Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

NDOTO za baadhi ya Watanzania za kutaka Bunge la Jamhuri ya Muungano limuondolee kinga Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ili aweze kushtakiwa kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka yake na kujihusisha na biashara akiwa Ikulu inazidi kuingia wingu zito baada ya baadhi ya wanasiasa kuweka bayana kuwa jukumu hilo ni la wananchi.
Hivi ni kwanini viongozi wetu watuone watanzania hamnazo kiasi hiki? Hapa hawajui kuwa wananchi na rais si personal issues,ni mkataba wa kisheria kuwa tukikuchagua unafanya haya na haya kwa mujibu wa katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,na kama kuna sheria zilizovunjwa basi haki inatendeka na si kurudisha issue muhimu za Taifa letu kwenye siasa na kutufanya wote wajinga.

Hapa sheria ichukue mkondo wake kama Rais mstaafu alizivunja na mwananchi wala hana haja ya kuulizwa hilo,hatuwezi kusem eti wananchi waamue,wananchi walishaamua na yeye akafanya tofauti,sidhani kama wananchi wangemchagua kama wangejua kuwa atafanya hayo madudu aliyoyafanya,na kwasababu wananchi walimwamini na kumchagua na kuwekeana naye mkataba chini ya kiapo kwa kutumia katiba ya nchi na mojawapo ya vitabu vitakatifu,na kwamba ulinzi wa mali za Taifa ikiwa ni mojawapo ya majukumu hayo yaliyopo chini ya mkataba,huwezi kudai eti wananchi ndiyo wenye maamuzi tena,hapa ni sheria na haki needs to take place.

Superman,inaelekea huna huruma na wananchi kabisa,matabaka ni shida kubwa sana tuliyonayo bongo na inayokomaa kwa kasi na pia empathy wengi wetu hatuna,na hata kama tunayo,basi ni based on hayo matabaka,shangaa unamwonea huruma Mkapa na mimi nawaonea huruma watanzania masikini. Tunaposema "Kupumzika" kabla hatujarosolve issues na concerns za wananchi kuhusiana na wizi wa mali zao chini ya mikataba ya ulinzi na uendelezaji wake kwa manufaa ya wote,tutakuwa tumewakosea haki na ni sawa na kudumaza demokrasia,mendeleo na uwezo wa kufikiri wa wananchi walio wengi wenye mahitaji muhimu ambayo ni haki yao lakini yamegeuzwa kama mitaji ya kuwapora haki zao za kimsingi na hivyo kubakia kama watumwa....Inasikitisha saaana!

Na wanachofanya wanasiasa hao ni kuendelea kuzitumia fedha walizoiba kuwalaghai wananchi kwa kuwatumia viongozi wengine waliochaguliwa na wananchi hao,tatizo ni kwamba wanapalilia Tanzania ambayo inaweza kukosa amani.

Nawaeleza kabisa viongozi hao kuwa dunia imebadilika na wasidhani watafunika kombe tu,it won't work like that,mambo yatakuja kubadilika siku moja na watu watajitolea kupigania uhuru upya,je wanataka hilo?

ccm ilijipatia umaarufu kwasababu ya harakati za uhuru,hilo litapita,ndio historia hiyo tunatakiwa tujifunze ili Taifa lisipitie huko,only if its neccessary....Mataifa makubwa tu kama USA walipigania Uhuru na baadaye wakaanza kuzichapa wao kwa wao,na migogoro kedekede,sisi tuna historia yetu na si lazima tupitie kama yao,lakini ukweli ni kwamba you can not full all the people all the time even if its true that you can fool some of them sometimes...

Kuna watanzania ambao hawatakubali kuona wanao na wajukuu zao wakiwa na potential ya kuwa watumwa ama masikini wa kutupwa kwenye Taifa lao, kama mnafahamu hilo ndugu viongozi,basi ni budi muwe makini.
 
Muacheni Ben, aliteleza kidogo kipindi chake cha pili lakini atakumbukwa kwa utekelezaji wa uimarishaji wa serikali yake na ukusanyaji wa kodi,kuimarisha TANROADS na ujenzi wa mabarabara
 
Juzi tu alikuwa na Rais Kikwete Mwanza na huko akamwagiwa sifa kibao yeye na Lowassa. Mambo ya Mkapa kushitakiwa sahauni labda awamu ijayo. Lakini hata wakati huo yatakuwa yanashughulikiwa ya JK na wala si yake tena kwani yatakuwa tayari yamefunikwa.
 
