Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa amtesa Rais Kikwete

na Charles Mullinda

DHAMBI ya ubaguzi na kuchafuana majina iliyoibuka wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa imeanza kumwandama Rais Jakaya Kikwete.

Rais Kikwete, sasa analazimika kubeba mzigo wa tuhuma zinazodaiwa kufanywa na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, wakati akiwa madarakani kwa muda wa miaka kumi.

Sasa anaonekana kuwekwa katika mtego wa kumlazimisha kuwatosa baadhi ya washirika wake wa karibu waliofanikisha ushindi wake katika uchaguzi wa 2005.

Angali bado na mzigo wa tuhuma za ufisadi zinazowaandama wasaidizi wake, Kikwete sasa ameanza kugeuziwa kibao na wana CCM wenzake kwa kumkosoa na kumtuhumu waziwazi mtangulizi wake, ‘mzee’ Mkapa, anayedaiwa alibadili kanuni za kumpata mshindi katika uchaguzi huo ili kuwezesha ushindi kwa Kikwete.

Aidha, Rais Kikwete ambaye ni mmoja wa vigogo 11 waliotajwa katika orodha ya mafisadi iliyotangazwa hivi karibuni na viongozi wa kambi ya upinzani, yuko katika hatari ya umaarufu wake kuendelea kuporomoka iwapo ataendelea na uamuzi wake wa kumkingia kifua Mkapa asijibu tuhuma zinazoelekezwa kwake.

Hatua ya hivi karibuni ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku kumshambulia Mkapa kuwa alipageuza Ikulu kuwa pango la walanguzi, inamgusa pia Rais Kikwete ambaye alikuwa mmoja wa mawaziri waandamizi katika Serikali ya Awamu ya Tatu.

Butiku katika kauli yake hivi karibuni kwa waandishi wa habari alikaririwa akidai kwamba, Mkapa aliruhusu Ikulu kuwa mahali ya walanguzi na wanyang’anyi na alimtaka ajitokeze kueleza namna yeye mwenyewe alivyogeuza eneo hilo takatifu kuwa mahali pa walanguzi.

Wachambuzi wa mambo wameeleza kuwa hatua ya Butiku kuibuka na kumshambulia Mkapa hadharani huku akimtaka ajitokeza kujibu mashambulizi yake ni majibu ya kambi ya upinzani ndani ya CCM kwa tabaka la wana CCM walio madarakani ambao ushindi wao ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na siasa za ubaguzi na kuchafuana majina.

Shutuma zilizotolewa na Butiku ambaye wakati wa kampeni za kumpata mgombea urais kupitia CCM mwaka 2005 hakuwa katika kambi ya Kikwete, anasema kwamba Mkapa akiwa Mwenyekiti wa CCM, aliamua kumuengua mapema makamu wake, John Malecela, asisonge mbele katika mchakato wa kugombea kuteuliwa kuwa mgombea kupitia chama hicho.

Kwamba Mkapa alibadili kanuni kwa shinikizo na bila sababu yoyote ya msingi, ambayo awali ilijadiliwa kuwa isibadilishwe, ya mjumbe mmoja kura tatu.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanadai zaidi kwamba, Mkapa alibadili kanuni hiyo kwa shinikizo ili kuhakikisha Rais Kikwete anashinda na kuwa mgombea wa CCM, na kwamba, anachokifanya Kikwete kwa sasa ni kulipa fadhila kutokana na ujasiri unaodaiwa kuonyeshwa na Mkapa wa kuhakikisha kijana wake anashinda katika mchakato huo.

Butiku anayetajwa na wafuatiliaji wa masuala ya siasa kuwa anatumiwa kama chambo na wapinzani wa wanamtandao ndani ya CCM, anamtaja Mkapa kama mtu msahaulifu, ambaye wakati akiwa Ikulu, alisahau yote aliyofundishwa na Mwalimu Nyerere, akashindwa kutofautisha uongozi na kutafuta mali na kwamba wakati anatoka katika uongozi alitafuta mtu wa kumbeba na kumpeleka Ikulu.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitivo cha Sayansi ya Jamii (FASS) aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la jina lake kuhifadhiwa, ameitafsiri kauli ya Butiku kuwa moja ya matamshi mazito yanayolenga kuichafua kabisa serikali ya Kikwete kuwa iliwekwa madarakani na Mkapa kwa ajili ya kumlinda yeye na baadhi ya wenzake.

