Mkapa above the law?: Allegations

Mkapa above the law?: Allegations

- Hapana magazeti ya Mengi ndiyo yaliyokuwa ya kwanza kumlipua Mkapa, baada tu ya kutoka urais, mambo ya Kiwira na ANABEN yalianiza magazeti ya Mengi na kumfanya Mkapa kuapa kwamba siku ya Mengi inakuja!

Respect.
IMESHAMJIA MKUU CHA MUHIMU AKAE MKAO WA TAMATI MAANA NGOMA IVUMAYO MKUU WA MEDANI ....

SASA TUSHAMFAHAMU VYA KUTOSHA KUWA YEYE NI NANI NA ANATUMIWA NA NANI.

JAMII ISHAMPUUZA KWANI AMEJINYANG'ANYA MWENYEWE HESHIMA ALIYOTUMIA JASHO LETU JINGI KUJIJENGEA.

MWANAHALISI SI GAZETI MAKINI TENA, NI HERI SASA HELA YA GAZETI HILO TUPATE MKATE WA FAMILIA ZETU.

MKUU WA MEDANI, MENGI NA TIMU YAKE WANAPASWA KUTAMBUA SINGLE IKIPIGWA MFULULIZO INACHUJA, KWA SASA TUSUBIRI TU BACK FIRE KWAO AS TENURE YA HUYO WANAYEDAI KAWATUMA INAPOELEKEA UKINGONI, 2015 SIYO MBALI KWA NAMBA ILA NI WAJINGA TU NDIO WANAOZUZUKA. MENGI 74 YRS OLD ANAJUA ANACHOKIFANYA KWA VIZAZI VIJAVYO LAKINI MUNGU SI ATHMAN KAMA MANDELA KAMUONA ZUMA ANAAPISHWA AKIRITHI MIKOBA NADHANI HAITAKUWA AJABU KWAKE KUMUONA AJAYE.

WASALAAM
 
Sijapendezewa na hao wawili kuwaombea baraka. Anyway, tumeambiwa tusamehe 70 mara 70!!!
Nadhani ni mara 7 Sabini, i stand corrected.....Hata hivyo kwasababu naamini sauti ya umma ni sauti ya Mungu,na watu hao hao ndiyo wanaowachagua na kuwatajirisha hao,(Kina RA nk)kwa baraka za wananchi,Then si Mungu ndiyo kawabariki? Again...I stand corrected....Unless Taifa la Tanzania ni Taifa la Shetani na si Mungu the argument inaweza kubadilika....Ni changamoto....Taifa la Kishetani?
 
- Hapana magazeti ya Mengi ndiyo yaliyokuwa ya kwanza kumlipua Mkapa, baada tu ya kutoka urais, mambo ya Kiwira na ANABEN yalianiza magazeti ya Mengi na kumfanya Mkapa kuapa kwamba siku ya Mengi inakuja!

Respect.
IMESHAMJIA MKUU CHA MUHIMU AKAE MKAO WA TAMATI MAANA NGOMA IVUMAYO MKUU WA MEDANI ....

SASA TUSHAMFAHAMU VYA KUTOSHA KUWA YEYE NI NANI NA ANATUMIWA NA NANI.

JAMII ISHAMPUUZA KWANI AMEJINYANG'ANYA MWENYEWE HESHIMA ALIYOTUMIA JASHO LETU JINGI KUJIJENGEA.

MWANAHALISI SI GAZETI MAKINI TENA, NI HERI SASA HELA YA GAZETI HILO TUPATE MKATE WA FAMILIA ZETU.

MKUU WA MEDANI, MENGI NA TIMU YAKE WANAPASWA KUTAMBUA SINGLE IKIPIGWA MFULULIZO INACHUJA, KWA SASA TUSUBIRI TU BACK FIRE KWAO AS TENURE YA HUYO WANAYEDAI KAWATUMA INAPOELEKEA UKINGONI, 2015 SIYO MBALI KWA NAMBA ILA NI WAJINGA TU NDIO WANAOZUZUKA. MENGI 74 YRS OLD ANAJUA ANACHOKIFANYA KWA VIZAZI VIJAVYO LAKINI MUNGU SI ATHMAN KAMA MANDELA KAMUONA ZUMA ANAAPISHWA AKIRITHI MIKOBA NADHANI HAITAKUWA AJABU KWAKE KUMUONA AJAYE.

WASALAAM

Hivi wewe unamwakilisha nani? Mwananchi wa kawaida?
Ushauri wangu kwako ni kwamba kama una shida ya mkate halafu unatumia pesa yako kwenye internet kuja hapa JF ni ufukara wa kifikra....Kabla haujataka huo mkate wa mwanahalisi kwanini usitafute mkate wako wewe mwenyewe? Taifa gani hili tunajenga!
 
