Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

Lazima tuhakikishe kwamba hili deni dhidi ya Mkapa halifutwi kienyeji. MKapa na mkewe wana mali walizojipatia kwa njia za haramu ambazo kama zikifilisiwa zinaweza kabisa kurudisha baadhi ya deni hili kubwa. Alikuwa na tamaa ya kuchukua mkopo ili kufinance mradi wake wa kifisadi wa Kiwira, sasa Watanzania tumemsimamisha. Hili la Mkapa kushindwa kurudisha deni kwa maoni yangu ni moja ya mafanikio makubwa sana katika vita dhidi ya mafisadi. Hongera wa JF, na wanahabari wote wa magazeti, TV na Radio waliovalia njuga swala la ufisadi kuhusiana na Mkapa.
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amekanusha kumtaja Rais mstaafu Benjamin Mkapa katika ripoti yake ya Mashirika ya Umma kuwa alitumia vibaya mkopo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Ludovick Utouh, alikanusha habari zilizoandikwa na gazeti la MwanaHalisi la Mei 13 mwaka huu, kwamba “Mkapa achota NSSF mabilioni ya shilingi na ashindwa kuyarejesha”.

“Napenda kukanusha taarifa hii, kwani katika ripoti yangu ya mashirika ya umma kwa mwaka unaoishia tarehe 30 Juni 2008, hakuna mahali nilipomtaja Mheshimiwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

“Katika ripoti yangu hiyo, aya ya 3.2.4 (ukurasa wa 74 hadi 77), nilitaka wakopaji tisa ambao kwa pamoja wamekopa NSSF jumla ya Sh 58,757,794,802 na katika deni lililotajwa na gazeti la MwanaHalisi la Sh 8,127,000,000 linahusu kampuni ya Kiwira Coal & Power Company,” alisema.

Aliongeza kuwa kutaja jina la Rais mstaafu Benjamin Mkapa kama mkopaji badala ya mkopaji halali ni kinyume na ripoti yake na huo ni upotoshaji ambao angependa kuukanusha kwa nguvu zote. “Ninaomba vyombo vya habari viwe huru kutumia ripoti yangu kama ilivyo na si vinginevyo, kwani kwa kutoa taarifa kama hiyo, kunapotosha umma na kunaweza kuleta mfadhaiko na chuki kwa waliotajwa isivyo halali,” alisema.

Alisema lengo la vyombo vya habari ni kutoa taarifa sahihi bila kuongeza maelezo ambayo yanaweza kusababisha taarifa husika ieleweke visivyo na ni imani yake kuwa umma utaendelea kuhabarishwa juu ya ripoti yake kwa usahihi. “Pale patakapokuwa hapaeleweki, naomba mje ofisini kwangu kwa ufafanuzi, kabla ya kuchapisha taarifa zinazopotosha na ambazo hazielezi yaliyo kwenye ripoti zangu,” alisema Utouh.

kaazi kweli kweli
 
Kama Mengi angeendelea kutaja hao anaodai mafisadi papa basi Mkapa angekuwa nambari sita kama si wa kwanza labada Mengi hakuwa na ugomvi nae. Maswali yoote haya huyu jamaa kakaa kimya anafikiri watz wanasogeza muda wasahau? anakinga ya kutoshitakiwa lakini hana kinga ya kunyamazia maswali yanayowakereketa watz wote katika kujua wapi zimekwenda rasilimali zao? kazi kwake...
 
Arudishe hela plus riba then aende zake akajiandea mabomu yanayosubiri kulipuka EPA, RADAR, M BANK etc.
 
Arudishe hela plus riba then aende zake akajiandae mabomu yanayosubiri kulipuka EPA, RADAR, M BANK etc.
 
Kwanini MKapa asifilisiwe ili kurudisha mikopo aliyokopa ambayo kuna ushahidi wa kutosha kwamba hana uwezo wa kuilipa?

Kufilisiwa haitoshi tunataka kuona anafikishwa kwenye vyombo vya sheria japo afikishwe kiwongowongo ,itatosha tu ,na wengine tutaridhika kwani naamini kabisa haya ya sasa ya akina Yona ni ya kiwongowongo lakini kadili siku ziendavyo yanayokuja kwa alama za nyakati japo hizo alama sijui zipo wapi ,mambo yatakuwa si ya kiwongowongo tena bali yatakuwa kweli.Ndio hapo mafisadi watakapojua kuwa Nyoka si mdudu (insect).
 

