Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Anayezungumzwa na babu si Fredy Maro ambaye ni mpiga picha wa ikulu hadi leo bali ni Joe Maro wa BoT ambeya yeye na Justine Maganga, ndio wamiliki wa kampuni iitwayo Wace Technology, ambayo ni wabia na Net Group katika lile dili la Tanesco. But its fact kwamba ni familia ya mama (bibi) yetu Anna Mkapa. Lakini hoja ya kusema kwamba THISDAY inaleta habari mpya tusahau ya zamani munawaonea, maana habari haiwezi kuwa ile ile kila siku na kwa hizi zinazotoka sasa nadhani tuwaunge mkono kwa nguvu zetu zote kwani wamethubutu. hii itasaidia kuwafanya walioko madarakani sasa kutofanya makosa na hivyo kututumikia. Vinginevyo tutakua tunaliwa na hakuna wa kuguswa. Labda kama miongoni mwetu tumeonja hiyo KEKI ya IKULU
 
THISDAY la leo limeandika DOING BUSSINESS FROM IKULU, likiwa na picha kubwa ya Mkapa na Anna na nyuma yao jengo la IKULU, wameandika kuwa kampuni yake iitwayo ANBEM limited ilianzishwa 1999 akiwa Ikulu na alijiita MJASIRIAMALI, na alikopa sh milioni 750/- lakini bahati mbaya leo hadi sasa halipo katika web. Sijui wamelihujumu? TUNAFUATILIA mwenye kupata habari kamili atutumie humu
 
Last edited by a moderator:
Halisi,

Nakubaliana nawe, kwa hili tuwaunge mkono Thisday na hizi habari wanazofuatilia ni nzito mno na wakifanikiwa itasaidia hata magazeti
mengine kuanza kufanya uchubguzi wa nguvu na sio porojo za nipashe.

Kwa Tanzania mafanikio yatakuja pole pole hata kama ni hatua ndogo ndogo bora tunasonga mbele ni nafuu kuliko kurudi nyuma.
 
Tatizo la Watz, vyombo vya habari vikitoa habari vinatolewa kasoro, na vile vinavyonyamaza vimenunuliwa....sijui lipi jema.
 
Doing business …from Ikulu

•ANBEM Ltd stated objectives include to act as merchants, general traders, warehouse, stockists, shopkeepers and operators of supermarkets, commission agents and carriers

•Latest total registered debts: 750m/-, borrowed from two local banks


THISDAY REPORTERS
Dar es Salaam


FORMER President Benjamin Mkapa and First Lady Anna Mkapa started their own company and became actively engaged in business as entrepreneurs and directors of a private firm while still at State House, we can comfortably reveal today.

Our investigations have established that as sitting president and first lady, Mr Mkapa and his wife registered a private company under the name of ANBEM Limited in 1999, just four years into his presidency.

The company was awarded certificate of incorporation number 36547, with Mr and Mrs Mkapa being allotted one nominal share each and listed as directors of ANBEM Limited.

The legal documents for setting up ANBEM Limited were drawn up by Dar es Salaam-based lawyers Kapinga & Company Advocates, and the business was duly registered as a private company limited by shares.

Among many other things, the stated objectives of ANBEM Ltd include: “To carry on business and to act as merchants, general traders, warehouse, stockists, shopkeepers and operators of supermarkets, commission agents and carriers.”

Further investigations by THISDAY have revealed that the company’s annual returns, filed with the Business Registration and Licensing Authority (BRELA) by 2005 when Mr Mkapa was retiring from the presidency, indicated that the occupations of the former president and first lady were company directors.

The 2005 annual report of ANBEM Ltd shows that the company had total registered debts amounting to some 750m/- by the time the accounts were filed.

“Total amount of indebtedness of the company in respect of all mortgages and charges of the kind which are required to be registered with the registrar of companies under the Companies Ordinance (is) 750,000,000/-,” says the report signed by Mr Mkapa himself on July 31, 2005 - when he was still the sitting president.

It has been established that ANBEM Ltd, with Mr and Mrs Mkapa as directors, was granted loans amounting to over 750m/- from two different local banks between July and December 2002 - while the couple was still at State House.