“Hii ni kauli nzito sana, inamaanisha kuwa Kikwete aliwekwa pale kwa dhumuni maalumu la kumlinda Mkapa dhidi ya madhambi aliyoyafanya wakati akiwa madarakani, kauli hizi zitamtesa sana Rais Kikwete kwa sababu zinaichafua kabisa serikali yake, hivi ndivyo ninavyoweza kuitafasiri kauli hii,” alisema mhadhiri huyo.

Kauli nyingine ya Butiku inayoonyesha kuwepo walakini katika mchakato huo inaeleza kuwa, wakiwa Dodoma kwenye uchaguzi wa kumpata mgombea wa urais kupitia CCM kulikuwa na mgombea mmoja anayedaiwa alikuwa akigawa fedha hadharani na kwamba alikuwa akiwajaza wajumbe wa mkutano huo kiasi kikubwa cha fedha.

Kwamba baada ya kusikia maneno hayo ndipo alipoondoka kwenda kumwandikia Mkapa barua ambayo hata hivyo mpaka anaondoka madarakani hakuwahi kuifanyia kazi.

Hili nalo linaelezwa kuwa ni hatua ya Mkapa kuhakikisha kuwa Kikwete anashinda katika uchaguzi huo licha ya baadhi ya wapambe wake kudaiwa kutoa fedha.

Kikwete ambaye amekwisha kutangaza kuwa kamwe hatamchunguza Mkapa dhidi ya tuhuma zinazomwandama, sasa analazimika kujiandaa kutoa ufafanuzi kwa wapiga kura dhidi ya kashfa mbali zinazoindamana Serikali ya Awamu ya Tatu, ikiwemo ile ya rada na madai ya Mkapa kufanya biashara akiwa Ikulu.

Kikwete pia anapaswa kuanza kujipanga upya kupambana na makundi ndani ya chama chake ambapo baadhi ya vigogo aliowaangusha katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2005, akiwemo Malecela wanaonekana kutofautiana na msimamo wake katika kupambana na ufisadi ndani ya serikali yake.

Kauli za kumbana Kikwete zimeibuka baada ya viongozi wa kambi ya upinzani kutaja orodha ya majina ya viongozi wanaodai kuwa wanahusika na vitendo vya rushwa na ufisadi.

Kundi la wana CCM walio nje ya mtandao wanaonekana kunufaika zaidi na madai haya ya wapinzani ambayo kwa kiasi kikubwa yameiweka serikali njia panda kwa kushindwa kutoa majibu ya moja kwa moja ya tuhuma hizo.

Aidha, maadhimisho ya miaka minane ya kifo cha Mwalimu Nyerere anayechukuliwa kuwa ni kielelezo cha uadilifu yametumiwa na wapinzani wa kundi la wanamtandao kuibua madai ya shutuma hizi huku wengine wakithubutu kueleza kuwa tuhuma za ufisadi zinazoiandama serikali ni mzimu wa Mwalimu Nyerere, ambaye wakati wa uhai wake aliwakataa katakata baadhi ya viongozi waliopo madarakani, akidai si waadilifu.

Source: Tanzania Daima
 
Mkapa amtesa Rais Kikwete

na Charles Mullinda
Tanzania Daima

Huu uchambuzi upo sahihi kwa kiasi kikubwa, swali ni kwamba baada ya yote haya kusemwa, JK atafanya nini ili kurudisha imani ya wananchi kwa serikali yake?
 
PM, Mkapa contribute 7.5m/- to fight hunger
2007-10-22 09:48:48
By Guardian Reporter

Prime Minister Edward Ngoyai Lowassa and former President Benjamin Mkapa are among prominent persons who contributed money during an anti-hunger fund-raiser that took place in Dar es Salaam over the weekend. Lowassa donated 5m/- while Mkapa gave 2.5/-.