Muacheni Ben, aliteleza kidogo kipindi chake cha pili lakini atakumbukwa kwa utekelezaji wa uimarishaji wa serikali yake na ukusanyaji wa kodi,kuimarisha TANROADS na ujenzi wa mabarabara
Mkuu salam:
Huku kuteleza kimdundiko mkuu badala ya kuinuka na KIDUDE unaibuka na MABILIONI HIYO NI KI MKAPA MKAPA na kwa mazuri aliyofanya alilipwa hakuwa anajitolea, nyumba dezo na marupurupu kibaooo!! Sasa watu wenye TAMAA kama hawa kwao ni Lupango tu, ni afadhali ya mwizi wa mfukoni wa Kariakoo anaweza kudai kuwa anaibia njaa, sasa huyu BENJAMINI atasingizia nini???
 
Juzi tu alikuwa na Rais Kikwete Mwanza na huko akamwagiwa sifa kibao yeye na Lowassa. Mambo ya Mkapa kushitakiwa sahauni labda awamu ijayo. Lakini hata wakati huo yatakuwa yanashughulikiwa ya JK na wala si yake tena kwani yatakuwa tayari yamefunikwa.

Mkuu utayafunika mambo lakini huwezi kufunika reality!

Kama Mkapa angewaachia wananchi maisha bora hata pamoja na wizi wote huo unadhani angekuwa na pressure kubwa kiasi hiki?

Kama wananchi wataendelea kuteseka na yeye na wenzake wote uliowataja wanaendelea kumiliki mali za Taifa unadhani nini kitafunika? Cheap politics,kangas kandambili pilau etc? Hayo yana mwisho kwani mahitaji ya mwandamu hayabaki the same everytime and certainly every generations.

Mkuu don't be that delusional,reality decides,its the facts nothing else,kama wananchi wataendelea kuumizwa kutokana na ufisadi,especially inavyoonekana sasa na jinsi ambavyo balaa hilo litawakumba pia si tu kizazi hiki bali pia kijacho,then mkuu you must be having some wishful thinking, ni bora ushauri wa walio wengi wazalendo ukazingatiwa ili kuepusha migogoro ama hata mapigano yanayoweza kuepukika.

Na kwa ajili hiyo namwomba Mh Rais aache kuwapumbaza watanzania kwa pesa za misaada huku mali za Taifa zikiporwa,thats more than insanity.
 
Duh !!! ama kweli maji hayapandi Mlima

Hahahaha, kweli mkuu!

....Iwapo Rostam anamiliki magazeti mengi nchini hapa utategemea habari gani zaidi?

Ajabu hawa hawa leo hii wanarudi tena na mbinu mpya...

Duh, tangu 2006 uliandika haya!

Sitatumia cheo wala ofisi ya umma kwa maslahi yangu binafsi...hivi hii ni ahadi ya ngapi?
🙂
Samahani sana jamani; habari hizi ziliniboa sana nilipozisoma jana usiku kiasi kuwa baadhi ya majibu yangu huko nyuma hayakuwa controlled. Samahani sana kwa wasomaji wote kutokana na majibu yangu mabaya ya huko nyuma.

Kuhusu Mkapa kujijengea utajiri siyo kwenye nyumba hii moja tu, kumekuwa na taarifa za kuwapo majumba mbalimbali aliyojipatia akiwa madarakani au baada ya kutoka madarakani. Kuna taarifa za jumba la kifahari huko Afrika ya Kusini, jumba jingine huko Washington au New York, jumba jingine kule Lushoto, na majumba kadhaa hapo Dar es Salaam. Kwa kiwango chochote kile huo ni utajiri.

Kibovu ni kuwa serikali yake ilijenga misingi mizito ya rushwa kiasi kuwa imekuwa ni kansa kwa nchi sasa hivi. Ingawa rushwa ilikuwapo nchini kabla yake, yeye alii-institutionalize na kuifanya iwe kubwa sana na ngumu kuong'olewa hasa kwa vile yeye mwenyewe alihusika nayo moja kwa moja. Serikali yake iliingia mikataba mbali mbali kwa rushwa ambayo ilikuwa ni mzigo kwa nchi nzima. Mikataba ya namna hiyo na madhara yake yanajulikana kinaganaga na sina haja ya kuitaja tena.

Sijui niseme nini ila ingawa Mkapa alifanya mambo kadhaa mazuri kiuchumi, alijenga msingi mbaya sana wa rushwa na yeye binafsi alijihuisha na rushwa kwa kiwango kikubwa kiasi kuwa mazuri yake yote yanafutika.