The latest revelations about the former president and first lady registering their own company and starting to do business while at Ikulu have been made after THISDAY reported this week that the Mkapa family owns an office building in the city where a new bank with some big-name local businessmen as shareholders is to be located.

According to our investigations, Mr and Mrs Mkapa bought the building, registered under certificate of title number 6809 at Number 8 Ocean Road in the up-market Sea View area in Dar es Salaam, from a company called Tanzania Building Works in 2002.

Situated right adjacent to the official residence of the former president and first lady, it is understood that the two-storey building will be the official headquarters of the upcoming Bank M (Tanzania) Limited, now in the final stages of being launched after a fast-track registration process that started only in February this year.

The bank has an initial share capital of 6.5bn/-, with various prominent members of the local business community listed as shareholders.

Mr and Mrs Mkapa served as president and first lady in the highest office in the land from 1995, and Mr Mkapa concluded his second and final term as president in 2005.

THISDAY has made all effort to seek Mr Mkapa’s comments on both Bank M (Tanzania) Limited and ANBEM Limited issues through written questions sent to his office in the city. However, no response has been received.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani hizo objectives ni za kawaida kama watu wengine wanavyosajili makampuni. Lakini, wanajiamini nini hawa THISDAY? sina hakika kama Mkono atakaa kimya si muda mrefu atafikisha mahakamani
 
Haki ya nani !! wallah nchi hii? Ndio maana kumbe watu wanaanda mpaka MTANDAO ufanye kazi kwa miaka 10 ili nao waje wawe wajasiriamali kutoka katika `kasri kuu` Kweli CCM kiboko!!
 
THISDAy wamesahau kuongeza kuwa"..they started the company while Mwalimu Nyerere was terminally ill in a London Hospital".

Polepole madai yetu kuwa CCM ni stock exchange ya viongozi yatazidi kuthibitika na maneno ya Mwalimu Moshi kuwa "hakuna kitakachoendelea hadi CCM ikae benchi" nayo yatakamilika.
 
Rais akija kukopa kwa TZ, ni bank gani hiyo itakayopoteza hata muda kuangalia kama anatimiza masharti?

Nafikiri ni makosa kwa rais aliyeko madarakani kuwa director kwenye private companies. Hivi sheria zetu zinasemaje?

TRA kweli wangeweza kumwendea rais Mkapa ni kumkaba kwa kushindwa kulipa tax inayotakiwa?

Ni sawa kwa mbunge kuwa mkurugenzi kwenye kampuni lakini nisingetegemea waziri mpaka rais na wao kuwa wakurugenzi.

Rais wa Tanzania pamoja na baraza lake la mawaziri wana marupurupu mengi mno na sioni ulazima wa kuendelea kujihusisha na biashara wakati wako kazini.
 
Kesi wanayoweza kushitakiwa ni "UHAINI, UCHOCHEZI, KASHFA (Deffamation). Naona kama hii ni kali sana. Hapo ndipo kipimo cha uvumilivu wa wanasiasa wetu ndani ya CCM
 
Kwa kesi ipi Halisi?

Hao THISDAY mbona wanaandika habari ambayo wala haikutakiwa kuwa habari? Mkapa na mkewe kuwa na kampuni kuna ubaya gani iwapo wamefuata masharti yote ya usajili?

Na hata kuwa na mikopo benki pia kuna tatizo gani? Azimio la Arusha lilishazikwa kwa kuwa replaced na Azimio la Zanzibar. Yale mambo ya enzi za Mwalimu ya kiongozi hatakiwi kuwa na nyumba za kupangisha wala hayapo tena!

Viongozi wanaruhusiwa kufanya biashara halali....though the objectivity of banks, tax authorities etc may be impaired when dealing with such a company!
 
Je kuna sheria yeyote wameivunja? kama ipo ningependa kuelimishwa.

Tukumbuke pia tuna azimio la Zanzibar ambao pamoja na mambo mengine lina ruhusu kiongozi kuwa na Nyumba, share etc.

