Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Mimi ningemshauri Mkapa nyamaze kabisa asiongee chochote kuhusiana na aliyofanya wakati akiwa madarakani. Kwanza aliingia madarakani kwa mbwembwe za kutangaza mali zake hadharani, lakini baada kuingia madarakani hakudiriki kuzungmzia chochote kuhusu utajiri wa ghafla alioupata yeye na Sumaye wake. Ustaarabu ni kwa yeye kunyamaza aiachie historia ifanye kazi yake kwa sababu alishajikosesha authority kama aliyokuwa nayo mtu kama Nyerere au Kawawa. Mkapa hawezi kuongea jambo bila kuwakumbusha wananchi jinsi alivyokuwa haitakii mema nchi hii kwa kutapanya rasilimali zetu bila kujali maslahi ya nchi.
 
Waandishi wa habari wengi pale Tanzania wanababaisha sana hasa katika kuhoji na kuandika mambo ya kisiasa. Kwa sasa hivi kila kukiach utakutana na headlines kama "Kikwete Kiboko Kweli Kweli"
 
Hizi tuhuma hazina ukweli kabisa... Huu ni uhuni unaotumika nchini kutaka kuwadharau waandishi wetu kwa sababu wanazungumzia issue za leo na sio jana...

Nakumbuka vizuri sana waandishi wetu waliyavalia njuga mambo kibao ktk awamu ya Mkapa na hata mengine kufikishwa ama kuwakilishwa na chama chetu cha Mawakili lakini palikuwepo na kundi fulani la wasomi ambao walitetea sana kwa utumiaji wa takwimu za kiuchumi kutupumbaza.

Wapo waliomsifu Mwinyi lakini system iliwavaa na kuziweka sifa hizo nje. Mmediriki hata Kumsuta Mwalimu kwa kupitia haohao waandishi wetu waajiriwa! Hawa jamaa binadamu wana familia zao zinazowategemea na nyie wanasiasa (waajiri) ndio mmekuwa mstari wa mbele kuongoza kila kinachoandikwa magazetini.

Nakumbuka pia hata ktk mijadala hii tuliopinga uongozi wa Mkapa tulionekana wafitini na walalahoi. Kuna baadhi ya wanabodi ambao walishuparia Ubora wa Utawala wa Mkapa. Hii ilikubalika lakini haikutosha Nyie (pro Mkapa) mkafikia kufuta ama kuondoa kabisa uwezo wa tovuti zinazompinga Mkapa, kufanya kazi zao.

Sasa hawa waandishi wataandika kipi ikiwa mwajiri wake kampa kazi ili kuuza gazeti.

Mnapoyafungia magazeti na vitisho kwa watu mnategemea hawa waandishi watakula hizo nyimbo za mlalahoi?.. Huu ni Ulimwengu wa Biashara na kama kweli mnaitakia nchi yetu hali basi viongozi wote wenye nafasi ndani ya CCM wasimiliki magazeti. Iwapo Rostam anamiliki magazeti mengi nchini hapa utategemea habari gani zaidi?

Ajabu hawa hawa leo hii wanarudi tena na mbinu mpya...
 
Mkandara,

Nakubaliana na wewe kwamba waandishi wa habari walijitahidi wawezavyo ila
serikali ya Mkapa ilikuwa inatumia vyombo vya dola kuminya hoja zilizokuwa zinawapinga.

Sasa ni mwaka toka JK awe rais, sijasiki Mtikila, Hamad au Mrema kawekwa ndani, nini kinaendelea? Badala yake naona wanaalikwa kwenye sherehe za kitaifa na wanaongea na rais watakavyo.

Huu ni mwanzo mzuri sana katika kukuza ushirikiano na amani ambayo Tanzania tunajivunia sana.

Sijui Mkapa anajisikiaje anapoona JK anapeta bila hata kuwafunga wapinzani?
 
Mtanzania

Ina maana rais amewaweka mfukoni viongozi wa upinzani?
 
MKAPAmnafiki mmoja alikwenda Zenj kule kshuhudia kupatika KWA AMANI YA VISIWANI nakutia sahihi ya unafiki huyu muulizeni wapi imefikia?mshenzi huyu,ndio maanamngu kamuumbua hafanani na mtu yoyote,kuanzia sura mpaka umbo michelini
 
Nadhani licha ya hiyo guilty consciousness,Mkapa anajaribu kufanya kila analoweza asisahaulike machoni na masikioni mwa watu.Unajua pamoja na usanii wa JK na madudu ya serikali yake,ndani ya mwaka mmoja alokaa madarakani umemfuta kabisa Ben kwenye macho na masikio ya watu.The guy was so rude,na alikuwa na dharau kwa waandishi wa habari bila wao hawezi kusikika.
Kuna mtu anaitwa Aden Rage,m-babaishaji flani ambaye anaweza kuongea lolote lile alimradi jina lake lisikike redioni au lisomwe gazetini.Nadhani Ben anajaribu kuiga hii strategy mufilisi ya Rage.
Kwa kweli ni upumbavu kutumia mfano wa jambazi kama Mzindakaya kudai kuwa ni matunda ya ubinafsishaji uliowakwamua wazawa.Nakumbuka hilo eneo analosifia Ben ndilo lililokuwa linaliliwa na wanyonge ambao hawakuwa na mtetezi.Sasa hii haitofautiani sana na mwonekano wake:Rais kitambi kikuuubwa na cheni nene ilhali wananchi wake wanakondeana kwa njaa.Sema tu hao wafadhili wakati mwingine wanapotoa misaada wana-neglect vitu kama mwonekano wa huyo anayeomba msaada.
 
Kichuguu,
Shukran na kama huyu mdudu angejua!
yaani sera nzima ya ubinafsishaji anakuja tupa mfano wa Mzindakaya!... Wangapi wamepata nafasi hiyo?. Je, hao ng'ombe 3,000 sijui wa kizungu wamesaidia nini zaidi kwa wananchi, hata kuchuliwa kama mfano bora wa ubinafsishaji .Vitu muhimu vyote kaviuza nje!.
Mfinyu wa kufikiri sana mbona kuna wafugaji wengi sana wenye ngo'mbe zaidi ya 3,000 kwa wakati wote mkoloni na Ujamaa na hawakupewa mashamba kuwawezesha wao. Mbali na wafugaji hata wasomi wote wa mifugo leo hawana kazi kutokana na kusahaulika kwa wizara nzima.
 
Hii taarifa kama niya kweli, it attracts more curiosity than answers to any queries watu wameuliza in the past...Ngoja nijaribu kuwa na positive spin... lakini kazi ipo.... Kwanii.. hawa akina Mzindakaya wako wangapi Tanzania?? Watolewe list basi alafu media ifanye kazi - mimi ntalingoja hilo!

With due respect kwa Mzee wetu wa Bunge, yeye ni very Senior na amekaa Serikalini muda mrefu sana (ambapo unzweza pia sema kapata wapi muda kufanya such a project anyway wakati ana majukumu ya public office mengi tuu) na sijui watu wa calibre yake ni wangapi kwa kweli kwa Tanzania nzima.

Hivi, ndio tuseme yeye mwenye Rais Msataafu hana mfano wake yeye binafsi anaoweza kuutumia? Yaani yeye kununua hizo mali zilizokuwa zinauzwa? Kwani process iliotumika akpata Mzindakaya anaweza share na public how it all worked?

Nadhani kama walivyosema wengine, shutuma ni kwenye process, procedures and luck of transparency ndio imezaa majungu na malalamishi mengii tuu...

Taasisi.
 
Taasisi,
Unajua huyu mtu alisahau kabisa Watanzania. Aliuza NBC kwa kumhadaa Mwalimu akae kimya. Mikataba yote ya akina Barick imepitishwa chini ya uongozi wake. Leo anamtaja Mzindakaya kama mfano wa kuwezesha wazawa. Can you imagine? Mtu aliyekuwa analimbukia na kuramba miguu ya wawekezaji leo anazungumzia "uzawa"? What a joke.
 
Hii taarifa kama niya kweli, it attracts more curiosity than answers to any queries watu wameuliza in the past...Ngoja nijaribu kuwa na positive spin... lakini kazi ipo.... Kwanii.. hawa akina Mzindakaya wako wangapi Tanzania?? Watolewe list basi alafu media ifanye kazi - mimi ntalingoja hilo!

...

Hivi, ndio tuseme yeye mwenye Rais Msataafu hana mfano wake yeye binafsi anaoweza kuutumia? Yaani yeye kununua hizo mali zilizokuwa zinauzwa? Kwani process iliotumika akpata Mzindakaya anaweza share na public how it all worked?

...

Taasisi.

Hawa wakina Mzindakaya wako weeengi...inategemea aina ya 'ubinafsishaji' walioufanya ndani ya awamu ya Mkapa-
Kwa mfano:
-IGP anapokuwa na mazahanati, mashamba, mimagari etc hata anafikia kuwa mwanasiasa kwa kugawa misaada kwenye 'jimbo' lake..huu nao ni ubinafsishaji au?
-PM anapokuwa na shamba+mifugo mpaka mingine majuzi ime-raba hadi vyombo vya dola vikaingilia, huo nao ni ubinafsishaji au?
-Idd Simba anapohodhi miradi kibao nayo ni ubinafsishaji au?
-Waziri EL(as he then was) anapohodhi kakijiji ka nyumba huko Ars nao ni ubinafsishaji au?
-Magufuli anapojiuzia kakisiwa kalikokuwa ngome ya wajerumani kwa kisingizio cha kununua nyumba ya serikali(..in this I stand to be corrected..) huo nao ni uwekezaji wa wazawa au?
-Yote tisa- kumi ni pale Mkapa anapogeuza Lushoto kuwa kituo cha kitalii kwa hoteli yake ya kitalii na jumba lake la kifalme huko kwenye iliyokuwa ikulu ya wajerumani- yeye naye alibinafsisha au? kama ndio mbona hazungumzii hilo?
Na kwa taarifa za kuaminika mara baada ya kufungua hoteli hiyo alipeleka fliers kwa wenye makampuni ya utalii ili wampelekee wageni- huo tuuite uwekezaji wa wazawa au?
..bila ku-mention nyumba alizonunua mama Mkapa maeneo mbalimbali hapa nchini katika sera ya kuuza nyumba za serikali...

There is a long list of this..but the issue is..kweli Mkapa ameona hilo la Mzindakaya na ng'ombe wake 3000 ndo national issue?
Huu ni upuuzi!
 
Jamaa anazidi kupeta tu. Ama kweli dua la kuku halimpati mwewe na Mungu si Athumani!

Mkapa conferred honorary degree
MAURA MWINGIRA
Daily News; Wednesday,January 10, 2007

THE United Kingdom's Newcastle University senate has conferred a Honorary Degree to retired president Benjamin William Mkapa.

Mr Mkapa was bestowed a Doctoral degree of Civil Law, which is the highest honour that the university could offer to few individuals worthy of such distinction.

A statement issued by the university said Mkapa has been honoured for his major contributions and impetus in the campaign to make poverty history. Mkapa was also hailed for his dedication to debt cancellation and hunger in the developing world.

"There's something familiar about Benjamin Mkapa's story; a graduate joins a political party with socialist leanings, rises rapidly through the establishment, then leads a landslide electoral victory. He then focuses on education and helps shift the economy to a successful and stable mixed model. He is popular though he does suffer criticism over his military policy from Clare Short," the statement from the University said.
 
Kama ni mfano basi yeye mwenyewe ndiye angekuwa mfano mzuri zaidi kuliko Mzindakaya.Maana Mchuchuma ni yake,na sasa wanakaribia kuanza kuzalisha umeme na kutuuzia,asingekuwa rais angepata hiyo opportunity? Kwa kweli anakejeli tu,na kutubeza wananchi.
 
major congributions.....and impetus to make poverty history? Mkapa? What a big joke!
 
Kama ni mfano basi yeye mwenyewe ndiye angekuwa mfano mzuri zaidi kuliko Mzindakaya.Maana Mchuchuma ni yake,na sasa wanakaribia kuanza kuzalisha umeme na kutuuzia,asingekuwa rais angepata hiyo opportunity? Kwa kweli anakejeli tu,na kutubeza wananchi.

Mzee Zanaki,
Mchuchuma nayo ya huyo mzee BM? Hao Wahindi na NDC kumbe hamna kitu!
 
Mzee Zanaki,
Mchuchuma nayo ya huyo mzee BM? Hao Wahindi na NDC kumbe hamna kitu!

Sorry sir,that shud have read Kiwira Coal Mine,yes ana share huko Kiwira na sio Mchuchuma
 
Back
Top Bottom