Speaking during the function, the chairman of Telefood Tanzania, Franco Tramontano, said the society needed more funds to curb hunger.

`Telefood Tanzania has funded a number of groups to enable them to establish projects that would get rid of hunger and reduce poverty levels. I call upon the assisted groups to employ jobless people as the only way to create quality life for all citizens,` said Tramontano.

He said Telefood Tanzania endeavoured to help the society overcome hunger and poverty.

For his part, a representative of the Food and Agriculture Organization, James Yonazi, said that Telefood endeavoured to solicit funds from donors and help poverty ridden areas.

Speaking at the same venue, the Head of Vodacom Foundation, Rachel Phares, said Vodacom had been contributing to the fight against hunger.

She said Vodacom would maintain its commitment to support community services such as education, health and agriculture.

The fundraising event was jointly organized by the Equal Opportunity Trust Fund, Telefood Tanzania and Vodacom Tanzania Limited.

SOURCE: Guardian
 
Mkapa alikuwapo au pesa ilitolewa na mama Anna Mkapa,sitaki kuamini kama mkapa alikaa meza moja na EL..muda wa saa 7 atakuwa akikabidhiwa tuzo yake.
 
Utaonea tu..... ya ni maneno ya kipanya kwa mjasiliamali

angalia kiambatanisho
 
Attachments

  • Utaongea tu.........JPG
    Utaongea tu.........JPG
    16.8 KB · Views: 30
Mkapa: Ukimya haufuti aibu uliyojipandia

Chris Alan: Tanzania Daima

NILISOMA kwa mshangao kauli ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa kwamba hatakubali kuburuzwa kwenye malumbano ya kisiasa kwa sababu amekwisha kustaafu!

Kauli hii ilikuwa ikijibu mfululizo wa tuhuma zilizoelekezwa kwake kwa takriban miezi mitano sasa, juu ya kuhusika kwake na uvunjaji wa sheria na kanuni wakati akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni mengi aliyotuhumiwa nayo Rais mstaafu Mkapa.

Kwa ufupi tu tuhuma hizi ni pamoja na kujihusisha na biashara wakati akiwa Ikulu; kutumia Ikulu kwa maslahi binafsi hali ambayo ni kinyume cha kiapo cha urais; akiwa Rais kujipatia mikopo kutoka benki bila hata kufuata taratibu za kibenki; kushirikiana na waziri wake wa Nishati na Madini kununua kampuni ya umma ya kuchimba mkaa wa mawe na kutengeneza nishati ya umeme; kujipanga pamoja na wafanyabiashara wenye mawaa kuendesha shughuli za kibiashara akiwa bado Ikulu.

Madai haya yametolewa na vielelezo kadhaa kuanikwa hadharani jinsi Rais Mkapa alivyokiuka miiko ya urais kwa kujifanya mjasiliamali akiwa Ikulu.

Kauli ya Rais Mkapa hivi karibuni kwamba "amekwisha kustaafu na hakuna njia ya kumfanya ajiunge kwenye malumbano ya kisiasa" ni kichekesho cha mwaka kwa sababu kinachoelezwa dhidi yake si malumbano ya kisiasa, ila ni tuhuma za ukiukaji wa maadili ya uongozi; ni tuhuma za kutumika vibaya madaraka yake, si malumbano ya kisiasa.

Wengi wanamfahamu Mkapa kama kiongozi aliyekuwa mbabe, asiyekuwa na subira, ilikuwa ni rahisi sana kwake kufoka, kukemea na hata kutumia lugha mbaya dhidi ya wale wenye msimamo tofauti na wa kwake.

Kwa maana hiyo kujitokeza safari hii na kudai kwamba amestaafu siasa hivyo hahitaji kubishana nao kuhusu tuhuma hizi ni kielelezo cha kukwama. Mkapa amekwama!