THISDAY la leo limeandika DOING BUSSINESS FROM IKULU, likiwa na picha kubwa ya Mkapa na Anna na nyuma yao jengo la IKULU, wameandika kuwa kampuni yake iitwayo ANBEM limited ilianzishwa 1999 akiwa Ikulu na alijiita MJASIRIAMALI, na alikopa sh milioni 750/- lakini bahati mbaya leo hadi sasa halipo katika web. Sijui wamelihujumu? TUNAFUATILIA mwenye kupata habari kamili atutumie humu

...Mkapa ana kesi ya kujibu:

1. Hiyo kampuni ilikua ikiendesha shughuli zake katika majengo ya EOTF, mali ya serikali bila kulipa kodi ya pango wala bili ya umeme, mai na hata watumishi na samani za serikali
2. Hiyo kampuni ilipewa pesa (ilizoita mkopo) hata kabla ya kuwa na hati ya nyumba na hivyo kupata fedha za kununulia nyumba
3. Waliopo ndani kabisa ya mfumo wanasema hata fedha zilizotolewa kama mkopo ni mazingaombwe kwani zilikua ni ahsante kwa kufanikisha upatikanaji wa NBC, lakini pia kuna ushahidi wa maandishi kwamba uongoozi wa NBC ulikua ukiipa kampuni ya Ben fedha bila maelezo
4. Mkapa na mkewe walidanganya (kinyume cha sheria ya makampuni) kwamba wao ni Wajasiriamali na baadaye kujiita wakurugenzi hata kabla ya kampuni kusajiliwa. Hilo ni kosa la jinai

5. matumizi mabaya ya madaraka kisheria ni rushwa chini ya sheria ya Kuzuia rushwa. Kosa lingine la jinai

Wananchi wafahamishwe ili waweze kuchukua hatua kama walivyofanya wenzao wa Zambia

Leo nimeishia hapa katika kuwakumbushia tulikotoka... Am still reviewing this topic, imepelekea Mwanakijiji kupungua posts kama 3 kufikia 15k!
 
Hoja ya Mkapa kutikisa Bunge

*Kamati yawasukumia wabunge Dodoma
*Ni kuhusu umiliki mgodi wa Kiwira


Na Edmund Mihale

Majira
Thursday, 04 June 2009 07:40

HATMA ya tuhuma zinazomkabili Rais mstaafu wa Awamu ya tatu, Bw. Benjamini Mkapa kuhusu umiliki wa mgodi wa makaa ya mawe Kiwira,mkoani Mbeya itajulikana katika Mkutano wa 16 wa Bunge unaotarajiwa kuanza Jumanne ijayo mjini Dodoma.

Tuhuma hizo ambazo zimeelezwa kuwa moja ya hoja nzito zitakazoisumbua Wizara ya Nishati na Madini, ziliibuliwa na Mbunge wa Vunjo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Aloyce Kimaro katika Mkutano wa 11 wa Bunge.

Tangu kuibuliwa hoja hiyo, baadhi ya wabunge wamekuwa wakishinikiza kiongozi huyo kuondolewe kinga na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu mshitaka ya matumizi mabaya ya ofisi wakati akiwa madarakani.

Bw. Mkapa anatuhumiwa kuhusika na umiliki wa mgodi wa uchimbaji makaa ya mawe wa Kiwira kwa kutumia kampuni yake ya Tanpower huku akidaiwa kununua mgodi huo kwa 'bei poa'.Wengine wanaotuhumiwa sambamba na kiongozi huyo, ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini enzi ya utawala wake, Bw. Daniel Yona.

Bw. Yona hivi sasa anaandamwa na kashfa nyingine ya matumizi mabaya ya ofisi na kuliingizia Taifa hasara ya mabilioni, hatua iliyomfikisha mahakamani na kesi yake inaendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi ndogo za Bunge wakati akiwasilisha taarifa ya majukumu na utekelezaji wa shughuli za Wizara yake kwa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini ya Bunge jana, Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja alisema kutokana na unyeti wa suala hilo, wamekubaliana na Kamati hiyo kutozungumzia suala hilo katika vikao vya Kamati hiyo hadi litakapotinga na kujadiliwa Bungeni.

"Najua kuna swali kuhusu maradi wa makaa ya mawe wa Kiwira hapa sasa kabla halijaulizwa naomba niseme kabisa suala hili tumeamua kulizungumzia katika vikao vya Bunge lijalo hata waheshimiwa wajumbe wa Kamati pamoja na Mwenyekiti Kamati ya Nishati na Madini, Mheshimiwa Shelukindo, tumemwomba tuliingize suala hili katika vikao vya Bunge," alisema Bw. Ngeleja.