- Hapana magazeti ya Mengi ndiyo yaliyokuwa ya kwanza kumlipua Mkapa, baada tu ya kutoka urais, mambo ya Kiwira na ANABEN yalianiza magazeti ya Mengi na kumfanya Mkapa kuapa kwamba siku ya Mengi inakuja!

Respect.
IMESHAMJIA MKUU CHA MUHIMU AKAE MKAO WA TAMATI MAANA NGOMA IVUMAYO MKUU WA MEDANI ....

SASA TUSHAMFAHAMU VYA KUTOSHA KUWA YEYE NI NANI NA ANATUMIWA NA NANI.

JAMII ISHAMPUUZA KWANI AMEJINYANG'ANYA MWENYEWE HESHIMA ALIYOTUMIA JASHO LETU JINGI KUJIJENGEA.

MWANAHALISI SI GAZETI MAKINI TENA, NI HERI SASA HELA YA GAZETI HILO TUPATE MKATE WA FAMILIA ZETU.

MKUU WA MEDANI, MENGI NA TIMU YAKE WANAPASWA KUTAMBUA SINGLE IKIPIGWA MFULULIZO INACHUJA, KWA SASA TUSUBIRI TU BACK FIRE KWAO AS TENURE YA HUYO WANAYEDAI KAWATUMA INAPOELEKEA UKINGONI, 2015 SIYO MBALI KWA NAMBA ILA NI WAJINGA TU NDIO WANAOZUZUKA. MENGI 74 YRS OLD ANAJUA ANACHOKIFANYA KWA VIZAZI VIJAVYO LAKINI MUNGU SI ATHMAN KAMA MANDELA KAMUONA ZUMA ANAAPISHWA AKIRITHI MIKOBA NADHANI HAITAKUWA AJABU KWAKE KUMUONA AJAYE.

WASALAAM

Fedha atayolipwa Rostam Azizi na Mwanahalisi,wewe na genge lako mtapata mkate wa Familia?Kiishaa ahidi malipo kwa kazi yenu bure na nzuri??Katika ubinafsi wake Rostam ni nani wako??Rostam alipwe hizo Billioni kisha Mnyamwezi fulani kutoka kule Ulyankulu apate cha kuwafanya wanae wapande ngazi za choo???Hii naona imekaa kama Fisi asubirie mkono wa mwenye kutembea shto kulia ukatike apate BreakFast?????????? Du Mtasubiri kweli
 
  • Allowed dubious payments to resume after earlier suspension by predecessor Mwinyi

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE third phase government of president Benjamin Mkapa is understood to have sanctioned fresh dubious payments out of the Bank of Tanzania (BoT) external payment arrears (EPA) account, after the preceding government suspended the predecessor scheme known as the Debt Conversion Programme (DCP).

It has now emerged that the second phase government, under president Ali Hassan Mwinyi, ordered the DCP scheme to be halted effective from June 30, 1993, following revelations of fraudulent payments being made by BoT from that account.

Mwinyi retired in 1995 after serving his second and final term in office. He was succeeded by Mkapa, whose government appears to have then moved to reverse Mwinyi’s decision via the replacement scheme entitled EPA, also administered by BoT.

It is this move by officials in the Mkapa administration that is now traced back as the origin of the subsequent massive looting of EPA funds in 2004/05.

According to latest THISDAY findings, senior officials in the third phase government are also believed to have allowed some of the same people implicated in the DCP scandal a decade earlier, to repeat the fraud and similarly outright theft of taxpayers’ money through the EPA account.

They include controversial businessman Jayantkumar Chandubhai (Jeetu) Patel, who was one of those singled out in the 1994 report of a parliamentary committee formed to investigate the DCP scandal.

The committee was chaired by the then Rorya legislator, Ayombe Ayila.

While Jeetu Patel escaped the police dragnet for the 1993/94 DCP scandal, over a decade later he has been indicted for alleged involvement in the brazen looting of the present-day EPA account.

Our new findings also show that on July 12, 1993, former Zanzibar attorney general Wolfgang Dourado wrote a letter to then president Mwinyi to bring his attention to what he described as fraudulent payments being made through the DCP scheme.

’’I am aware of a case where I strongly suspect a swindle. Millions of shillings are involved. There is therefore a strong possibility that the suspected culprit will be able to have his misdeeds covered up,’’ said part of Dourado’s letter to Mwinyi.

He was referring to the involvement of one V.G Chavda in the DCP scam.

Stated Dourado: ’’The culprit has influential friends and lots of money to throw around. I would not have troubled Your Excellency if the swindle did not involve a loss to Tanzania’s coffers, in both foreign exchange and local currency.’’