Kwanza amekwama kwa maana kwamba hana majibu ya tuhuma zinazomkabili. Hawezi kujisafisha dhidi ya tuhuma hizi kwa sababu yote anayohusishwa nayo ni ukweli na kweli tupu. Amethibitika kujitafutia ukwasi kwa kutumia hadhi ya urais kitu, kinachomwondolea ujasiri wa kuweza kusimama hadharani na kudai kwamba yeye ni msafi, kwa njia hiyo ameamua kujifunika na kukaa kimya, akitumia mbinu dhaifu kwamba eti madai haya yote ni malumbano ya kisiasa ambayo hatayajibu kwa sababu amestaafu.

Pili, kudai kwamba tuhuma dhidi yake ni malumbano ya kisiasa, Mkapa ameamua kupotosha ukweli na dhana nzima ya uadilifu katika uongozi wa nchi.

Ameamua kutumia propaganda kugeuza tuhuma za uvunjaji wa miiko ya uongozi na matumizi mabaya ya madaraka kuwa malumbano ya kisiasa. Hapa Mkapa anatuhumiwa kwa kuitumia Ikulu vibaya, anatuhumiwa kujitumbukiza kwenye biashara kwa kutumia jina la urais, yaani taasisi ya urais, kwa manufaa yake na wale wa nyumba yake; ametuhumiwa kuungana na waziri wake kujitwalia mali ya umma kinyemela, huu ni uporaji kama uporaji wa anina nyingine yoyote.

Kwa maneno yasiyovishwa nguo, Mkapa anastahili kuwekwa kizimbani kwa mambo aliyoyafanya akiwa madarakani, yapo mengi machafu ambayo Watanzania wangefarijika kuona kwamba majibu yake yanapatikana kwa njia ya mkondo wa sheria. Inawezekana kwamba Rais kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania hatashitakiwa kwa mambo ambayo alitenda akiwa madarakani, lakini hili linahitaji tafsiri na mjadala mpana, haya mambo ni yapi?

Je, ni halali kusema kwamba Rais aliyeendesha uchuuzi Ikulu alikuwa akitekeleza kazi za urais? Au Rais aliyetumia Ikulu au taasisi ya urais kwa manufaa yake binafsi na wale wa nyumbani kwake, nayo ni utekelezaji wa kazi za urais?

Sawa. Mkapa anaweza kuwa ameamua kuweka mdomo wake kufuli, na kweli anaweza asiseme lolote walau kwa sasa, lakini jambo moja ni lazima alijue kwamba sasa ameabishwa mno, ameanikwa, amevuliwa nguo anastahili kuchutama ili kujisetiri kutokana na aibu inayomkabili.

Tunamkumbuka Mkapa kama Rais aliyeishi kibabe na kufanya mambo mengi kibabe hasa yale yaliyogusa ukosoaji wa utawala wake. Alifanya hivyo kwa sababu alikuwa na dola na kwa sababu pia hulka yake ndivyo ilivyo. Lakini kwa sasa hana tena dola, hana tena nguvu za kutisha watu ndiyo maana ameamua kubadili mwelekeo wa maisha yake kuwa ya kinyenyekevu kama njia ya kujilinda na kutafuta huruma.

Kwamba Mkapa sasa anataka aonewe huruma kwa kukaa kimya kana kwamba tuhuma hizi zinazoelekezwa kwake ni za chuki na uzushi. Anasaka huruma asiyostahili. Anasaka huruma hii kwa kugeuza tuhuma za ukiukaji wa maadili ya uongozi kuwa malumbano ya siasa ambayo hawezi kuingia kwa sababu amestaafu.

Pamoja na mbinu hizi za kubadili tuhuma dhidi yake kuwa malumbano ya kisiasa, ingawa hata hivyo hajafaulu, kitu kimoja kipo wazi kwamba Mkapa tunayemjua sisi anaumia ndani kwa ndani, ana hasira; kifua kimemjaa; shikikizo limemjaa kifuani na angependa kuwashughulikia wale wote wanaomwanika kiasi hiki, kwa bahati mbaya hana ubavu huo kwa sasa. Hawezi kuamrisha yeyote sasa.