Mbali na hoja hiyo, wizara hiyo inatarajia kuwasilisha hoja ya rasimu ya marekebisho ya Sera ya madini ya mwaka 1997 iliyokamilika Novemba 2008 kwa kuzingatia mapendekezo ya kamati mbalimbali zilizoundwa kwa maagizo ya Serikali

Bw. Ngeleja alisema awali, rasimu hiyo iliwasilishwa kwa wadau Desemba 2 hadi 3 mwaka 2008 kwa kuwashirikisha wadau kutoka wizara, taasisi mbalimbali za Serikali wachimbaji wakubwa na wadogo, wabunge, washirika wa maendeleo, Sekretarieti ya Jumuia ya Madola, wataalamu kutoka vyuo vikuu, mashirika yasiyo ya kiserikali na vyombo vya habari.

Alisema Rasimu ya Sera ya Madini ya mwaka 2009 imeainisha maeneo ya kipaumbele ambayo yataongeza fungamanisho la sekta ya madini na sekta zingine za uchumi ili kuleta maendeleo endelevu na kuchangia pato la Taifa.

Alisema maeneo mengine ya sera ni kuongeza mazingira ya kiuchumi kuimalisha mfumo wa sheria kurekebisha mfumo wa kodi kuimalisha usimamizi wa sekta ya madini na ushiriki wa Serikali na Watanzania katika shughuli za madini

Aliyataja maeneo mengine kuwa ni kuboresha uchimbaji mdogo, malipo ya fidia ya ardhi kuhamasisha na kuendeleza uongezaji wa thamani ya madini na usimamzi wa mazingira afaya na usalama katika shughuli za madini.

Alisema Wizara yake imeendelea na mchakato wa marekebisho ya Sheria ya Madini ya mwaka 1998 kwa kukusanya maoni na ushauri wa awali kutoka kwa wadau.

Akizungumzia mkakati wa wizara yake katika mwaka 2008/09, alisema itaendelea kuwainua wachimbaji wadogo katika maeneo yao na kuwasaidia kupata mafunzo ili kuongeza maarifa, kuwapatia mikopo na mitaji,uongezaji thamani masoko na kurekebisha mfumo wa kodi, usimamizi na utaratibu za shughuli zao.

Katika mafaniko ya wizara hiyo, Bw Ngereja alisema imefanikiwa kufanya ukaguzi wa ubora wa kiasi cha dhahabu kilichozalishwa na kuuzwa nje ya na kampuni za madini za Geita, Bulyanhulu, Tulawaka Resolute na North Mara kwa lengo la kujua mapato yaliyopatikana na kiasi kilichostahili kulipwa kama mrabaha kwa Serikali.

Alisema ukaguzi huo umewezesha Serikali kuanza kulipwa kodi ya mapato kutoka katika kampuni ya dhahabu ya Geita kwa kiasi cha dola za Marekani 2,149,179.
 
Wakati kikao cha Bunge kikitegemea kuketi siku si nyingi kuna madai ya hoja fulani kuibuka. Mambo mengi ni yale yle yaliokua yaki semwa siku zote.

Ngoja tuone kama kuna la maana litatendeka au kama ni business as usual.
 
mimi binafsi namheshimu sana Rais mstaafu mheshimiwa Benjamini mkapa kwanza nikiwa kama mpenda michezo kwa uwanja wa kisasa aliotuachia pili katika suala zima la kutengeneza nguzo za kufuafua uchumi lakini huwa nikisikia na kusoma magazeti eti Kiwira coal maining inamilikiwa na jamaa zake wa karibu tena wengine ni wanafamilia za karibu kabisa ninabaki kujiuliza hivi kwa haya yaliyozungumzwa jana na waziri mkuu wa sasa hata wakikirudisha hicho kiwanda hisa zake zote serikalini hili halitabaki kuwa doa kubwa kwake au mbele ya nyuso za watanzania walio makini na wenye upeo wa kuelewa?

na hasa kwa kuzingatia vitabu vya dini kuwa Musa alifanya kazi kubwa ya kuwataoa waizirael toka utumwani huko Misri kwa farao lakini kosa moja tu likamfanya kutofika nchi ya ahadi kanani licha ya mungu wake kumsamehe, je mheshimiwa katika mazingira haya kama yasemwayo yote ni hakika ni hivyo kweli? je heshima yake kwa watanzania ipo kwenye daraja ya juu kama awali? au kwa hilo moja lisemwalo ndo tumuhukumu?
please note;naomba changia kwa lugha positive ukitambua kuwa alikuwa kiongozi wa taifa letu tusiwe kama wale jamaa wajinga wa the utamu sisi ni watu makini
 