His letter served to highlight the alleged fraud and theft of public funds carried out by Chavda, and furthermore advised then-president Mwinyi to suspend the DCP scheme and order an official investigation.

’’When investigations into the DCP scandal are completed, a clear picture will emerge. This will show that the DCP funds were repatriated abroad, instead of being invested on the four farms (owned by Chavda),’’ said Dourado.

’’For the moment, Mr President, it is important to ensure that the accounts in question remain frozen until completion of investigation,’’ he added.

Two months after receiving this letter, Mwinyi gave the order for all payments from the DCP scheme to be suspended.

Similarly, after revelations of the 133bn/- EPA account embezzlement scam were made public, President Jakaya Kikwete swiftly ordered all payments from this account to also be halted.

In the circumstances, it remains unclear why the subsequent Mkapa administration allowed the payments from the erstwhile DCP scheme to resume.

Source:ThisDay
 
Tutaluamu sana mwaka huu; na kulaumu sio suluhisho.

Toeni nini kifanyike, tatizo au wizi umeshatokea, TUFANYE NINI?
 
Tutaluamu sana mwaka huu; na kulaumu sio suluhisho.

Toeni nini kifanyike, tatizo au wizi umeshatokea, TUFANYE NINI?

sheria si zipo? kwanini wahusika hawachukuliwi hatua, vinginevyo tutaendelea kuwapalilia viburi wahusika
 
Lisije libongo limoja likaja na solution ya kupeleka kesi mahakamani!!!

Maana ndo mnaona suluhisho, Ila ni wepesi wa kusahau kuwa SOON LIYUMBA aka "kidume" ataachiwa HURU kwa matatizo yenu ya kupeleka kesi hovyo hovyo bila utafiti mahakamani.

Wabongo wanapenda kuchezewa akili, PCCB wameshawajulia wanapeleka kesi bila utafiti mahakamani mnafurahia kisha watuhumiwa wanaaachiwa huru.

Kalaghabao!
 
sheria si zipo? kwanini wahusika hawachukuliwi hatua, vinginevyo tutaendelea kuwapalilia viburi wahusika

Nilijua tu wabongo ndo suluhisho lenu!!!! KUKURUPUKA! Hamna suluhisho mbadala!, kila siku mnafikiria nani kaiba nini...wataendelea kuiba daima na mtaendelea kubakia masikini milele!, bahati nzuri mie nimeshabadilika sio mlalamikaji tena na toka niache kulalamika nimeona faida yake!

Soma hapo juu.
 
Nipeni tenda niwape suluhisho! Na mimi niwaibie kidogo ingawa nitakuwa nimezifanyia kazi angalau!
 
Yona, familia ya Mkapa matatani
Ni kuhusu Kiwira

Mwandishi Wetu Mei 20, 2009
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

VIGOGO wengine wanaotuhumiwa katika kesi za kifisadi wakiwamo wanasiasa na wafanyabiashara wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa baada ya uchunguzi dhidi yao kukamilika; huku kukiwa na madai ya kuwepo ulipizaji visasi katika uandaaji wa kesi hizo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya serikali na asasi zake nyeti zimethibitisha kwamba kesi zitakazofunguliwa nyingi zitawahusu watu ambao wamekuwa na misimamo tofauti kisiasa na kijamii na watu wenye nguvu hivi sasa ndani ya serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Aidha, miongoni mwa watuhumiwa ambao watafikishwa mahakamani ni wale wale ambao tayari wana kesi zinazowakabili; baadhi zikiwa tayari katika hatua mbalimbali mahakamani.

Raia Mwema inahifadhi baadhi ya majina ya watuhumiwa ambao bado hawajafikishwa mahakamani, lakini wanaotajwa kufunguliwa mashitaka yao na ambao wana kesi zinazowakabili ni pamoja na Daniel Yona ambaye alikuwa waziri mwandamizi katika serikali ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.

Yona, ambaye aliwahi kuongoza wizara nyeti ikiwamo Wizara ya Fedha na Wizara ya Nishati na Madini, tayari ameshitakiwa kwa makosa yanayohusishwa na misamaha ya kodi kwa kampuni ya uhakiki wa dhahabu ya Alex Stewarts Business Assayers ya Marekani, akiwa na wenzake, Basil Mramba aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha na aliyekuwa Katibu Mkuu wake, Gray Mgonja. Mramba na Mgonja waliingizwa katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kabla ya kuondoka na hatimaye kushitakiwa.

Kwa mujibu wa habari hizo, Yona anaweza kushitakiwa sasa akituhumiwa kutumia vibaya madaraka wakati wa mchakato wa ubinafsishaji wa mradi wa mkaa wa mawe wa Kiwira, ambao yeye akiwa Waziri wa Mkapa walihusika katika ununuzi wa mradi huo.