Mkopo anaodaiwa Mkapa umedhamiwa kwa asilimia mia moja na serikali. Kwa mujibu wa kanuni za Benki Kuu (BoT), kawaida serikali haidhamini mtu binafsi. Mkapa anahusishwa na umiliki wa mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira kupitia kampuni yake ya ANBEM anayosadikiwa kumiliki na mkewe, Anna...
Kwa hiyo alikopa kama kampuni. Habari ya kanuni against kukopesha mtu binafsi inakujaje hapo MwanaHALISI?

... kwa kuwa alidhaminiwa na serikali, basi ni serikali itakayolazimika kulipa au kufuta deni. Hata hivyo, CAG anasema hakuna nyaraka zozote zinazothibitisha kuwa serikali ilidhamini mkopo huo.
Kama hakuna uthibitisho kuwa serikali ilidhamini mkopo, sasa mmejuaje kwamba serikali imedhamini?

Mkataba wa mkopo huo ulitiwa saini 10 Julai 2007. Hata hivyo kuna udhaifu. CAG hakuona hati miliki ya mali iliyowekewa dhamana, jambo ambalo ni kinyume cha mwongozo wa NSSF juu ya vitegauchumi.
Mali iliyowekewa dhamana au iliyowekwa dhamana. Na umeshasema serikali ilidhamini huu mkopo, sasa mali gani tena ilitakiwa kuwekwa dhamana kupata mkopo? MwanaHALISI, unaacha ma gap kibao kwenye reports zako.
 
Hili suala la serikali kudhamini mikopo ya watu binafsi ambayo ina utata mwingi ni suala nyeti sana.
Kwa nini serikali inajiingiza katikati ya biashara za watu??
Nani yupo nyuma ya vurugu hii ya serikali kujiingiza kwenye uchafu huu?
Ni utaratibu gani na mazingira gani hutumiwa kufanikisha hujuma hizi?

Je serikali inaweza kujitoa vipi katika udhamini huu wa Kimafia ili kuwezesha Mahakama kumfikisha Kortin MH Ben na Mkewe Anna kujibu tuhuma za kuibebesha zigo serikali kwa faida zao binafsi??

Ndiyo maana wapambe wa Ufisadi hapa JF wanafoka mapovu midomoni mwao na kushangilia maovu yote???

Kabla ya uchaguzi wa 2010 tutaona mengi.
 
Shida tuliyonayo hapa JF kwenye hii the so called vita dhidi ya ufisadi ni lack of strategies,hatujui kipi tushikilie,tuko hohehahe!
Kabla hata hatuashikilia msimamo wetu kuwa ilikuwa wrong kwa kiongozi mkuu wa nchi kufanya biashara,sasa tunataka kuwa alipe madeni hayo ama afilisiwe kwa kushindwa kuyalipa.
Kiukweli kama hakutakiwa kuwa na biashara akiwa ikulu basi anatakiwa kunyangwanya kila mali aliyojimilikisha isivyo halali ama arudishe mwenyewe kistaarabu.

Ingekuwa afadhali kama hata hiyo biashara ingeendelea na kulisaidia Taifa,wapi,pesa za mikopo zimeliwa na mgodi sijui kama hata unafanya kazi,hivyo huo ni ujambazi,ila hatujui utofauti wake kutokana na vurugu mechi iliyoko...Na ndio maana kuna watu wenye balls za kuufananisha mkopo na wizi wa mchana kweupe ndani ya forum hii,ni maajabu ya mzee Rajabu kuzaa mtoto anaitwa Rajabu.

Cha msingi hapa ni kuwaacha hawa viongozi wetu wastaafu wapumzike,tunachotakiwa kufanya kwa juhudi ni kuhakikisha kuwa Somaiya anatoa hizo miliioni mia nne kwa ajili ya vijana wetu wa uvccm ili waweze kufanya makongamano na kusafiri ili waweze kuona mengi kwa manufaa yetu sote.

Pia tuwe na mshikamano ili tuweze kuifikisha Taifa Stars kwenye kombe la dunia,pia Simba na Yanga,mengine yote tuwaachie viongozi wetu ili tusivunje amani yetu tuliyoizoea kabla hatushinda kombe la Afrika. Mungu mbariki Maximo,JK,Manji,RA na wengine wote wazalendo wenye kulipenda Taifa letu,Simba na bila kusahahu Yanga.
 
Sijui nikiamua kuacha kazi kama nitapata akiba yangu wallah. Kuna kilichobaki huko kweli?

Nadhani serikali inatakiwa kutoa tamko kuhusiana na viongozi kuchukua akiba ambazo hawakuziweka wao. Wafanyakazi wa serikali hawaweki akiba NSSF, inakuwaje wanakuwa na stahili za kukopa kutoka mfuko huo?