Hata kama anakataa kujibu tuhuma hizi, na hata kama haitakuwa rahisi kumshitaki, ukweli ni kwamba hadhi na staha ya Mkapa imeshuka, imeporomoka na kufikia kiwango cha chini ikilinganishwa na hapo kabla ya habari ya matendo yake machafu kuwekwa wazi.

Katika jamii inayoheshimu miiko na maadili, pia uungwana hutawala jinsi watu wanavyofanya mambo yao. Tanzania kwa kiasi fulani ni taifa linalopambana kujenga maadili ya utawala na jamii inakumbushwa wakati wote kuishi kwa miiko, kuzingatia sheria na taratibu. Ukivunja miiko kuna njia mbili za kuadhibiwa. Moja, waweza kufikishwa kwenye vyombo vya sheria na kuadhibiwa.

Pili, jamii yaweza kukuadhibu kwa kukuzomea. Kwa kimombo huitwa ‘mobilise shame' kwa Mkapa hata kama atakataa kujibu tuhuma hizi na hata kama mwisho wa yote haitawezekana kumshitaki kortini, lakini ni ukweli usiokuwa na shaka yoyote kwamba imewezekana ‘kumobilise shame' dhidi ya Mkapa.

Hata kama Mkapa atajitahidi kiasi gani kujificha na kukwepa kujibu tuhuma hizi kwa kuzigeuza kuwa malumbano ya kisiasa; na hata kama atajitahidi kiasi gani kutafuta huruma ya umma dhidi ya tuhuma zake, ukweli unabakia kuwa mmoja, hadhi yake haiwezi kuwa ile ile, amefichuliwa kuwa ni mtu tofauti kabisa na misimamo yake aliyohubiri ya uwazi na ukweli. Hakuwa muwazi wala mkweli kwa mambo mengi akiwa Ikulu.

Ndiyo maana binafsi ningependa kumpa Mkapa salamu hizi, kwamba hata kama akijifukia ardhini na kuweka mdomo wake kufuli kubwa la Viro hawezi kuwa yule yule, amefunuliwa na yu na uchafu mwingi, dawa si kunyamaza kwa sababu uchafu hautoki kwa kunyamaza. Imewezekana kumobilise shame dhidi ya Mkapa kwa hiyo kujificha kwake hakutamsafisha.

Ninaamini hata kushindwa kwa Mkapa kupata tuzo ya Mo Ibrahim iliyokwenda kwa Rais mstaafu wa Msumbiji, Joaquim Chissano, pamoja na kwamba Tanzania ni nchi isiyo na mfano wa kukaribiwa kwa amani na utulivu katika Afrika, jinsi alivyoboronga katika njanja za kidemokrasia na uadilifu vimempora tuzo hiyo muhimu.

Ni bahati nzuri kwamba waliomwanika Mkapa ni magazeti ya Tanzania, ingekuwa ni ya Kenya au nchi nyingine yoyote ya Afrika au nje ya bara hili, ingeelezwa kwamba yametumiwa. Kwa hili, tuna kila sababu ya kujipongeza kwamba ni lazima viongozi wa aina ya Mkapa wajue kwamba hata kama katiba za mataifa yao zitakuwa zinawalinda dhidi ya mashitaka yoyote dhidi yao wakati wakiwa madarakani, umma una uwezo wa kumobilise shame dhidi yao.

Email:chrischrisalan@yahoo.com
 
Mngesema baada ya JK kuteuliwa tungeliwaelewa;hata mzee Bomani aliahidiwa U-PM na Mwinyi 1990 lakini hawa akina Mohamed Seif wakainyaka nyeti hiyo na kumpeleka kijana Mabiti akafanye balaa kule Mwanza,mzee Bomani akaumia hakulalama mpaka ameenda kaburini ,Butiku Ukuu wa Mkoa tu ulikutoa jasho itakuwa u-PM?

Mkapa aliwapa watanzania kipenzi chao,haijalishi ana uwezo au la; na ndio maana ya historia.Usibishane na nguvu za wakati mzee Butiku na wenzio,sasa tumechoka kusikia Mkapa,Mkapa,Mkapa na jana Channel Ten tumekuona ukishangilia Mkapa kukosa tuzo ya Mo Ibrahim,mind u hakuomba ila wao walimuona anafaa kufikiriwa;ila kauli yako ya kusema eti kukosa kwake ni kutokana na udhaifu na shutuma ,umetufadhaisha sana WTZ wengi na sasa tunakuona kuwa si Mwalimu aliyeuleta umaskini nchini bali watu wa aina yako mabingwa kujipendekeza na uoga ukiwa damuni,hamkuwa wakweli kwake ,majitu mnamtaka mzee yule ateue hata mkurugenzi wa kampuni ya kuoka mikate ailimuradi mkipita huko muitwe wazee!!!
Shame on u Butiku na wote wenye mtizamo hasi
 
For this person who calls himself FDR Jr.....You are a senior member here at JF but you seem to have forgotten the real purpose of JF. We are here to call a 'spade' for what it is.... a spade!

We do not need your propagandas here on Mkapa...I know, you know (although you pretend not to), and all Tanzanians know what Mkapa has done. It's true that he's done SOME stuff that's expected of all presidents...and that is to do the right things for his people. But then, I guess he changed his mind in the whole mission and decided to do the right things for himself and his family....and that is to steal from us, Tanzanians.

President(s) have all the power, and it is expected of any president to use the power entrusted to him/her by his/her people for the betterment of his/her people and country! To the contrary, Mkapa did did the opposite of this!

Instead he used his power and influence to acquire more power, money, properties and anything else he and his wife can think of because of greed!

I tell you this, we Tanzanians are very peaceful people. We are so peaceful and powerless that this crook even has the nerve to state that... "amekwisha kustaafu na hakuna njia ya kumfanya ajiunge kwenye malumbano ya kisiasa"... He should know that these are not mere allegations, these are serious charges against his conduct while in office! He should be investigated and if evidence is found of his misconduct, then he should be prosecuted BY LAW!

Jamani hivi sie wa-Tanzania tutazubaa hivi mpaka lini? There has to be a starting point, a safe haven for all of us, please let us make JF that safe haven! Thank you.
 
Watu bwana!
Bado haijanikaa akilini mwangu! Yaani Dua ya kumwombea BWM akose tuzo kama Mtanzania- ila upendo na uvumilivi na kusameheana kama nguzo za uzalendo wetu ndo vinaanza kumomonyoka?
Hiki cha kumwombea dua mbaya Mtanzania akose tuzo (for whatever reasons!) ni kitendawili kwangu!
 
Wenzako tumeshakitegua kitendawili hicho, labda nawe ipo siku utafanikiwa kukitegua.
 
Watu bwana!
Bado haijanikaa akilini mwangu! Yaani Dua ya kumwombea BWM akose tuzo kama Mtanzania- ila upendo na uvumilivi na kusameheana kama nguzo za uzalendo wetu ndo vinaanza kumomonyoka?
Hiki cha kumwombea dua mbaya Mtanzania akose tuzo (for whatever reasons!) ni kitendawili kwangu!

Hilo swali lako linaweza jibiwa kwa uhakika na hao wana kamati walioamua kuwa hafai kupata tuzo hiyo
 
Mngesema baada ya JK kuteuliwa tungeliwaelewa;hata mzee Bomani aliahidiwa U-PM na Mwinyi 1990 lakini hawa akina Mohamed Seif wakainyaka nyeti hiyo na kumpeleka kijana Mabiti akafanye balaa kule Mwanza,mzee Bomani akaumia hakulalama mpaka ameenda kaburini ,Butiku Ukuu wa Mkoa tu ulikutoa jasho itakuwa u-PM?

Mkapa aliwapa watanzania kipenzi chao,haijalishi ana uwezo au la; na ndio maana ya historia.Usibishane na nguvu za wakati mzee Butiku na wenzio,sasa tumechoka kusikia Mkapa,Mkapa,Mkapa na jana Channel Ten tumekuona ukishangilia Mkapa kukosa tuzo ya Mo Ibrahim,mind u hakuomba ila wao walimuona anafaa kufikiriwa;ila kauli yako ya kusema eti kukosa kwake ni kutokana na udhaifu na shutuma ,umetufadhaisha sana WTZ wengi na sasa tunakuona kuwa si Mwalimu aliyeuleta umaskini nchini bali watu wa aina yako mabingwa kujipendekeza na uoga ukiwa damuni,hamkuwa wakweli kwake ,majitu mnamtaka mzee yule ateue hata mkurugenzi wa kampuni ya kuoka mikate ailimuradi mkipita huko muitwe wazee!!!
Shame on u Butiku na wote wenye mtizamo hasi

.....ZUMBUKUKU WEWE FDR! Wewe na mtu yeyote yule anayedhani kwamba kumkemea Mkapa na mifisadi mingine katika nchi yetu ni makosa. Mkapa alichaguliwa kuwa rais wa TZ na alitakiwa ku-fullfill duty zake kama rais and for that we were going to honor him and respect him. Lakini badala ya kufanya yale aliyoapa kutufanyia, i.e. kutuongoza kizalendo na kwa uadilifu, yeye aliendesha biashara na kufanya uporaji and for that we are going to condemn him and hate him till the end of his days. Huyu jamaa will go down in history as the worst president Tanzania ever had and someday in the future, his estate or his grandchildren will be prosecuted in much the same way as Hitler's or Mussolini's seeds are being prosecuted in the world.
 
mzalendohalisi ( na wengine mnaoingia kwenye gurupu lake)

mkapa lazima aombewe kukosa hiyo tuzo kwa sababu hastahiki, angelikuwa yeye ni kiongozi msafi, na aliyekaa madarakani kwa faida ya wananchi wake, angejitokeza kujibu tuhuma anazoelemeshewa kuhakikisha kuwa yeye hana makosa na wanaomuita fisadi ndio wakosa.

kwa kushindw kufanya hivyo, kunamuona yeye moja kwa moja ni jeuri, asiependa watu wake, na asiejali wananchi wake wanamtazama kwa jicho gani.

na kama ni hivyo, tunzo ya Ibrahim Mo ya nini? wkati tunzo hiyo ni kwa kiongozi mwenye sifa ambazo yeye hana.

asanteni waratibu wa Ibrahim Mo award kwa kutompatia mkapa zawadi hiyo
 
.....ZUMBUKUKU WEWE FDR! Wewe na mtu yeyote yule anayedhani kwamba kumkemea Mkapa na mifisadi mingine katika nchi yetu ni makosa. Mkapa alichaguliwa kuwa rais wa TZ na alitakiwa ku-fullfill duty zake kama rais and for that we were going to honor him and respect him. Lakini badala ya kufanya yale aliyoapa kutufanyia, i.e. kutuongoza kizalendo na kwa uadilifu, yeye aliendesha biashara na kufanya uporaji and for that we are going to condemn him and hate him till the end of his days. Huyu jamaa will go down in history as the worst president Tanzania ever had and someday in the future, his estate or his grandchildren will be prosecuted in much the same way as Hitler's or Mussolini's seeds are being prosecuted in the world.

Jazba za nini????!!!!!Tushakuwa zumbukuku tena ,nini kosa langu??? Au ni dhambi kutofautiana misimamo?? !!
Kazi kwelikweli
 
Litafuteni gazeti la baraza la jana pengine tutaona kuna umuhimu wa kutofautiana ili tuendelee.
Tanzania ,nakupenda kwa moyo wote
 
Jazba za nini????!!!!!Tushakuwa zumbukuku tena ,nini kosa langu??? Au ni dhambi kutofautiana misimamo?? !!
Kazi kwelikweli

FDR Jr. my apologies for the name calling. And as you said, we should strive to differ in our opinions, ingawa wengine tunaona mna dalili za kushabikia ufisadi and at the same time condemning Butiku and anyone who dares to speak up against ufisadi - like ME.
 