Hata hivyo imeelezwa kwamba Mkapa hatokuwapo katika mashitaka hayo na badala yake wanaotarajiwa kushitakiwa pamoja na Yona na familia yake, watu wanaotajwa kuwa karibu na familia ya Rais huyo mstaafu pamoja na watu wengine maarufu.

Mbali na Yona imeelezwa kwamba mmoja wa watumishi muhimu wa serikali wakati wa utawala wa Mkapa ambaye tayari ana kesi mahakamani ni mmoja wa watu watakaofunguliwa mashitaka mapya yakihusu upotevu wa fedha za BoT. Mtumishi huyo ambaye kwa sasa tunahifadhi jina lake naye anatajwa kuwa mtu wa karibu na Mkapa.

Kesi nyingine ambazo zimeelezwa kuwa katika maandalizi ya mwisho ni ile inayohusu tuhuma za rushwa kuhusiana na ununuzi wa rada ya kijeshi iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa takriban Shilingi bilioni 70.

Habari zinasema serikali imeajiri mtaalamu wa mambo ya sheria kutoka Uingereza ambaye amekuwa akikamilisha maandalizi ya kesi hizo kabla ya kukabidhi mamlaka husika kwa utekelezaji.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwapo kurushiana mpira kati ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuhusiana na mashitaka dhidi ya watuhumiwa wa kesi hiyo, na kwa upande mwingine kati ya watendaji wa serikali ya Tanzania na wapelelezi wa Uingereza kutoka kitengo cha uhalifu mkubwa cha Serious Fraud Office (SFO).

Wanaotajwa katika kesi hiyo ni pamoja na mwanasiasa maarufu aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa miaka kumi, Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge na wafanyabiashara Shaileth Vithlani na mwenzake Tanil Somaiya. Vithlani na Tanil walikuwa wamiliki wa kampuni ya Merlin International Limited, ya Dar es Dalaam, kampuni ambayo inahusishwa na biashara kadhaa na Jeshi la Tanzania zenye utata.

Katika sakata hili yumo pia Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Idriss Rashidi ambaye sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kwa upande mwingine wamo maofisa wa serikali ambao walihusika katika mchakato wa ununuzi wa rada hiyo.

Wachunguzi waligundua kwamba kiasi cha Paundi za Uingereza milioni 12 (takriban Sh bilioni 15/-) kililipwa katika akaunti ya Vithlani iliyopo Uswisi iliyotumika katika kufanikisha biashara hiyo wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa.

Hata hivyo, habari za ndani zimeeleza kwamba sehemu kubwa ya kesi zinazotarajiwa ama zilizokwisha kufikishwa mahakamani ni zile zinazowahusu watu ambao hawana watu wa "kuwakingia kifua" ama wale wanaotajwa kuwa na msimamo tofauti na watawala wa sasa kisiasa na kijamii.

"Angalia wote walifikishwa mahakamani ni wale ambao wana tofauti na watawala wa sasa na wale ambao wana mahusiano mazuri wao wanaendelea kuwa salama hata kama kuna ushahidi wa aina gani. Mimi nimekusanya ushahidi wa kutosha lakini wakubwa zangu wamesita kupeleka jalada mbele," alisema ofisa mmoja wa chombo cha dola.

Ofisa huyo amesema hata baadhi ya watuhumiwa wa kesi za wizi wa fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) waliofikishwa mahakamani ni wale ambao waliwahi kuhusishwa na wanasiasa ambao wanatofautiana na watawala wa sasa ama rafiki zao.

"Angalia Jeetu Patel ambaye pamoja na kuwa amesaidia sana katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005, amejikuta akifikishwa mahakamani huku wenzake waliochukuwa fedha pamoja wakiendelea kuwa salama," alisema ofisa mwingine akiungana na mwenzake kuitaka serikali kutojenga matabaka katika uchukuaji hatua.

Tayari vyombo vya dola vimekuwa vikijenga hoja za kukwama kwa ushahidi kutoka nje ya nchi, huku vikifumbia macho ushahidi wa wazi uliopo nchini ikiwa ni pamoja na taarifa za ukaguzi na za wapelelezi wa ndani zilizothibitisha waziwazi kuwapo kwa jinai katika baadhi ya matukio yanayowahusu watu walio karibu na watawala.

Hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hosea alisema ya kuwa, mwaka jana taasisi hiyo ilichunguza rushwa kubwa 10, na kwamba wanatarajia kufikisha mahakamani kesi nyingine tano kubwa hivi karibuni. Hata hivyo hakuzitaja.