NSSF inatakiwa ituhakikishie sisi wateja wake kuwa Balance sheet yao iko sound. Na waache kufanya michezo na pesa za watu. Kama ni kukopesha watu, wangeanzia na wateja wao. Hii DECI style ya kukopeshana na viongozi inaanzia wapi?
 
Poleni sana kwani Nyerere hakuwa mkabila na hakujua kuwa BWM ni machinga

Nyerere alimfahamu BWM kama mlinzi. Si mnakumbuka wakati ule walinzi wengi walikuwa chinga's (Ukichimama nitakua kwa rungu na ukikimbia nitakua kwa nchale, amua mwenyewe) kabla ya kuwaachia wamasai.
 
Shida tuliyonayo hapa JF kwenye hii the so called vita dhidi ya ufisadi ni lack of strategies,hatujui kipi tushikilie,tuko hohehahe! ........ Mungu mbariki Maximo,JK, Manji, RA na wengine wote wazalendo wenye kulipenda Taifa letu,Simba na bila kusahahu Yanga.

Sijapendezewa na hao wawili kuwaombea baraka. Anyway, tumeambiwa tusamehe 70 mara 70!!!
 
kinga ni imla tu tutamshitaki tu dumuzi kabisa huyu. kula mbele na nyuma rasilimali zetu. nakasirika kabisa. ni hasira tu! nguvu ya watz ni kukamata na kumalizia mbali tu ndo kilichobaki. ukipewa kazi na boss ya kurina asali hautakiwi kabisa kula asali bali kulamba mikono yako tu! yeye amesaliti boss wake ambaye ni mtanzania. noma sana. sijui hata nijieleze vipi. ningeweza kumtukana ningemtukanilia mbali
 
Shida tuliyonayo hapa JF kwenye hii the so called vita dhidi ya ufisadi ni lack of strategies,hatujui kipi tushikilie,tuko hohehahe!
Kabla hata hatuashikilia msimamo wetu kuwa ilikuwa wrong kwa kiongozi mkuu wa nchi kufanya biashara,sasa tunataka kuwa alipe madeni hayo ama afilisiwe kwa kushindwa kuyalipa.
Kiukweli kama hakutakiwa kuwa na biashara akiwa ikulu basi anatakiwa kunyangwanya kila mali aliyojimilikisha isivyo halali ama arudishe mwenyewe kistaarabu.

Ingekuwa afadhali kama hata hiyo biashara ingeendelea na kulisaidia Taifa,wapi,pesa za mikopo zimeliwa na mgodi sijui kama hata unafanya kazi,hivyo huo ni ujambazi,ila hatujui utofauti wake kutokana na vurugu mechi iliyoko...Na ndio maana kuna watu wenye balls za kuufananisha mkopo na wizi wa mchana kweupe ndani ya forum hii,ni maajabu ya mzee Rajabu kuzaa mtoto anaitwa Rajabu.

Cha msingi hapa ni kuwaacha hawa viongozi wetu wastaafu wapumzike,tunachotakiwa kufanya kwa juhudi ni kuhakikisha kuwa Somaiya anatoa hizo miliioni mia nne kwa ajili ya vijana wetu wa uvccm ili waweze kufanya makongamano na kusafiri ili waweze kuona mengi kwa manufaa yetu sote.

Pia tuwe na mshikamano ili tuweze kuifikisha Taifa Stars kwenye kombe la dunia,pia Simba na Yanga,mengine yote tuwaachie viongozi wetu ili tusivunje amani yetu tuliyoizoea kabla hatushinda kombe la Afrika. Mungu mbariki Maximo,JK,Manji,RA na wengine wote wazalendo wenye kulipenda Taifa letu,Simba na bila kusahahu Yanga.

Mangi kama ni mbege umekunywa leo, basi imewekwa molases
 
Swali kwako CAG, je mkopo huu ulitolewa baada ya Mkapa na Yona kujimilikisha Kiwira katika mazingira ya kifisadi au kabla!? Hebu tufafanulie zaidi badala ya kumuogopa Mkapa kama Mungu.

CAG akanusha kumtaja Mkapa
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 15th May 2009

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amekanusha kumtaja Rais mstaafu Benjamin Mkapa katika ripoti yake ya Mashirika ya Umma kuwa alitumia vibaya mkopo wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Ludovick Utouh, alikanusha habari zilizoandikwa na gazeti la MwanaHalisi la Mei 13 mwaka huu, kwamba "Mkapa achota NSSF mabilioni ya shilingi na ashindwa kuyarejesha".