Makani apania kumburuta Mkapa kortini

*Adai Rais huyo mstaafu amekosa kinga
*Asema kifungu cha Katiba kinapotoshwa

Na Suleiman Abeid, Shinyanga

SAKATA la tuhuma za ufisadi wa baadhi ya viongozi nchini limechukua sura mpya baada ya mmoja wa wanachama wakongwe wa CHADEMA, Bw. Bob Makani, kutangaza kusudio lake la kumfikisha mahakamani Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa.

Mwana CHADEMA huyo ambaye ni mjumbe wa kudumu katika kamati ya utendaji ya Taifa ya chama hicho, alitangaza kusudio hilo juzi alipokuwa akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Shinyanga katika viwanja vya shule ya msingi Jomu.

Bw. Makani alisema baadhi ya watu wamekuwa wakikitafsiri vibaya kifungu cha Katiba ya nchi kinachozungumzia kinga ya kushitakiwa kwa Rais mstaafu na kusema kuwa kifungu hicho hakitoi kinga kwa makosa binafsi, yaliyotendwa na Rais mstaafu.

Alisema hali hiyo ndiyo imesababisha Rais aliye madarakani hivi sasa aogope kumshughulikia Bw. Mkapa, kwa madai kuwa anafahamu wazi kuwa kuna mambo aliyoyatenda ambayo hayaruhusiwi kufanywa na Rais akiwa Ikulu.

Alisema ibara ya 46 ya Katiba ya nchi inasema Rais hawezi kushitakiwa kwa makosa aliyoyafanya akiwa Rais, ambapo Rais Jakaya Kikwete anatumia mwanya huo wa kutomshitaki Bw. Mkapa kwa vile alikuwa Rais.

“CHADEMA inasema, tafsiri yetu ni kwamba ibara hiyo inamlinda tu Rais kwa mambo aliyoyafanya akiwa Rais...apelekwe mahakamani akashitakiwe, na kama hawana wa kumshitaki, mimi najitolea nitakwenda kumshitaki,” alieleza Bw. Makani.

Aidha Bw. Makani alimwomba Rais Kikwete avunje Baraza la Mawaziri na kuliunda upya akiwaacha wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Alisema hali ya vitendo vya ufisadi na rushwa nchini imesababisha wananchi kuwa na hali ngumu kimaisha ambapo tofauti ya mapato kati ya maskini na tajiri imekuwa kubwa zaidi.

Alisema wakati kundi kubwa la wananchi wenye kipato cha chini wanapata matatizo ya maisha, wapo watu wanakula chakula kwa mrija na kwamba nchi hivi sasa inaelekea pabaya.

Kwa upande mwingine, Bw. Makani alisema hali ya mambo ndani ya CCM hivi sasa si nzuri na kwamba chama hicho kinaelekea kusambaratika.

Aliwataka wana CCM ambao wanaona mbali kuanza kujitoa ndani ya chama hicho kabla hakijasambaratika na kutoa mfano wa Dola ya Warumi, ambayo ilisifika kwa ukali, lakini ilifikia sehemu ikasambaratika.

“CCM inasambaratika, kama kuna mtu wa CCM hapa namwomba ahame kabla haijasambaratika, Dola ya Warumi ilikuwa kali lakini ilisambaratika, itakuwa CCM? Sasa hivi imegawanyika na imebinafisishwa," alisema Bw. Makani.

"Sasa hivi ukitaka kuwa kiongozi ndani ya CCM lazima uwe tajiri, nafasi zinapatikana kwa zabuni, kama unazo fedha utashinda na kama huna kwa heri,” alieleza Bw. Makani.

Alisema hata muasisi wa CCM marehemu Mwalimu Nyerere akifufuka leo, hawezi akajiunga na chama hicho tena na kwamba anaamini atajiunga na CHADEMA.

Source: Majira
 
SAKATA la tuhuma za ufisadi wa baadhi ya viongozi nchini limechukua sura mpya baada ya mmoja wa wanachama wakongwe wa CHADEMA, Bw. Bob Makani, kutangaza kusudio lake la kumfikisha mahakamani Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa.

Patamu hapo...ninatumai hatokimbilia (Mkapa) South Africa kutibiwa.
 
Back
Top Bottom