Awali ilielezwa kwamba Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Eliezer Feleshi, alikwishatoa kibali cha kushitaki angalau watuhumiwa watano wakubwa wakati watuhumiwa wengine kesi zao zikiwa katika hatua za mwisho, lakini TAKUKURU na Polisi walipata kigugumizi cha kuziwasilisha kesi hizo mahakamani.

Kumekuwa na taarifa kwamba pamoja na sheria kutolazimisha watendaji kuwasilisna na mamlaka ya juu kabla ya kufikisha kesi mahakamani, kumekuwa na kawaida ya kuwasiliana na mamlaka hizo kwa hoja kwamba, "suala linalohusu haki ya mtu linapaswa kuangaliwa kwa umakini mkubwa."
 
Yona, familia ya Mkapa matatani

Mwandishi Wetu Mei 20, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Ni kuhusu Kiwira

VIGOGO wengine wanaotuhumiwa katika kesi za kifisadi wakiwamo wanasiasa na wafanyabiashara wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa baada ya uchunguzi dhidi yao kukamilika; huku kukiwa na madai ya kuwepo ulipizaji visasi katika uandaaji wa kesi hizo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya serikali na asasi zake nyeti zimethibitisha kwamba kesi zitakazofunguliwa nyingi zitawahusu watu ambao wamekuwa na misimamo tofauti kisiasa na kijamii na watu wenye nguvu hivi sasa ndani ya serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Aidha, miongoni mwa watuhumiwa ambao watafikishwa mahakamani ni wale wale ambao tayari wana kesi zinazowakabili; baadhi zikiwa tayari katika hatua mbalimbali mahakamani.

Raia Mwema inahifadhi baadhi ya majina ya watuhumiwa ambao bado hawajafikishwa mahakamani, lakini wanaotajwa kufunguliwa mashitaka yao na ambao wana kesi zinazowakabili ni pamoja na Daniel Yona ambaye alikuwa waziri mwandamizi katika serikali ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.

Yona, ambaye aliwahi kuongoza wizara nyeti ikiwamo Wizara ya Fedha na Wizara ya Nishati na Madini, tayari ameshitakiwa kwa makosa yanayohusishwa na misamaha ya kodi kwa kampuni ya uhakiki wa dhahabu ya Alex Stewarts Business Assayers ya Marekani, akiwa na wenzake, Basil Mramba aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha na aliyekuwa Katibu Mkuu wake, Gray Mgonja. Mramba na Mgonja waliingizwa katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kabla ya kuondoka na hatimaye kushitakiwa.

Kwa mujibu wa habari hizo, Yona anaweza kushitakiwa sasa akituhumiwa kutumia vibaya madaraka wakati wa mchakato wa ubinafsishaji wa mradi wa mkaa wa mawe wa Kiwira, ambao yeye akiwa Waziri wa Mkapa walihusika katika ununuzi wa mradi huo.

Hata hivyo imeelezwa kwamba Mkapa hatokuwapo katika mashitaka hayo na badala yake wanaotarajiwa kushitakiwa pamoja na Yona na familia yake, watu wanaotajwa kuwa karibu na familia ya Rais huyo mstaafu pamoja na watu wengine maarufu.

Mbali na Yona imeelezwa kwamba mmoja wa watumishi muhimu wa serikali wakati wa utawala wa Mkapa ambaye tayari ana kesi mahakamani ni mmoja wa watu watakaofunguliwa mashitaka mapya yakihusu upotevu wa fedha za BoT. Mtumishi huyo ambaye kwa sasa tunahifadhi jina lake naye anatajwa kuwa mtu wa karibu na Mkapa.

Kesi nyingine ambazo zimeelezwa kuwa katika maandalizi ya mwisho ni ile inayohusu tuhuma za rushwa kuhusiana na ununuzi wa rada ya kijeshi iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa takriban Shilingi bilioni 70.

Habari zinasema serikali imeajiri mtaalamu wa mambo ya sheria kutoka Uingereza ambaye amekuwa akikamilisha maandalizi ya kesi hizo kabla ya kukabidhi mamlaka husika kwa utekelezaji.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwapo kurushiana mpira kati ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuhusiana na mashitaka dhidi ya watuhumiwa wa kesi hiyo, na kwa upande mwingine kati ya watendaji wa serikali ya Tanzania na wapelelezi wa Uingereza kutoka kitengo cha uhalifu mkubwa cha Serious Fraud Office (SFO).

Wanaotajwa katika kesi hiyo ni pamoja na mwanasiasa maarufu aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa miaka kumi, Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge na wafanyabiashara Shaileth Vithlani na mwenzake Tanil Somaiya. Vithlani na Tanil walikuwa wamiliki wa kampuni ya Merlin International Limited, ya Dar es Dalaam, kampuni ambayo inahusishwa na biashara kadhaa na Jeshi la Tanzania zenye utata.