Mkuu sikuzote it is very hard to build a reputation but very easy to lose it. Mfano mzuri ni mtu unaye muamini akikudanganya. Hata akuambie vipi kuwa kakudanganya mara moja tu utaanza kujiuliza matendo yake ya nyuma na hata matendo yake ya baadae utaya shuku. Hata kama kafanya mazuri mangapi hiyo haiwezi kuwa kisingizio cha kufumbia macho hili jambo moja tu. Tunajuaje kama kuna mengine ambayo bado hatuya fahamu? Tutajuaje kama Kiwira isinge valiwa njuga angeendelea na utapeli huo?
 
mimi binafsi namheshimu sana Rais mstaafu mheshimiwa Benjamini mkapa kwanza nikiwa kama mpenda michezo kwa uwanja wa kisasa aliotuachia pili katika suala zima la kutengeneza nguzo za kufuafua uchumi lakini huwa nikisikia na kusoma magazeti eti Kiwira coal maining inamilikiwa na jamaa zake wa karibu tena wengine ni wanafamilia za karibu kabisa ninabaki kujiuliza hivi kwa haya yaliyozungumzwa jana na waziri mkuu wa sasa hata wakikirudisha hicho kiwanda hisa zake zote serikalini hili halitabaki kuwa doa kubwa kwake au mbele ya nyuso za watanzania walio makini na wenye upeo wa kuelewa?

na hasa kwa kuzingatia vitabu vya dini kuwa Musa alifanya kazi kubwa ya kuwataoa waizirael toka utumwani huko Misri kwa farao lakini kosa moja tu likamfanya kutofika nchi ya ahadi kanani licha ya mungu wake kumsamehe, je mheshimiwa katika mazingira haya kama yasemwayo yote ni hakika ni hivyo kweli? je heshima yake kwa watanzania ipo kwenye daraja ya juu kama awali? au kwa hilo moja lisemwalo ndo tumuhukumu?
please note;naomba changia kwa lugha positive ukitambua kuwa alikuwa kiongozi wa taifa letu tusiwe kama wale jamaa wajinga wa the utamu sisi ni watu makini

Ndugu yangu bila shaka una heshima ya woga, ambayo ni mbaya kwani ni utumwa.
Mkapa amefanya mengi mabaya akiwa mkuu wa nchi si hili la kiwira tu kama ulivyosema, usimwogope kumwambia ukweli bali usitumie maneno machafu katika kumwambia ukweli. Kuna rada, ndege, EPA, TICTS,net group nk.

Mkapa alikiuka katiba kwa kutenda yale aliyoyatenda akiwa ikulu na hilo analijua wazi.

Kama kuna mazuri aliyoyatenda akiwa mkuu wa nchi hatupaswi kumshukuru kwani alikuwa anatimiza wajibu wake. Alituomba tumpe kura zetu ili atende hayo mazuri, sasa leo hatuwezi kumshukuru kwa kufanya mazuri. Tulimpa kazi na tukawa tunamlipa mshahara na malupulupu lukuki kwani ndiyo mkataba kati yake na sisi ulivyosema.
 
  • Watetezi wake wajipanga upya
  • Watuhumiwa ufisadi wamo

Na Saed Kubenea

MPANGO wa kumtetea rais mstaafu Benjamin Mkapa umelenga mbali. Umeandaliwa mahsusi kubeba wote wanaolalamika kuwa Rais Jakaya Kikwete amewatelekekeza, MwanaHALISI limeelezwa.

Taarifa za ndani ya serikali zinasema mpango wa kumsafisha Mkapa, uliozinduliwa bungeni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Ijumaa iliyopita, umelenga orodha ndefu.

“Ndugu yangu, Mkapa naye ana ndugu na marafiki. Lakini pia anajua mengi juu ya kila aliyeko madarakani sasa. Akiamua kubwatuka asubuhi moja, nchi inaweza kutikisika,” ameeleza.

Pinda alilieleza bunge kuwa Mkapa ni mcha Mungu, mwadilifu, siyo fisadi na hana fedha nje ya nchi, katika kile ambacho wafuatiliaji wamesema ni “kupoza hasira za Mkapa na kuogopa ulipizaji kisasi wakati ukiwadia.”