"Napenda kukanusha taarifa hii, kwani katika ripoti yangu ya mashirika ya umma kwa mwaka unaoishia tarehe 30 Juni 2008, hakuna mahali nilipomtaja Mheshimiwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

"Katika ripoti yangu hiyo, aya ya 3.2.4 (ukurasa wa 74 hadi 77), nilitaka wakopaji tisa ambao kwa pamoja wamekopa NSSF jumla ya Sh 58,757,794,802 na katika deni lililotajwa na gazeti la MwanaHalisi la Sh 8,127,000,000 linahusu kampuni ya Kiwira Coal & Power Company," alisema.

Aliongeza kuwa kutaja jina la Rais mstaafu Benjamin Mkapa kama mkopaji badala ya mkopaji halali ni kinyume na ripoti yake na huo ni upotoshaji ambao angependa kuukanusha kwa nguvu zote. "Ninaomba vyombo vya habari viwe huru kutumia ripoti yangu kama ilivyo na si vinginevyo, kwani kwa kutoa taarifa kama hiyo, kunapotosha umma na kunaweza kuleta mfadhaiko na chuki kwa waliotajwa isivyo halali," alisema.

Alisema lengo la vyombo vya habari ni kutoa taarifa sahihi bila kuongeza maelezo ambayo yanaweza kusababisha taarifa husika ieleweke visivyo na ni imani yake kuwa umma utaendelea kuhabarishwa juu ya ripoti yake kwa usahihi. "Pale patakapokuwa hapaeleweki, naomba mje ofisini kwangu kwa ufafanuzi, kabla ya kuchapisha taarifa zinazopotosha na ambazo hazielezi yaliyo kwenye ripoti zangu," alisema Utouh.
 
Mangi kama ni mbege umekunywa leo, basi imewekwa molases

Nkamangi,maisha ni mafupi,kunywa mbege ukipata nafasi,ni chakula ya asili.
Hivi wakiweka molases inakuwa vipi?
Kuna wanaokunywa kahawa kila siku,wao ni sober kabisa lakini ndio wanachagua viongozi hao kila kukicha.
Hao wanaokunywa mbege wameichagua ccm? Ama ni mbege ya wapi unaizungumzia?
Cha msingi ni mujue mnachokitaka na si porojo tu,kama ni porojo tu ni bora muwekeze nguvu zenu kwenye shughuli nyingine za kimaendeleo,muhakikishe Taifa Stars inashinda na Yanga na Simba zinafanya vizuri,haya mambo ya viongozi hamuyawezi. Subirini watawaombea pesa kutoka kwa wafadhili wetu wa ndani na nje ya nchi ili kuweza kukijenga chama cha mapinduzi kwani ndicho chenye kudumisha amani.
Ni maoni tu Nkamangi.
 
Natofautiana kidogo hapa kuhusu immunity ya Mkapa kwani sijui mwizi kama huyu anastaili kuwa na Kinga hiyo ambayo inasemwa, kwani kinga haiwezi kumlinda mwizi kiasi hiki.Pia mimi bado namwona JK kama ndiye amempa hiyo kinga kwani huyu Mkapa anatakiwa hajibishwe hata aongee tujue kwamba anasingiziwa au ndio aliamua kuvunja sheria.
Je Raisi wetu aliapishwa kulinda nini na kutetea nini kama hata hizi ambazo ziko wazi ameshindwa .Yeye JK Anajua kutumia kodi ya wanainchi walalahoi kwenye safari zake ambazo hatujui anachofuata.
Hakika inatakiwa sasa sikumoja watu wachukue huamuzi mikononi ili ukweli ujulikane. Lakini kwa hizi story za abunwasi hatutakaa tufike tunakoenda salama.
kweli watanzania bado tunasafari ndefu ya kutokomeza ufisadi ndio tumeanza tu.Lakini hatupaswi kukata tamaa ipo siku itaeleweka tu.
Naamini Mkapa huko halipo usingi haupati vizuri kwani dhambi hizi sinamsumbua kwelikweli ni basi mzigo wa mwizi haubebeki.
 
Kama Mengi angeendelea kutaja hao anaodai mafisadi papa basi Mkapa angekuwa nambari sita kama si wa kwanza labada Mengi hakuwa na ugomvi nae. Maswali yoote haya huyu jamaa kakaa kimya anafikiri watz wanasogeza muda wasahau? anakinga ya kutoshitakiwa lakini hana kinga ya kunyamazia maswali yanayowakereketa watz wote katika kujua wapi zimekwenda rasilimali zao? kazi kwake...

- Hapana magazeti ya Mengi ndiyo yaliyokuwa ya kwanza kumlipua Mkapa, baada tu ya kutoka urais, mambo ya Kiwira na ANABEN yalianiza magazeti ya Mengi na kumfanya Mkapa kuapa kwamba siku ya Mengi inakuja!

Respect.

FMEs!
 
Back
Top Bottom