Katika sakata hili yumo pia Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Idriss Rashidi ambaye sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kwa upande mwingine wamo maofisa wa serikali ambao walihusika katika mchakato wa ununuzi wa rada hiyo.

Wachunguzi waligundua kwamba kiasi cha Paundi za Uingereza milioni 12 (takriban Sh bilioni 15/-) kililipwa katika akaunti ya Vithlani iliyopo Uswisi iliyotumika katika kufanikisha biashara hiyo wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa.

Hata hivyo, habari za ndani zimeeleza kwamba sehemu kubwa ya kesi zinazotarajiwa ama zilizokwisha kufikishwa mahakamani ni zile zinazowahusu watu ambao hawana watu wa “kuwakingia kifua” ama wale wanaotajwa kuwa na msimamo tofauti na watawala wa sasa kisiasa na kijamii.

“Angalia wote walifikishwa mahakamani ni wale ambao wana tofauti na watawala wa sasa na wale ambao wana mahusiano mazuri wao wanaendelea kuwa salama hata kama kuna ushahidi wa aina gani. Mimi nimekusanya ushahidi wa kutosha lakini wakubwa zangu wamesita kupeleka jalada mbele,” alisema ofisa mmoja wa chombo cha dola.

Ofisa huyo amesema hata baadhi ya watuhumiwa wa kesi za wizi wa fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) waliofikishwa mahakamani ni wale ambao waliwahi kuhusishwa na wanasiasa ambao wanatofautiana na watawala wa sasa ama rafiki zao.

“Angalia Jeetu Patel ambaye pamoja na kuwa amesaidia sana katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005, amejikuta akifikishwa mahakamani huku wenzake waliochukuwa fedha pamoja wakiendelea kuwa salama,” alisema ofisa mwingine akiungana na mwenzake kuitaka serikali kutojenga matabaka katika uchukuaji hatua.

Tayari vyombo vya dola vimekuwa vikijenga hoja za kukwama kwa ushahidi kutoka nje ya nchi, huku vikifumbia macho ushahidi wa wazi uliopo nchini ikiwa ni pamoja na taarifa za ukaguzi na za wapelelezi wa ndani zilizothibitisha waziwazi kuwapo kwa jinai katika baadhi ya matukio yanayowahusu watu walio karibu na watawala.

Hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hosea alisema ya kuwa, mwaka jana taasisi hiyo ilichunguza rushwa kubwa 10, na kwamba wanatarajia kufikisha mahakamani kesi nyingine tano kubwa hivi karibuni. Hata hivyo hakuzitaja.

Awali ilielezwa kwamba Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Eliezer Feleshi, alikwishatoa kibali cha kushitaki angalau watuhumiwa watano wakubwa wakati watuhumiwa wengine kesi zao zikiwa katika hatua za mwisho, lakini TAKUKURU na Polisi walipata kigugumizi cha kuziwasilisha kesi hizo mahakamani.

Kumekuwa na taarifa kwamba pamoja na sheria kutolazimisha watendaji kuwasilisna na mamlaka ya juu kabla ya kufikisha kesi mahakamani, kumekuwa na kawaida ya kuwasiliana na mamlaka hizo kwa hoja kwamba, “suala linalohusu haki ya mtu linapaswa kuangaliwa kwa umakini mkubwa.”

Tunajua CCM na seriksli yao wana poteza muda ili yasahaulike lakini wakumbuke kwamba hata baada ya miaka 100 mashtaka yatafunguliwa na wajukuu wa akina mkapa na wenzao mali zao zitataifishwa.
 
..Raia Mwema wako reliable sana na habari za Kesi za Mafisadi.

..wametoa hint kuwa kuna kigogo aliyekuwa mtumishi wa serikali wa muda mrefu na tayari ana kesi mahakamani atafunguliwa kesi nyingine. inawezekana ni Mgonja au Chenge.

..hizi kesi zinavyokuwa nyingi namna hii sidhani kama Yona na wenzake watakwepa kutumikia kifungo.
 
Katika sakata hili yumo pia Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Idriss Rashidi ambaye sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ...
Kati ya watu wooote, huyu Idriss Rashidi ndio nasubiri kwa hamu kuona itakuwaje.

Nataka kuona kwa mara ya kwanza katika historia (naomba nisahihishwe hapa) kiongozi anashtakiwa wakati yuko madarakani, sikumbuki hata mmoja. Mgonja alipata clue akastaafu days before the charges were unsealed. Nalaila Kiula sidhani alishtakiwa akiwa Waziri. Hata Mahalu nadhani alitolewa kabla. Chenge, Mramba, Yona, wote hawa ni has been's.

