottom