Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Sitatumia cheo wala ofisi ya umma kwa maslahi yangu binafsi...hivi hii ni ahadi ya ngapi?
 
Utajaza wewe hiyo ni ya ngapi...........!
Wenzio wanaendelea kula tu,tena bila ya wasiwasi wanajua yote tuyasemayo na kuyalaani.
Sauti zetu ni kama tunampigia kelele kiziwi kwa sasa.
 
Mkuu mheshimiwa Kada mpinzani, mjibu Mafuchila.
 
hapo mie naogopa bwana,hiyo list ya ao wenye duka lenyewe inanitia wasiwasi kabisa,na ndio maana staff wengi wanakimbilia uko
 
Ibrah,
KadaMpinzani, hawezi kukumbuka hiyo kanuni, kwani alikuwepo Zenji wakati wanapitisha azimio. Kwi kwi kwi
 
hapo mie naogopa bwana,hiyo list ya ao wenye duka lenyewe inanitia wasiwasi kabisa,na ndio maana staff wengi wanakimbilia uko


Mkuu Middle

Staff wengi kutoka banks nyingine hapo jijini au una maana gani hasa?
 
Yebo Yebu mkuu, tatizo si kumiliki mali ila namna ulivyozipata hizo mali.

Miiko ya uongozi ya Chama mama (TANU) sina hakika na CCM inakataza kutumia nafasi ya umma kwa kujinufaisha.

Ni vema Mzee wetu akajisafisha kwa kutuambia alikopa benki gani kupata mitaji hiyo, hatutaki kujua alikopa shilingi ngapi!


Watanzania mpaka siku tuamke ndipo tutaweza kuwa na kiongozi atakayefuata maadili. Kwa sasa hivi tunategemea miujiza tu; kama mnavyojua miujiza kuna wakati inakuja na kunawakati inakuwa patupu. Hawa jamaa wanatunga sheria wenyewe, wanazisimamia wenyewe na kujilinda wenyewe...kwa nini wasijigaiwie wenyewe? Mimi ninachoshuru ni kwamba angalao haka ka-jengo pale sea view kamepata ukarabati na sasa panakuwa bank; watanzania watapata ajira hapo na wao wakajijengee kajengo kao huko kawe, mbezi, tegeta, tabata n.k

Ninachoogopa ni hayo majina kwenye umiliki wa hiyo benki, sidhani kama faida ya hiyo bank itajenga au kukarabati jengo lingine hapo Tanzania au itatumika kununua majengo mengine America, Europe na Asia.

My point is watanzania ni kama tunawaruhusu walio madarakani na waliokuwa Mkapa et al kujifanyia watakavyo. Hivyo tukisikia wanafanya vijimambo kama hivi tusilalamike kwa sauti kubwa sana...tutachekwa.
 
Yebo Yebo,
Nakubaliana na maneno yako kwa kiasi kikubwa. Watanzania tumelala na ndiyo maana hawa viongozi wanatuchezea namna hii.

Kinachoshangaza hata vyama vya upinzani havikupiga kelele wakati wizi wa nyumba za serikali unaendelea. Nyumba zile ziko katika prime areas. Bei yake ktk soko ni kubwa zaidi ya bei ambayo viongozi walijitwalia.

Kitu cha ajabu na kutikitisha ni kwamba: wakati wizi huu unaendelea, magazeti, viongozi wa upinzani, walikuwa wamemkaba koo Sumaye kwa kukodisha shamba la eka 7 kibaigwa!!
 
jokakuu

Unakumbuka ufafanuzi alioutoa MKJJ kuhusu mazingaombwe...huo ndio mfano mwingine sahihi kabisa.


Hilo shamba la eka 7 lilikuwa mazingaombwe lilitumiwa katika haya mazingaombwe stadi.
 
This day huwa wanaibuka na issues za walio ondoka pale Serikali ya sasa inapokuwa kwenye deep shit . Rudini nyuma mchunguze . Sasa hii habari ya Mkapa itawachukulia muda na huku JK na kundi wanapunua.NO one is serious hapa This Day ni mali ya wana mtandao na si zaidi ya hapo kazi yao kuwamaliza wale wa zamani kinamna na pia ku divert issues . Hoja hii ingaliandikwa na Tanzania Daima ungalisikia kila kona wanasimama kuanzia Chimwaga hadi JK mwenyewe . Usanii tu hapa .
 
Lunyungu ,nakuunga mkono ni kweli hapa wanataka kutufanya tusahau kupigia kelele wale wanafunzi wa Ukraine,wakinamama walioandamana hadi ikulu juzi kupinga kunyanganywa mashamba yao na wale jamaa wa Twigta cement n.k.
 
Hii nyumba inasemekana mkapa alinunua kutoka kwa waziri mmoja wa wakati wake,huyo waziri aliinunua kutoka kwa huyo muhindi wa Tanzania Building Works.Huyu muhindi ana contract nyingi tu za ujenzi za serikali,na anawaibia kwelikweli.
 
Hii ndiyo CCM bwana na usalama wao . Maana manyumba haya hata JK kanunua lakini kimya leo issues za maana ziko nje basi wamekuja na hili . Kila mara likija jambo la maana mara utasikia Mahalu nk na baada ya siku chache kila kitu kimya . Ditto ilipamba moto wakaja na Mahalu leo hakuna lolote Ditto anapenda na Mahalu pia. CCM hawawezekani hawana nia ya kubadili Nchi ile kima endeleo na Kulikoni na This Day ni magazeti ya wana mtandao pure .
 
Dhana yako si sahihi. Ingekuwa hivyo, watu wote waliowahi kuwa marais au viongozi wa nchi duniani wangekuwa ni matajiri sana kama yeye. Lakini ukweli siyo hivyo ila kwa wale wachache waliowahi kupata tuzo kama za Noble prizes. Huyu Mkapa hakupata tuzo zozote za kimataifa kama zile alizopata Nyerere lakini yeye ni tajiri mkubwa kuliko Nyerere liocvha ya kuwa Nyerere alikuwa ni mwalimu wake na ndiye aliyempa kazi ya Urais, kama siyo matokeo ya wizi kutumia nafasi yake ya urais. Sasa hivi anatafuta nafasi ya kuhalaliasha wizi wake kwa kutumia mlangoi wa nyuma. Tunamsubiri Sumaye naye arudi atufungulie benki kubwa au kampuni kubwa ili kuhalalisha pesa alizovuna kinyume cha sheria wakati wa utawala wake.

Kuwa na nyumba ndio utajiri?
 
Kuna kila sababu za kumtaka Mkapa na Mkewe waeleze mali zoto walizokuwa nazo na jinsi walivyozipata. Mimi naamini kabisa kwamba katika mikataba ya kuileta Netgroup Problems (Makaburi), mikataba ya madini amnayo mpaka leo imefanywa siri, mikataba ya kununua Rada, Ndege ya Rais (ikumbukwe ndege hii ilinunuliwa wakati Mkapa amebakiza miezi michache kumaliza wamu yake), ununuzi wa magari ya Jeshi. Kuna habari pia kwamba Mkapa ana nyumba SA na katika baadhi ya nchi za magharibi. Kama yeye kweli ni Mr Clean, basi hakuna cha kuogopa asimame hadharani ili awaeleze Watanzania mali zote alizokuwa nazo na kipato chake chote wakati alipikuwa mfanyakazi serikalini mpaka alipofikia Urais.

Waswahili husema panapofuka moshi........
 
Pia kuna mkataba wa kuuza mali zilizokuwa za TTCL ambao aliyepewa mkataba wa kuuza mali hizo ni Shemeji yake Mkapa Feddy Maro, sijui alikuwa na uzoefu gani wa kusimamia uuzwaji wa mali, na hii tenda ilitangazwa wapi na wasimamizi wa kuamua nani aliyekuwa mshindi walikuwa kina nani.

Ikumbukwe kwamba TTCL ilikuwa na mali nyingi sana Tanzania nzima, kuanzia nyumba za wafanyakazi, maofisi, magari na vifaa mbali mbali vya ofisi.
 
Babu una maana Fred ambaye ni mpiga picha na alikuwa mpiga wa Rais BM ?
 
Kuwa na nyumba ndio utajiri?

Samahani sana jamani; habari hizi ziliniboa sana nilipozisoma jana usiku kiasi kuwa baadhi ya majibu yangu huko nyuma hayakuwa controlled. Samahani sana kwa wasomaji wote kutokana na majibu yangu mabaya ya huko nyuma.

Kuhusu Mkapa kujijengea utajiri siyo kwenye nyumba hii moja tu, kumekuwa na taarifa za kuwapo majumba mbalimbali aliyojipatia akiwa madarakani au baada ya kutoka madarakani. Kuna taarifa za jumba la kifahari huko Afrika ya Kusini, jumba jingine huko Washington au New York, jumba jingine kule Lushoto, na majumba kadhaa hapo Dar es Salaam. Kwa kiwango chochote kile huo ni utajiri.

Kibovu ni kuwa serikali yake ilijenga misingi mizito ya rushwa kiasi kuwa imekuwa ni kansa kwa nchi sasa hivi. Ingawa rushwa ilikuwapo nchini kabla yake, yeye alii-institutionalize na kuifanya iwe kubwa sana na ngumu kuong'olewa hasa kwa vile yeye mwenyewe alihusika nayo moja kwa moja. Serikali yake iliingia mikataba mbali mbali kwa rushwa ambayo ilikuwa ni mzigo kwa nchi nzima. Mikataba ya namna hiyo na madhara yake yanajulikana kinaganaga na sina haja ya kuitaja tena.

Sijui niseme nini ila ingawa Mkapa alifanya mambo kadhaa mazuri kiuchumi, alijenga msingi mbaya sana wa rushwa na yeye binafsi alijihuisha na rushwa kwa kiwango kikubwa kiasi kuwa mazuri yake yote yanafutika.
 
kama all the things are "facts" then let them burn in HELL and never come out ! yaani huu ni ujambazi wa hali ya juu, ebu naomba mtu aje na statistics za kuonyesha umaskini ulivyo, kila kiongozi anapoimba laki 1 serikalini basi ujue watz 5-7 hufa kutokana na kukosa chakula, dawa, maji safi, magonjwa sugu yanayosababishwa na maji+maambukizi, n.k. ajali barabarani ambapo pesa zilizoibiwa zingetumiwa ktk ukarabati wa barabara kuzuia ajali ! yaani ni mambo mengi sana mpaka mtu unashindwa kujicontrol na upuuzi wa hawa viongozi wetu.

Nadhani udikteta saa nyingine unafaa kuweka mambo sawa !! Maana watu kama akina JK, lowassa wanajifanya "wanafiki" hawajui kinachoendelea.
 
Back
Top Bottom