Nataka nione kama kiongozi wa Tanzania atasema ninajiuzulu kwa sababu ya haya mashitaka.
 
Nataka nione kama kiongozi wa Tanzania atasema ninajiuzulu kwa sababu ya haya mashitaka.

- Waziri Ngasongwa, alijiuzulu kabla ya kusitakiwa kutokana na ripoti ya Warioba, iliyowashitaki kina Kiula na Mlingwa ukaribu wake na Mkapa ukam-save na kushitakiwa, baada ya kujizulu mapema.

Respect.

FMEs!
 
Mkapa maji marefu

• Slaa: ‘Tutamfanyia' kama EPA

na Sauli Giliard na Rahel Chizoza

Tanzania Daima~Sauti ya Watu​

NDOTO za baadhi ya Watanzania za kutaka Bunge la Jamhuri ya Muungano limuondolee kinga Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ili aweze kushtakiwa kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka yake na kujihusisha na biashara akiwa Ikulu inazidi kuingia wingu zito baada ya baadhi ya wanasiasa kuweka bayana kuwa jukumu hilo ni la wananchi.

Vuguvugu la kumwondelea kinga Mkapa hivi sasa limeanza kuibuka upya wakati wabunge wanajiandaa na mkutano wa bunge la bajeti ya mwaka wa fedha wa 2009/2010 baada ya baadhi yao kushindwa kuwasilisha hoja binafsi bungeni katika mikutano iliyopita.

Moja kati ya wabunge walioonyesha nia ya kuwasilisha hoja binafsi ya kutaka kiongozi huyo aondolewe kinga ni Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (CHADEMA), na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Jimbo la Wawi, Hamad Rashid (CUF).

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Ndesamburo alisema kuwa hawezi kuipeleka tena hoja hiyo bungeni baada ya kukutana na kujadiliana juu ya mkakati wa kufanya hivyo ambapo inaonekana azma hiyo inaweza kufikiwa bila kuwa na mlolongo mrefu.

Alisema kutokana na vifungu vya katiba vinavyohusiana na suala hilo, ilionekana kuwa bunge haliwezi kufanya hivyo kwa kuwa itahitajika theluthi mbili ya kura za wabunge kitu ambacho si rahisi kwa mazingira ya sasa.

"Ni kweli, nilikuwa na hoja kama hiyo, nilikuwa niitoe bungeni. Tulikuja kukaa na kujadiliana, siwezi tena kuipeleka bungeni. Hata kiongozi wangu, Dk. Wilbrod Slaa, alishasema kuwa Mkapa hana kinga," alisema Mbunge huyo.

Hoja kubwa inayotaka Mkapa kushtakiwa inatokana na kiongozi huyo kutuhumiwa kuhusika na umiliki wa Mgodi wa Uchimbaji wa Makaa ya Mawe wa Kiwira pamoja na waziri mstaafu ambaye kwa sasa anakabiliwa na mashtaka ya kutumia madaraka vibaya na kuliingizia taifa hasara ya jumla ya sh bilioni 10, Daniel Yona.

Tuhuma dhidi ya Mkapa zilishamiri zaidi baada ya mbunge wa la Vunjo, Aloyce Kimaro (CCM), kudai bungeni kwenye mkutano wa 11 kuwa mgodi huo umenunuliwa na kiongozi huyo kwa bei ndogo kuliko ilivyostahili.

Kauli hiyo ya Kimaro na vuguvugu lilikokuwapo lilichochea baadhi ya wanasiasa kuamua kupeleka hoja binafsi bungeni kutaka kiongozi huyo aondolewe kinga ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili lakini wanasiasa hao waliamua kuachana na mpango huo kwa kile walichokidai kuwa Rais mstaafu huyo anashtakika na hana kinga yoyote linapokuja suala la jinai.

Akizungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Karatu, Dk. Willbrod Slaa, alifafanua kuwa iwapo Rais atafanya kosa lisilohusiana na madaraka aliyokuwa nayo, anashtakika kwa mujibu wa sheria na Bunge haliwezi kujadili tena suala hilo kwa kuwa hana kinga yoyote.

"Katiba haiongei chochote kuhusiana na Rais Mstaafu kuwa na kinga kwa makosa ya jinai kwa mujibu wa Ibara ya 36 na hata kama suala hilo lingepelekwa bungeni, asilimia kubwa ya wabunge ni CCM, wasingeweza kumhukumu kiongozi wao, ingawa hana kinga anayopaswa kuondolewa.

"Rais Mstaafu kwa kazi yake hawezi kushtakiwa wala kuhojiwa na mtu yeyote lakini kwa Rais kutumia jina lake kibiashara, ni matumizi mabaya ya madaraka na ni kosa la jinai,"

alisisitiza Dk. Slaa.

Kutokana na hali hiyo Dk. Slaa alisema uamuzi wa suala hilo upo mikononi mwa wananchi kama ilivyokuwa kwa masuala ya EPA ambapo wao wataendelea kulizungumzia suala hilo majukwaani hata kama Serikali itaendelea kukaa kimya.

"Tulipotembelea mikoa yote na kueleza wananchi juu ya ufisadi wa EPA, viongozi wa CCM wakiwemo wabunge, mawaziri na hata Rais walishikiwa mabango ndipo walipoamua kuwapandisha kizimbani baadhi ya watuhumiwa.

"Mafanikio hayo yanatokana na umma kutuunga mkono baada ya kuamini tulichokuwa tukiwaeleza, na sasa tutaendelea kutumia utaratibu huo kwa kuwa tunaamini umma una nguvu," alisema Dk. Slaa.

Aliendelea kusisitiza jukwaa lililo huru kwa mwanasiasa yeyote ni umma huku akisisitiza kuwa mafanikio ya upinzani katika suala la wizi wa Malipo ya nje (EPA) lilichangiwa kwa kiasi kikubwa na mwitikio wa wananchi, hivyo chama chake kitaendelea kuitumia njia hiyo hadi pale ufumbuzi wa kumshtaki kiongozi huyo utakapopatikana.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanabainisha kuwa nguvu ya kutaka kinga dhidi ya Mkapa iondolewe ilipoteza mwelekeo baada ya Ndesamburo kufuta wazo lake la kuipeleka hoja binafsi bungeni ambapo kama ingefanikiwa kuingia bungeni ilitarajiwa kulitikisa bunge na nchi.

Wachambuzi hao waliendelea kuwa Tanzania imeonekana kushindwa kufuata nyayo za nchi jirani ya Zambia ambayo chini ya utawala wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Hayati Levy Mwanawasa, ulifanikiwa kumpandisha kizimbani Rais aliyetangulia, Fredrick Chiluba, kwa tuhuma za ufisadi mara baada ya kuingia madarakani.

Hata Rais Jakaya Kikwete alipohojiwa juu ya kuwa tayari kumpandisha Mkapa kizimbani kama ilvyotokea huko Zambia, alinukuliwa akisema kuwa ni vema mstaafu huyo akaachwa ampumzike kwa kuwa amefanya kazi kubwa ya kuijenga nchi.

Katika hatua nyingine Dk. Slaa ameendelea kuilaumu serikali kwa kitendo chake cha kutochukua maelezo ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), marehemu Daud Balali, enzi za uhai wake juu ya tuhuma za wizi wa mabilioni katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) na kusema kuwa kutaathiri mwenendo mzima wa kesi za EPA zinazoendelea.

Alisema hali hiyo imekuwa ikisababisha baadhi ya kesi hizo kukosa ushahidi japokuwa hati zake zilipitiwa na wataalamu wa sheria akiwemo Mkurugenzi wa Mashtaka, Elieza Feleshi, jambo linaloashiria kuwa huenda watuhumiwa hao wakaachiwa huru.

"Tatizo hapa ni kukosekana kwa maelezo ya shahidi muhimu ambaye ni Balali. Huyu ndiye aliyeidhinisha malipo yote zikiwemo folio namba 14, 24, 28 na 35 ambazo ziko BoT. Nashangaa kwa nini hili halikufanyika wakati pale Muhimbili kuna wagonjwa waliolazwa na pingu mkono na wanachukuliwa maelezo yao," alisema Dk. Slaa.

Aliongeza kuwa kutokana na udhaifu juu ya uendeshaji wa kesi zinazohusiana na wizi wa EPA, kiongozi huyo ameapa kuwa wataendelea kufuatilia suala hilo pasipo kuingilia uhuru wa mahakama na kujitapa kuwa hakuna wa kuwazuia kwa kuwa wanapigania mali ya umma.

Mwenendo wa kushughulikia tuhuma za ufisadi hasa uliofanyika katika Serikali ya Awamu ya Tatu umekuwa ukitiliwa wasiwasi na baadhi ya wanasiasa na wananchi kwa kueleza kuwa ni kiini macho huku wengine wakidai kuwa waliotuhumiwa ni ‘dagaa' wakati vigogo wakiendelea na shughuli zao za kila siku.
 
Mtamuua huyu Mzee wa Watu.

Simuungi mkono kwa mabaya aliyofanya. Ila nafikiria kuwa angetubu makosa na arudishe kila kilicho chetu na kisha aachwe apumzike.

Kuna mengi mazuri alifanya lakini binadamu ndiyo hivyo tena, wengi hatutosheki.
 
Back
Top Bottom