Honestly I see nothing wrong there
 
Kanda2,

Kama huoni tatizo hapo na kuna watu wengi wanakubaliana na wewe basi
ndio maana tuna matatizo.

Conflict of interest hapo ni rahisi mno kujitokeza.

Binafsi sitegemei na nisingependa kuona rais wa nchi anakuwa mkurugenzi
kwenye makampuni binafsi wakati bado yuko madarakani. Ndio maana wanalipwa vizuri ili kuondoa tamaa za utajiri. Akimaliza muda wake anaweza kufanya biashara apendavyo lakini sio akiwa rais.
 
Kanda2,

Kama huoni tatizo hapo na kuna watu wengi wanakubaliana na wewe basi
ndio maana tuna matatizo.

Conflict of interest hapo ni rahisi mno kujitokeza.

Binafsi sitegemei na nisingependa kuona rais wa nchi anakuwa mkurugenzi
kwenye makampuni binafsi wakati bado yuko madarakani. Ndio maana wanalipwa vizuri ili kuondoa tamaa za utajiri. Akimaliza muda wake anaweza kufanya biashara apendavyo lakini sio akiwa rais.

Nchi inaongozwa na utawala wa sheria na sio "mategemeo" au "mapenzi" ya watu. Kama hakuna sheria iliyovunjwa then hakuna tatizo bila kujali wengi au wachache wanakubali/wanakataa
 
Kanda2

Nakuunga mkono na mguu...

Niliwahi kusema kuwa hawa viongozi na waliokuwa viongozi wanafanya haya mambo yote wakijua kuwa hakuna sheria/chombo/vyombo wala mwananchi yoyote mwenye balls za kusema "this is wrong". Sasa kama tutaendelea kuwa hivyo mimi naona makosa sio ya hao viongozi na waliokuwa viongozi; makosa ni yetu wenyewe...tafadhalini sana hebu tulalamike taratibu bila sauti...tena sasa kuna hii EAF wakenya, waganda etc wanaweza kutucheka sana...aibu.

Hawa ThisDay mbona wanamuandama sana Mkapa? kuna jambo gani hapa...kama CCM ameshaachia kiti, na Mtandao wameshaweka Timu yao Kila mahali...lakini mbona bado wanamuandama. Mwenye inside please atuelimishe hapa.
 
Nadhani hizo objectives ni za kawaida kama watu wengine wanavyosajili makampuni. Lakini, wanajiamini nini hawa THISDAY? sina hakika kama Mkono atakaa kimya si muda mrefu atafikisha mahakamani

MImi sijaelewa huyu bwana anapinga au ana unga mkono!!?

Achana na hiyo.
Mwaka 2001 first Lady akiwa na Body Guard wake nyuma anaaingia duka fulani town hapo kisutu zamani kituo cha maba si ya mikoani nikishughudia akinunua majora ya vitamba vya pazia anaenda kutengeneza pazia (i thought kwamba anaenda kupamba ikulu yetu.....) kumbe amepata tenda mahara ya kusupply curtains kwenye nyumba ya kigogo mwengine sijui wizara fulani....nikabaki mdomo wazi......!
kazi za wa jasilimia mali wadogo anafanya First Lady na hawa wadogo wadogo wafanye nini...?nikajibiwa wakuchukue mkopo wa alfu ishilini na tano (25,000/-)wachome vitumbua.
 
Watanzania tuna matatizo sana:
(a) Kuuliza kwamba kwanini Thisday wanamfuatilia sana Mkapa, maana yake ni nini hasa. Kwani jamaa wameanza kuandika jana habari zake kuhusu ni jiinsi gani alivyokuwa najinufaisha kupitia ofisi yake. Kuhusisha Thisday na mtandao ni utoto kwani jamaa inabidi ajibu hizi tuhuma na sio kutafuta sababu za nani mchawi wa kutoa habari.
(b)Tunaposema hakuna tatizo tunamaanisha nini hasa? binafsi naona tatizo lipo tena kubwa tu. Kuwa na rais ambaye anafanya biashara kutokea IKULU, haki kwa washindani wake kibihashara itatokea wapi?
(c) TUache porojo, tujadili issue.
 
Back
Top Bottom