Alikuwa akijibu baadhi ya hoja za wabunge ambao wamekuwa wakisisitiza kuwa Mkapa ahojiwe na hata kufikishwa mahakamani kutokana na kukiuka maadili ya utawala bora.

Kilio kikubwa cha wabunge kimekuwa juu ya miliki ya mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya ambao inadaiwa kampuni ya Mkapa na familia yake, ilijibinafsishia tena kwa bei ya “bure.”

MwanaHALISI limeelezwa kuwa hatua ya Pinda ya kumtetea Mkapa hadharani imekuja baada ya kukwama kwa mpango wa awali wa kumfanya rais huyo wa zamani kuwa Kamanda wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM), ambao wangepewa jukumu la kumlinda.

“Kwanza angetangazwa kuwa Kamanda wa Vijana. Akasimikwa na Rais Jakaya Kikwete, na kwa kofia hiyo, angejitokeza kwa nguvu zote na kuvunjilia mbali tuhuma zote huku akibebwa na vijana,” kimeeleza chanzo cha habari hizi.

Imefahamika kuwa kiongozi wa vijana ambaye angebeba bango la Mkapa angekuwa yule anayeheshimika kwa vijana wengi; mwenye hoja nzito na ambaye hatiliwi mashaka na wengi katika umoja huo.

Hata kama kijana wa aina hiyo angepatikana, na taarifa zinasema alikwishatonywa, tatizo jingine lingekuwa jinsi ya kushawishi vijana kuwa kamanda wao siyo tena Mzee Rashid Mfaume Kawawa, na bila sababu yoyote nzito.

Hata hivyo, kutopatikana kwa kijana mwenye uwezo wa kuunganisha wenzake kumbeba Mkapa, kulifanya hata pendekezo jingine kukwama.

Hili ni lile lililohusu makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Samwel Malecela. Kumekuwa na ushawishi wa chini kwa chini, tangu mwaka jana kwa kuhusisha baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu (CC) kumfanya kamanda wa vijana.

Mkakati wa ukamanda wa vijana umekuwa ukienda sambamba na kauli za wabunge za kumtetea Mkapa; na hivi karibuni Chrysant Mzindakaya (Kwale-CCM) alilazimika kunukuu maandiko matakatifu kumtetea.

Kwa hiyo kuibuka kwa Pinda na utetezi ambao haukutarajiwa, kumechukuliwa na wachunguzi wa siasa za sasa kuwa Mkapa bado ana nguvu “nyuma ya pazia.”

Taarifa zinasema kinachofanyika hivi sasa ni mshikamano miongoni mwa wote ambao wanalalamika kuwa wametupwa nje ya duara la madaraka tangu Rais Kikwete aingie madarakani.

“Sasa hakuna sababu ya kuangalia nani ametupwa nje na kwa sababu ipi. Kila mtu aweza kuwa na sababu zake. Hawa wakiungana wana uwezo mkubwa wa kurudi kwa kishindo hata kama ni kwa sanduku la kura,” ameeleza mmoja wa wabunge.

Miongoni mwa walio kwenye foleni na wenye shauku kubwa ya kurejea madarakani, ni aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa.

Wengine ni waliokuwa mawaziri wa zamani wa nishati na madini, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha waliojiuzulu kufuatia kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond ambayo ndiyo pia ilimng’oa Lowassa.

Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge, Katibu Mkuu wa zamani wa CCM Philip Mangula, mweka hazina wa zamani wa CCM, Rostam Aziz, ni miongoni mwa wanaoweza kuungana na yeyote ili kuhakikisha hadhi yao inarejea.

Kauli ya waziri mkuu Pinda sasa itatumika kama wito wa kuunganisha wote wenye malalamiko kuwa serikali ya Rais Kikwete imeshindwa kuwalinda na kuwatetea na wote ambao kwa muda sasa wamevikwa tuhuma za ufisadi.

Wachunguzi wanasema kinachotendeka ni maandalizi ya kutafuta muwafaka kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.


Source:
Gazeti la MwanaHALISI
 
Kubenea kweli kaishiwa sasa anaunga unga habari kwa super glue tu...
 
Mbona nimeshindwa kuielewa hii habari? what is the message!
 
Kubenea kweli kaishiwa sasa anaunga unga habari kwa super glue tu...

.... jinsi unavyompinga Kubenea nilitegemea utasema anaunganisha kwa ulimbo... kumbe superglue...well, that should hold then!!
 
Back
Top Bottom